Kikwete akutana na Uhuru Kenyatta, Ikulu - Nairobi

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
IMG_20160508_165213.jpg
Rais wa awamu ya nne wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete amekutana na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta leo asubuhi, ikulu Nairobi.

Mhe Kikwete amefanya mazungumzo kwa takribani masaa matatu na Rais wa Kenya Mhe Uhuru, Mhe Kikwete yuko nchini Kenya akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika msiba wa aliyekuwa mke wa Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki.
 
Rais Msaafu Jakaya kikwete ni Mwanadiplomasia mahiri, tukumbuke mgogoro wa Kenya akishiriki kikamilifu kuutatua na sasa hivi ameombwa kuwa mmoja wa wasuluhishi katika mgogoro wa Libya.
Umesema sahihi...huyu mtu ni bingwa katika diplomasia na siasa za kimataifa.
 
View attachment 345690 Rais wa awamu ya nne wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete amekutana na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta leo asubuhi, ikulu Nairobi.

Mhe Kikwete amefanya mazungumzo kwa takribani masaa matatu na Rais wa Kenya Mhe Uhuru, Mhe Kikwete yuko nchini Kenya akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika msiba wa aliyekuwa mke wa Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki.

Hata kwenye misiba anawakilishwa.
 
Linapokuja suala la umahiri katika diplomasia ndani ya nchi hii huwezi kuacha kuwataja hawa manguli wawili.dk salim na dk kikwete hakika hawa wamefuzu kwa umahiri mkubwa katika diplomasia.
Hongera dk kikwete
Hongera dk salim
 
JK anasubiri uteuzi awe balozi wa kudumu wa Tanzania UN....ingawa najua JK yeye anapenda kuzurula! Ana wish awe Waziri wa Mambo Nje! Miaka 20 ya kuzurula hajazoea tu na kukinai?
 
Back
Top Bottom