lifeofmshaba
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 867
- 219
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Msaidizi Mtendaji Mkuu wa Uongozi Institute, Linda Manu baada ya kuzindua bodi ya chuo hicho jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Ritva Koukku-Ronde, Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia na Balozi wa Finland, Juhani Toivonen
Katika pita pita yangu kwenye vyombo vya habari leo nimekutana na habari ya kusikitisha sana,
Raisi Kikwete ameanzisha taasisi ya kuwafua (shule/chuo) viongozi ili kupa viongozi WENNYE MAADILI
nilipigwa butwaa na hii habari, kwa sababau zifuatazo
- je maadili yanaweza kufundisha kwa kiongozi vyuoni au ni utashi wa mtu?
- Ni nani serikali mwenye maadili ya kutosha kufundisha wengine huko serikali?
- lakini pia hii ni ishara kwamba kikwete hajui nini chanzo cha viongozi wake pamoja na yeye kutokuwa na maadili?
- je TAKURUKU wanafanya kazi vya kutosha na wanameno? na jeshi la polisi na tume ya maadili ya viongozi wameshindwa kazi hii ya kuwanyoosha?
- kwa nini kikwete anataka kuendelea kufanya kazi na viongozi wasio na maadli kuhasi cha kuwapeleka shule
- Kikwete anaogopa nini kutumia sheria zilizopo kuleta maadili ya viongozi, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha wanapokosea
- huu ni upotezaji wa pesa kwa kuwalipa watakaotoa somo kwa hao viziwi na kuwalipa posho watakaudhuria hiyo semina
hii ni pamoja na ukweli kwamba yeye ni chanzo kikuu cha viongozi hao kutokuwa na maadili kwa kuwa dhaifu katika kutoa maamuzi magumu, lakini pia rushwa na uongozi wa kupeana bila kujali sifa na anayepewa ili yeye ni mwanzilishi / mwasisi
Maadili ya viongozi uwezi kuwafundisha kwa semina au washa wengi wao ni wasomi katika taaluma zao wameshafundishwa maadili kinachotokosekana serikali kwa sasa ni uzalendo na mfumo mbovu wa uongozi wa uwajibikaji na uwajibishwaji mfano wiki iliyopita raisi Kikwete alimchagua Mrindoko kuwa Naibu waziri wa wizara ya maji, lakini huyo huyo Mrindoko ni zao la ufisadi na mmoja ya watanzania aliyeifikisha TANESCO hapo ilipo sasa na kuliingiza taifa pamoja na TANESCO hasara kubwa. Je ili nayo Kikwete anataka wakasome shuleni,
Maadili ya viongozi hayajengwi na semini wala washa yanajengwa na shirie kali zinazotekerezwa na kufuatwa, ni lini tumejaribu kutumia sheria kuwasukuma viongozi wetu kuwa na maadili ikashindikana?
Kwa nini tunawabembeleza sana viongozi wan chi hali taifa likiwa na wasomi rukuki waliotayari kulitumikia taifa lao
Kikwete kwa ili umeshemsha tena, naona bado ujajua tatizo ni nini?
Tatizo ni wewe kupindisha na kuchezea sheria za nchi kama ulivyofanya kwa wezi wa EPA, na kamwe utopata viongozi makina na wazalendo, maadili yanaalia ikulu na uzalendo ni ndio kiini pekee za maadili.
Futa hayo mafunzo yako hakuna kitu hapo ni matumizi mabaya ya pesa tu.