Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MTIHANI NI ULE ULE "JK" ALIREMBA MWANDIKO MUDA HAUKUTOSHA AKAFELI, JPM HASOMI INSTRUCTIONS ATAFELI VIBAYA ZAIDI
Wakati Nasoma enzi hizo mwalimu wangu alikuwa akinisihi nisome kwa bidiii sana ili niweze kufaulu mitihani yangu! Na kila wakati ambapo mitihani ilikaribia alikuwa akinikumbusha Mambo mawili makubwa tena yeye alikuwa akiyasema mambo hayo kwa lugha ya kingereza tena Kingeza cha mkoloni kilichonyooka "Time is part of the exam" kwamba Muda ni sehemu ya Mtihani" Alikuwa akinisihi sana kuzingatia Muda na Mara zote aliniambia ili kuwahi muda "Anza na swali rahisi"
PILI alinisihi sana tena kwa msisitizo mkubwa kwamba Kabla ya Kuanza kufanya mtihani wangu basi NISOME MAELEKEZO hata kama Mtihani ni rahisi namna Gani! Kama ilivyo hulka yake alisisitiza jambo hili kwa lugha ya malkia uingereza "Instruction is the main question of the exam" kwamba Malekezo ni swali la msingi kwenye Mtihani"
Hata Tulipokaa katika Chumba cha mtihani huku tukiwa kimya Kabisa wengine wakitetema kwa woga na wengine wakiwa na Haraka ya Kutaka kujibu maswali ili wasisahau yale waliokariri Msimamizi wa Mtihani, alitusihi sana tusome Maelekezo!
Mambo haya Mawili sikuyasahau Kamwe katika Maisha yangu yote ya Kimasomo na Pia nimeona umuhimu wake katika Maisha yangu ya kawaida baada ya Kumaliza masomo!
Kuzingatia Muda na Kusoma maelekezo imeendelea kuwa mambo ya msingi zaidi ya ile table ya 10 kwani haya mambo mawili yanatumika zaidi kuliko kumi mara Kumi au ile formula ya "pai D Skwea"
"Anyway back to the topic"
Ninavyoamini mimi Uongozi ni sawa kabisa na Mtihani kwani vipengele vyote vya mtihani vinafanana kabisa na Vipengele vya uongozi japo muktadha unaweza kuwa tofauti! Nikivitaja vichache kama vile 1. Muda, Uongozi una Kikomo cha muda na Mtihani pia una ukomo wa muda, 2.Uongozi unaambatana na Matarajio ya Kipimo cha Uwajibikaji na Utekelezaji Mtihani Unambatana na kipimo cha Uelewa na Umakini.
Kwa mantiki Hiyo unapokuwa Kiongozi lazma utambue kwamba Una mtihani wa kuukabili mbele yako na ni wajibu wako kuufaulu ili kutimiza mategemeo ya waliokuchagua.
JK Alipoingia madarakani 2005 alianza mtihani wake vizuri Tena kwa Matumaini makubwa yenye Ari Nguvu na Kasi iliyojenga imani ya matokeo ya maisha bora Kwa kila Mtanzania,
Kilichomponza Mtahiniwa Huyu "JK" alisahau Kuanza na Maswali rahisi "Hakuseti Priorities" Akaanza kufanya swali alilokutana nalo kwa mpangilio wa mtihani, Kwa bahati mbaya Maswali hayo yalikuwa Magumu na yenye maksi Ndogo!
Pia kasi yake katika KuyakabiLi maswali ilikuwa hafifu hasa ukizingatia hulka yake ya Kuremba Mwandiko, Akajikuta anajibu maswali machache kwa Muda mrefu!
Alianza na Barabara, Akahamia shule za kata, Akaleta walimu wa Voda Fasta, Muda ulivyoanza kuyoyoma Akapaniki Akajikuta Anafuta physics akachanganya na Chemistry, Akajenga Njia tatu Dar, Akaifanya Chimwaga Kuwa "UDOM" Akasajili wanachuo zaidi ya Laki, Bodi ya Mikopo Ikashindwa Kuwakopesha, akachanyikiwa Akamua Kutoka Nje! Akakutana Na 50cent Akapiga nae selfie! Alipostuka muda umeyoyoma zaidi Akaingia na Chabo la "eskro" msimamizi akamdaka Akaomba msamaha Akarudi kwenye "EPA" sory ni Pepa akaanza na swali la Mwendo kasi, Akafanya na La kipenyo daraja Kigamboni, Yakajengwa Majengo Marefu, Ukaanzisha Taasisi ya Usimamizi wa Mifuko ya hifadhi ya Jamii, akapunguza Kodi ya mshahara na kujenga Misingi ya Kufikia asilimia 9% Akaongeza Kima cha Chini cha mshahara, Msimamizi Akataja Muda uliobaki akapaniki Tena Akasahau swali la Afya, akarukia Katiba akalikosea akafuta, akarukia Vitambulisho vya Taifa akasahau Formula, akapiga chabo china kwa Ujira wa Gesi akasoma vibaya Jibu Akapeleka Gesi Bagamoyo, Wa mtwara wakaandamana, akapiga chabo kwa dangote, Hakuliona Swali la TRA na Bandari Swali rahisi kwenye Jibu la Kodi, Akastuka Kusikia Muda Umekwishaaaaa huku daftari la Kura hajandika JINA, Msimamizi Akamuuliza unampendekeza Nani akusaidie hii practicle? Akajibu haraka haraka "Benadi" Ikasikika Sauti ya Mkufunzi "Mkaahapa" atakusaidia "Magu", Mtihani Ukakusanywa JK akawa amefeli, waliomtegemea wakamlaumu, wakahisi Hakufanya Kitu, Kumbe alifanya vingi ila Maksi hazikutosha Kufaulu, hakufeli kwa Eti kwasababu alikuwa Hana Uwezo La hasha! ALIFELISHWA NA MUDA!
JPM akaingia Kuokoa Jahazi kwenye "PEPA two" Alijua Mwenzie Kafeli kwa sababu Ya Muda" Haraka haraka Akaanza practictal Tena practical ya Kutumbua, Basi anatumbua Kwa kasi Huyooo! Akateua Team ya wasaidizi, "MASIKINI HAKUSOMA MAELEKEZO " Kumbe Majipu yana ambukiza, mtihani Hakuwa kuyatumbua bali kwani Utasambaza Vimelea Bali ilikuwa ni Kutafuta dawa ya Kimfumo ili Kutibu jipu bila hata Kutumbua na kumaliza Kabisa Vimelea!
MASKINI kayatumbua Hadi Timu ya Wasaidizi Wote nayo imeota Majipu! ALIPOJUA TUNAMUANGALIA akafunika Vioo tusione Kinachoendelea Maabara! TUSUBIRI MSIMAMIZI ASEME MUDA UMEKWISHA! Hofu yangu Ni kwamba Inawezekana Hata Msimamizi Nae akapatwa na Vimelea Hivyo na Hatimae Asikumbuke Kabisa Kuhusu Muda! Na Ikitokea Mtahiniwa Huyu JPM akafeli Basi Atafeli Mara Mbii zaidi ya Mwenzie Kwani Teyari Keshakosea Swali HAKUSOMA MAELEKEZO! - Naitwa Rahymes Msahihishaji wa Mtihani TUKUTANE WAKATI WA MATOKEO!!