Kwani unataka akakiri mara ngapi zaidi ya kukusanya vyama vyote vya upinzani kwa upande wa CCM?
NCCR-Mageuzi, chama mwana-mpotevu, sasa kimerudi rasmi tena bila kificho nyumbani kwa baba yao wa UFISADI mheshimiwa CCM sawa tu na wenzake UDP, DP, TLP na CUF na tangu sasa wananchi kote nchini sasa tunaelewa leo kuliko hapo jana kwamba chama cha kweli cha upinzani chenye kubeba matumaini ya WaTanzania kujinasua toka lindi la UFISADI ni chama gani - jibu zuri unalo wewe hapo!!
Lakini kosa kubwa analolifanya ni kule kujisahaulisha kwamba vyama hivyo siku nyingi sana havina wanachama hai zaidi ya kuwa simba mkali ndani ya ki-brief case ya huyo huyo mbebaji na familia yake (Cheyo, Mrema, Lipumba, Mtikila aka Mzee wa loose balls na sasa Mbatia).
CDM ongezeni kasi kupitia M4C kila kona ya nchi hii maadam ANTIREFORMISTS sasa wameamua kurundikana pamoja bila kificho tena mchana kweupe wanafiki wote haoooo!!