Kikwete aleta haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete aleta haya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Geza Ulole, Dec 7, 2009.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  Baada ya kung'ang'ania kutovunja urafiki na mafisadi leo hii tunaona mafisadi hawa wakitumia kila mbinu kuvunja mshikamano wa wananchi walioanza kuona CCM si serikali matokeo yake sasa kila dini inamuongozo wake na baadhi ya miongozo imekaa kidini zaidi na sio kwa maslahi ya nchi! Ewe baba wa taifa Mwenyezi alikupa upeo wa kuona yapi makapi na yapi machicha!

  Leo hii tuna kiongozi anayetupeleka ulipopatabiri! nasubiri tu mwongozo utakaodai sharia law! na uko njiani, tujifunze makosa tusirudie makosa Lebanon inakuja hiyo! Hapa kiongozi wa kidini anajisifu kwa kuweza kushinda uchaguzi uliopita kwa hiyo inamaanisha watu waliambiwa wapigie kura wenye dini yao! Tunachokitafuta tutakipata kama RA asiyejdhibitika hata uraia wake ni upi? ndo analeta yote haya na inashindikana kuwajibishwa mimi naangalia uwezekano wa kukana uraia sijiskii fahari ya kusema mimi ni Mdanganyika! Hivi jeshi letu lipo jamani naona sasa CCM itatupeleka Zimbabwe kama sio Lebanon?


  Waislamu wazindua programu kutekeleza mwongozo wao 2010
  [​IMG]
  Salim Said

  KAMATI ya Siasa ya Shura ya Maimamu jana ilizindua programu ya Elimu ya Uraia yenye lengo la kutekeleza kwa vitendo waraka wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Programu hiyo inataja sifa za msingi za chama na mgombea anayepaswa kuchaguliwa, masuala ambayo yalisababisha utata mkubwa baada ya nyaraka hizo za Shura ya Maimamu na Kanisa Katoliki kutolewa.

  Mpango huo umo kwenye kitabu cha kurasa 76 na unataka Waislaam kuutekeleza kwa vitendo mwongozo uliozinduliwa na kamati hiyo Agosti 26 mwaka huu.

  Programu hiyo ilizinduliwa jana kwenye Msikiti wa Mtoro jijini jijini Dar es Salaam na balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Ufaransa na Italia, Abbass Sykes. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Sykes alisema: "Nchi hii ni ya Watanzania wote, hakuna chama wala mtu mwenye hati miliki ya kutawala nchi hii."

  Alisema kila chama na mtu bila ya kujali rangi, dini, kabila au mahali alipotoka, ana haki ya kuomba uongozi ili mradi awe amegombea nafasi ya uongozi kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

  Sifa za mgombea zinatajwa katika mada nambari tano ya kitabu hicho cha 'Elimu ya Uraia' kikitaja bayana sifa za mgombea anayetakiwa kupigiwa kura na Waislamu. "Awe kiongozi mwadilifu, anayejua matatizo makuu ya nchi na wananchi na mjuzi wa kuyatatua.

  Matatizo makuu ya nchi ni udini, ubaguzi dhidi ya Waislaam au baadhi ya watu, rushwa, uchafuzi wa mkataba wa Muungano na ukosefu wa maadili kwa viongozi," inasema sehemu hiyo katika ukurasa wa 65.

  "Awe kiongozi mwenye utashi wa kuwasaidia wananchi wote bila ya kujali tofauti zao, ajali zaidi maslahi ya umma kuliko ya chama chake, awe tayari kusaidia urejeshaji wa haki za wananchi zilizotaifishwa na serikali ikiwa ni pamoja na shule, ardhi na majengo."

  Kitabu hicho kinaeleza kuwa ili mgombea apigiwe kura, anapaswa awe anafahamu haki na dhuruma walizofanyiwa Waislaam kwa kutotendewa haki sawa na dini nyingine na awe tayari kufuta makubaliano baina ya serikali na kanisa.

  "Kiongozi huyo lazima awe tayari kutomwaga damu ya Waislaam kama ilivyotokea mara kadhaa katika misikiti, maandamano ya kudai haki au katika mahubiri ya kidini."

  Kuhusu chama kinachostahili kuingia madarakani, kitabu hicho kinafafanua kuwa ni kile ambacho serikali yake haitawazuia Waislaam kufuata na kutangaza dini yao kwa uhuru na ambayo haitabadilisha sheria za Waislaam zinazohusu mambo ya mirathi, ndoa na talaka.

  Kamati hiyo ya siasa ya Shura ya Maimamu, ilikumbushia migogoro mbalimbali baina ya serikali na Waislaam na kwamba chama kinachofaa ni lazima kiwe tayari kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya Waislaam yaliyotokea miaka iliyopita.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake, itakubali kufanyika kwa uchunguzi wa mauaji ya waislaam katika maandamano ya kutetea Qur-an 1988, mauaji ya msikitini Morogoro 1994, mauaji ya kinyama msikitini Mwembechai 1998, mauaji ya imamu wa msikiti wa Mwembetanga 2001 na mauaji katika maandamano ya Waislaam ya kupinga kufungwa kwa mwenzao aliyesema Yesu si Mungu mwaka 2001," inafafanua sehemu ya kitabu hicho.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake haitakuwa tayari kupokea maagizo, sheria na misamiati mipya dhidi ya Waislaam kama vile magaidi au siasa kali na kuwasikiliza masheikh na maimamu pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislaam."

  Awali katibu wa kamati ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema: "Muongozo (wa awali) umefanikiwa sana hasa mikoani, katika mikoa ya kanda ya kusini zaidi ya asilimia 90 ya viongozi walishinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni Waislaam wanaojielewa."

  "Asilimia 75 ya wilaya zote za Tanzania zimefanya warsha na makongamano kuuchambua mwongozo, hotuba za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja zimeanza jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislaam limetanga kura ya maslahi kuwa ajenda yao kuu 2010 na Taasisi 15 zimesaini makubaliano ya pamoja kuelekea uchaguzi mkuu." Kwa mujibu wa sheikh Ponda, program mpya ya elimu ya uraia itatekelezwa katika mifumo ya machapisho, warsha, semina, makongamano, mikutano ya hadhara na hotuba kali za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja katika miskiti yote nchini.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16500
   
 2. a

  alex50 JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  kaz kweli kweli!!!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  cuf
   
 4. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kunya anye kuku tuu (kanisa katoliki) akinya bata kahara sio?Waislamu miaka yote wanadai mahakama ya kadhi bila ya kupewa, wakati Kenya mahakama ya kadhi ipo na kila kitu fresh kabisa...

  Waacheni watoe miongozo yao kwa kutumia dini zao....ni haki ya kikatiba kabisa kuelimishana viongozi gani anawafaa na kiongozi hawafai
   
 5. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  kwani TZ ni Kenya
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mauwaji mengi naona yametokea wakati RAIS wa Tanzania alikuwa ni MKRISTO. Naona ndiyo maana waliamua kumtumia MPAMBE ili AMCHAPE kibao kwenye ru-public lwa watu.

  Baadaye mwaka 2001, hivi nani alikuwa Waziri wa mambo ya NDANI? Mkristo ehh?

  Huyo SYKES naona na yeye kaanza kufulia. Yaani na kuneemeka kwake kule kote bado anasimama na kusema Waislaam wameonewa? Nakumbuka Mbezi beach zamani ilikuwa imejaa vibao kibao vikionyesha jinsi ya kwenda kwake. Jamaa yangu alikuwa na kitabu cha chanjo cha ovyo na watengenezaji ni hao Sykes family.

  Naanza kuamini kuwa UZEMBE wa uongozi wa juu, unaanza kutoa mwanga wa watu kuja madai ya KIPUUZI namna hii. Wanachokitaka watakipata. Kama mwataka vita basi NGOJA TU IJE ili tuchinjane. Tuchukue SILAHA tuchapane na atakayeshinda ndiye atawale na wengine wote tuwe au WAISLAAM au WAKRISTO. Au wote tukose dini ili walau isiwe kilio cha Mkristo/Muislaam ila NIWE NA DINI YANGU. Kweli ukimpa YARD atachukua MAILI.
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  Nenda zako usitudanganye hapa huko Kenya kuna mzozo kama huu katiba mpya Makanisa yamepinga sheria za mahakama ya kadhi kuwemo ndani ya katiba ya jamhuri ya Kenya! Hata balozi wa Kenya Tanzania alisha shauri Tanzania isithubutu kuanzisha mahakama ya kadhi maana huko Kenya ni balaa! Anzisha nchi yako kaka na uweke hata sharia law hamna atakayekubughudhi! Tumezaliwa hamna mahakama ya Kadhi na tutakufa hamna mahakama ya kadhi wala mjomba wake sharia hapa Tanzania! Mjaazi Mungu uijalie hekima Jamhuri juu ya hili! Amen
   
Loading...