Kikwete Alidanganya - Mwanahalisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Alidanganya - Mwanahalisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaHabari, Sep 12, 2008.

 1. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale ambao hawajasoma hii bado.

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa hujui kama ni mwongo na msanii wa kutupwa?. Mapesa ya EPA yanamgusa mkuu wa kaya kwani ndiyo yaliyompeleka IKULU.
   
 3. Tonga

  Tonga Senior Member

  #3
  Sep 12, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ndio maaana anajikanyaga, anakwenda mbele anarudi nyuma yetu macho,
  akija kwa Bush anamlamba kisogo kuwa anashughulikia mambo kikamilifu ili azidi kupewa misaada...atacheza marktime na hii issue ila ukweli utafichuka tu, hili zali halitakufa kiholela limeturudisha nyuma miaka 10 kimaendeleo...hata Mungu hataacha uovu huu uendelee kuizika Tanzania katika dimbwi la umaskini.
  Aluta Continua mapambano bado yanaendelea ndio kwanza kumepambazuka.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,208
  Trophy Points: 280
  Huyu fisadi Rostam Azizi anaiangamiza nchi yetu akishirikiana na mafisadi waliokuwa madarakani

  Na Saed Kubenea
  May 14, 2008

  MAKAMPUNI ya kuzalisha umeme ya Richmond na Dowans yanamilikiwa na mtu mmoja, MwanaHALISI limegundua.

  Vyanzo mbalimbali vya taarifa ndani ya serikali vimekiri pia kwamba hayo ni makampuni ya mfanyabiashara mmoja mashuhuri raia wa Tanzania.

  Kupatikana kwa taarifa hizo kumefuta madai ya baadhi ya viongozi nchini waliokuwa wakisema kuwa Dowans ni kampuni iliyosajiliwa nchini Costa Rica, Marekani Kusini.

  Lakini taarifa zinasema kuwa serikali imethibitishiwa na Mwanasheria Mkuu wa Costa Rica kwamba nchini humo hakuna kampuni inayofahamika kwa jina la Dowans.

  Aidha, imefahamika kuwa akaunti za kampuni ya Dowans, ambayo mfanyabiashara Rostam Aziz amewahi kukiri kufahamiana kibiashara na maofisa wake, ziko Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu.

  Taarifa hizi zimeleta mshangao na maswali mengi, kwani wachunguzi wa mambo wanauliza, kama akaunti ziko Dubai, nani amekuwa akikusanya fedha kila mwezi kwenye dirisha la hazina.

  Vyanzo vya habari vya gazeti hili vinasema wafanyakazi wa kampuni ya mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam ndio walikuwa wakikusanya fedha hizo.

  "Ilifikia mahali kigogo mmoja wa Hazina akawasiliana kwa barua na Ikulu kueleza nani hasa alikuwa anaagiza au kukusanya fedha hizo, na wakati mwingine kuleta rabsha pale anapocheleweshewa malipo," vimeeleza vyanzo vya habari.

  Kupatikana kwa taarifa kuhusu makampuni haya kunaondoa utata, siyo tu juu ya umiliki wake bali pia nani amekuwa akichota mamilioni ya shilingi kutoka hazina kugharimia mradi huu.

  Kwa karibu miaka miwili sasa, mmiliki wa makampuni haya amekuwa akikinga Sh. 152 milioni kutoka Hazina kila mwezi kama gharama za mitambo bila kujali kama umeme umezalishwa au haukuzalishwa.

  Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri unaoanza tarehe 10 mwezi ujao, unatarajia kuelezwa ugunduzi huu wa mmiliki wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda atakapokuwa anatoa taarifa ya serikali ya utekelezaji wa mapendekezo ya Ripoti ya Kamati ya Dk. Harrison Mwakyembe.

  Ni katika mkutano huo wa Bunge, Pinda ataorodhesha hatua zilizokwishachukuliwa na serikali katika kutekeleza mapendekezo 23 ya Kamati ya Mwakyembe.

  Moja ya hatua ambazo zinatarajiwa kutangazwa ni ile ya serikali kutekeleza maoni ya Kamati ya kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah.

  Taarifa kutoka serikalini zinasema Hoseah ataondolewa kwenye nafasi yake kabla ya Mkutano wa 12 wa Bunge kuanza mjini Dodoma.

  Kamati ilipendekeza Hosea awajibishwe kwa sababu alilitia aibu taifa kwa kutoa taarifa potofu kuhusu mkataba kati ya serikali na Richmond.

  TAKUKURU ilisema kwamba mkataba wa Richmond haukuwa na matatizo na kwamba serikasli ilikuwa haijapoteza lolote katika kuwa kwenye mkataba huo.

  Mwingine ambaye anatarajiwa kung'olewa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Athur Mwakapungu ambaye anaponzwa na kushiriki kwake katika mchakato mzima wa kutoa zabuni kwa Richmond na kuficha ukweli kwa Kamati ya Mwakyembe.

  Taarifa zinasema huenda Mwanasheria mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika akasalimika kutokana na mfumo wa utendaji ndani ya ofisi yake. Haikuelezwa zaidi.

  Hata hivyo imefahamika kuwa baadhi ya watendaji katika ofisi hiyo watawajibishwa kutokana na kushiriki kwao katika mchakato mzima wa mkataba huo.

  MwanaHALISI limedokezwa kwamba, kwa sasa serikali inafanya taratibu za kisheria kuona namna ya kusitisha malipo hayo ambayo tafsiri yake ni kuvunja mkataba na Dowans.

  Uamuzi huo wa serikali umechochewa na taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Costa Rica kwa Kamati Teule ya Bunge kwamba nchini humo hakuna kampuni inayoitwa Dowans.

  Dowans ambayo imekuwa inadaiwa kusajiliwa Costa Rica iliingiza ndani ya nchi mitambo kutokea Afrika Kusini huku akaunti zake zikiwa Dubai.

  Katika uchunguzi wake, MwanaHALISI imebaini, serikali kwa kupitia Timu Maalumu (Task Force) iliyoundwa na waziri mkuu, pamoja na mambo mengine, ilipitia mkataba kwa kina na kuona namna ya kusitisha malipo kwa Dowans.

  Tayari serikali imefungua akaunti maalum kwa ajili ya kuhifadhi fedha ambazo zingekuwa zinatiririkia kwenye mikono ya Dowans hadi "kieleweke."

  Bunge la bajeti linatarajiwa kuanza Juni 10 huku joto la kisiasa nchini likiwa juu, kufuatia tuhuma mbalimbali za ufisadi na mawaziri kuendelea kujiuzulu kwa tuhuma hizo.

  Katika mkutano wa 10, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na wenzake Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, walijiuzulu kutokana na mkataba wa kifisadi wa Richmond/Dowans.

  Hata hivyo, waziri mkuu amethibitisha kuwa viongozi wote waliojiuzulu, wanafuatiliwa kwa makini ili kujua walivyohusika katika kashfa za ufisadi.

  Pinda alikuwa akiongea na waandishi wa habari, juzi Jumatatu juu ya hatua za serikali katika kutekeleza mapendekezo ya kamati ya bunge. Alisema fikra za serikali ni kwamba "haitoshi kwa viongozi hao kujiuzulu."
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hii mimi naiita ni thubutu kuu lenye ujasiri wa hali ya juu lifananalo na kupapasa pumbu za Simba.
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...muhimu hapa ni kwa mpapasaji kujua amevaa gloves au anatumia tongs!!
   
 7. A

  AeIoU Member

  #7
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Huyu mkuu wa kaya yetu sidhani kama ajajua kitu anachofanya pale ikulu. Imeonekana kwamba hana msimamo na hata mamlaka na jambo hata moja. Ila juzi alijitahidi kumpiga tafu nape kwa kuwa anakumbuka zile fadhila za mzee nauye, mkuu wa kaya alipokuwa katibu wa ccm singida miaka ya sabini mzee nauye alimpiga tafu sana na kumpandisha chati hadi akaanza kujukikana kwa viongozi wa juu na kuaminiwa. Hivyo isingekuwa rahisi kumtosa kabisa kwani ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA.
   
 8. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #8
  Sep 12, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nilisha andika katika maoni tofauti kuhusu ufisadi uliotokea na unaoendelea tunaendelea kuawtafuta wakina Lowassa,Karamangi Rostam,Chenge,Mkapa na wengine wengi tunashindwa kuelewa ya kua hawa mafisadi(WEZI) ni system au circle au mduara ambao haukamiliki bila Kutaja Mh.Rais Kikwete.Anajua yote kwa kina nini kilichotokea na yeye mwenyewe kama mshiriki mkuu ndio maana wakati wote ana kigugumizi katika kutoa maamuzi kuhusina na ufisadi.Jitihada zetu za kuwatafuta mafisadi kwa kuwatafuta akina Rostam n.k nisawa na kutaka kupata umeme wakati waya kuna kipande kilichokatika.Ili mzunguko wa umeme ukamilike hapa kipande cha waya kinachokosekana ni Mh.Jakaya kikwete tukiisha kiunganisha tutapata umeme yaani picha halisi kuhusu ufisadi umefika wakati wa koleo kuliita koleo vinginevyo we beating around bush!MUNGU IBARIKI TANZANI
  Advocate Jasha.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi kuna tusichokijua katika vicious circle of ufisadi? sasa tunapaswa kuchukua hatua tu
   
 10. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Cha msingi hapa ni kuwa pesa haikuwa ya serikali ile.pesa ya mataijiri wa ulaya bravo wote walioiba
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duu! hivi na wezi nao hupongezwa??
   
Loading...