nkosikazi
JF-Expert Member
- Mar 11, 2010
- 361
- 337
Ni mara nyingi sana Sitta amekuwa akipingana na msimamo wa serikali ambayo yeye ni mmoja wa viongozi wake waandamizi. Amekuwa akifanya hivyo openly kabisa kwa kwenda kwenye vyombo vya habari na kuipinga na kuikosoa serikali.
Hivi karibuni Amiri Jeshi Mkuu, ambaye pia ndiye rais wa nchi ameagiza wahamiaji haramu waondolewe hapa nchini. Naamini hili limefanikiwa vizuri sana. Ajabu anatokeza mheshimiwa Sitta na kulikosoa zoezi lililoanzishwa na Boss wake mbele ya vyombo vya habari! Si mara ya kwanza wala ya pili bali ni mara ya kumi sasa akiwa tofauti na msimamo wa serikali na pia chama chake. Iliwahi kutolewa hoja na kina Mgeha kuwa Sitta afukuzwe uanachama, lakini hii hoja haikushika kasi na bado Kikwete ameendelea kumkumbatia. Kwa kweli sijajua mantiki ya kuwa na kiongozi kama Sitta kwenye baraza la mawaziri. Ningelikuwa Kikwete ningeisha mtema siku nyingi sana! Anaidhoofisha sana taasisi ya uwajibikaji wa pamoja. Pia anaidhoofisha sana taasisi ya Urais. Hili Kikwete halioni?