Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,903
Kipindi kile, ingawa ulikuwepo ukosoaji wa aina ya utawala uliokuwepo , kikwete alikua sahihi katika yale aliyoyafanya. Ukimpa nafasi ya kujieleza kutokana na yale utakayoyaona kama alikosea, atakupa maelezo na unaweza kumwelewa kua alikua sahihi.
Ni kweli kwamba kwa kanuni zetu za kibinadamu, hakuna mtu aliyekamilika, na yeye analifahamu hilo na atakiri kabisa kuwa baadhi ya maeneo alikosea.
Inawezekana kabisa, kwani hata kiongozi mkubwa kabisa wa Taifa hili Nyerere, alikiri kua kuna baadhi ya makosa aliyafanya, na akashauri tujiepushe kuchukua yale mabaya yake, tuchukue mazuri, hapo ubinadamu umekamilika.
Sasa Magufuli naye, jinsi anavyoendesha mambo yake, wengi tumevutiwa nae, na tunaona yupo sahihi kwa kiwango kikubwa, lakini kama binadamu kuna anayokosea na yapo pia yale ambayo atakosea, ni hulka ya kibinadamu hakuna mkamilifu.
Hivyo si ajabu sana kuona akikosolewa sasa hata baadae pia, maana sisi tumeumbiwa ukosaji, hatu wakamilifu.
Kinachohitajika ni kujaribu kupunguza makosa, na hayo yanafanyika kwa kuchagua timu ya watu weledi watakaotenda mambo kwatika ubora kulingana na uwezo wetu.
Tukumbuke kwamba hili ni taifa changa na bado halina uwezo wa kufanya kila kitu kwa ukamilifu, kwa hivyo hakuna kiongozi atakayeweza kutimiza kila kitu, hata wazazi pia nyumbani hawana uwezo huo, mwenye uwezo huo ni Mungu pekee, kwani ndiye mkamilifu na mweza wa yote.
Sasa sioni ni kwanini tuone huyu amekosea sana, na yule yupo sahihi zaidi wakati nyakati ni tofauti.
Kitabu cha kale kimepita na mambo yake, iwe ukamilifu na upungufu, na kitabu kipya kinaandikwa kikiwa na ukamilifu na upungufu wake.
Siku njema.