Kikwete amekwama mara 7

wandugu,hakuna kitu kibaya duniani kama NJAAAAAAAAAAA.
Huyu mwenye thred amezidiwa na njaa ameamua kuuza utu wake na hivyo ameleta hisia na chuki za mabwana zake hapa jamvini.
hii tabia ni sawa na simba mwenye njaa,ambaye huwa hachagui chakula,chochote kinachojitokeza mbele,hata mwanae,yeye anatia mdomoni.sasa huyu jamaa yeye anaropoka tuuuuuuuuuuu ilimradi amesema na amemridhisha na kumfurahisha BOSS WAKE.
Lakini sishangai kwa sababu hata YESU NA MUHAMMAD pamoja na mitume wengine waliokuwa wasafi na walihubiri neno la mungu nao walipingwa, sasa kwanini kikwete akose wabaya na wenye husuda wakati waliokosa nafasi pale magogoni 'WALIOTOSWA' bado wanaishi na wanatamani wangekuwa pale.tuache upotoshaji usio na maana.
 
kushuka kwa sarafu ya tanzania dhidi ya dola ni tatizo la kidunia,fanya utafiti kidogo ktk nchi 5 duniani kama hujaaibika,utakuta sisi tuna nafuu kubwa.hutakiwi kuwa mlalamikaji,unatakiwa ku provide slution for problems bro,mbona una tuangusha/great thinker gani ww?
 
memwaga pumba bila ushahidi wowote, ngoja nikupe ushahidi kuwa Kikwete Rais, bora.

Tanzania kwa mara ya kwanza kabisa imepata tuzo ya Utawala bora kutoka Umoja wa Mataifa, ulishasikia tuzo kama hiyo kabla ya Kikwete?

Halafu kwa mara ya kwanza Tanzania imepanda chart ya Kuishi, kama afya haijaimarika tu genpa kutoka kuishi miaka 50 mpaka kufikikia 56 kwa kipindi kifupi cha Kikwete? jiulize.

Mengine yote uliyoandika ni pumba tupu. Nioneshe moja tu ambalo Kikwete hajafanya zaidi ya Rais mwingine wowote wa Tanzania. Nnakuhakikishia hauna.
Nawaonea huruma wanao......
 
Aibu!
Kuna mtu aliuliza swali hivi hakuna watu wa TISS wanaoitakia mema nchi hii?

Kwahiyo ndo tufanyeje cye wananchi unapopoteza muda kubuni hadithi za hekaya kama hizi unatunga na hadithi nyingine ya kufurahisha juu ya nini cha kufanya paka shume weee!!!
 
mimi sioni unalolilalamikia hapa kwani CCM ipo na nguvu zake, serikali ipo na inaendelea kuongoza. Staili ya kuongoza ya JK inatofautiana na ya wengine na unaweza kuwa huipendi.

JK hagombei tena hivyo ni vyema tuzungumzie wagombea watarajiwa kama wenzetu wa USA wanavyofanya kwa uhuru otherwise kujadili topic hii ni kupoteza muda
 
Nawaonea huruma sana wana CCM!Wanashabikia hata upuuzi alimradi watetee chama!
Wana maisha magumu lakini wako tayari kuuza "vitumbua vyao" kwa kinamama na hata "tigo zao" kwa kinababa ili tu wapate nguvu kidogo za kuendelea kutetea maovu kwenye hii nchi!
Ole wao,maana baada ya siku si nyingi "vitumbua" vitalegea na "tigo" zitapoteza network!Tazama,siku hizo watalia na kusaga meno!
 
Kumbuka, huko unakopataja kote nend kaone maendeleo, Bagamoyo, kwa mfano leo kuna chuo kikuu, kuna viwanda vikubwa sana, kuna kiwanda cha chuma kinajengwa (nadhani umekiona kama unapita njia hizo) Kikubwa katika Afrika Mashariki.

Wewe ulie mjini, unaweza mpaka kuwa na muda wa kuja kubishana JF, kama siyo neema hiyo ni nini?

Hakuna kimoja mmeweza kukitaja ambacho Kikwete hajafanya zaidi ya Rais mwingine wa Tanzania. Nnawaambia hamna, mtabaki porojo za kubuni tu.

Naomba soma nilichoandika vizuri, nakubali maendeleo yako huko mpaka hata kule kwetu, nilichouliza hiyo tuzo tuliyopewa ina faida gani kwa wtu hao? ama unataka kusema iliambatana na pesa ndizo zimejenga hayo uliyoyataja? Ningekubali tu kutaja maendeleo lakini hiyo tuzo haina maana yoyote kwetu, ama unataka kusema hata leo hii akitunukiwa nishani ya shujaa mstahiki kwetu ni faida? Na nimekwambia mpaka sasa hajaitangaaza Chalinze kuwa Wilaya, ama tusubiri mpaka 2014? Kumbuka wenzake walifanya kwao, unasemaje hili?
 
Back
Top Bottom