Kikwete aingia mtaani

Kikwete aingia mtaani

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,148
Reaction score
162,558
Raisi mstaafu,Jakaya Mrisho Kikwete,jana aliingia mtaani na kufanya shopping Mliman City.

======================
attachment.php

KWA mara ya kwanza tangu aondoke madarakani mwanzoni mwa mwezi huu, jana Rais Jakaya Kikwete alionekana akifanya manunuzi katika maduka yaliyopo jengo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Kikwete, ambaye alikuwa amevalia suti maarufu kama ?kaunda suti? yenye rangi nyeusi, alionekana akiingia katika viunga vya Mlimani City saa 5:00.

MTANZANIA Jumamosi ambalo lilikuwepo katika viunga hivyo vya Mlimani City lilishuhudia Kikwete akiwasili katika maeneo hayo akiwa katika msafara wa magari manne na pikipiki moja.

Rais huyo mstaafu pia alikuwa ameambatana na mkewe, Salma Kikwete, aliyekuwa amevalia mavazi ya kitenge pamoja na walinzi wao wanne.

Hatua hiyo ilionekana kushangaza baadhi ya watu waliokuwepo katika maeneo hayo, huku wengi wao wakionekana kutaka kumsalimia.

MTANZANIA Jumamosi ambalo muda wote lilikuwa likimfuatilia Rais Kikwete na mke wake, lilishuhudia wakiingia katika maduka ya Game na kufanya manunuzi kwa dakika zisizopungua 10 hadi 15 na baadaye kutoka nje na walinzi wake wakionekana kubeba mifuko iliyokuwa na bidhaa walizonunua.

Kama ilivyo hulka ya Rais Kikwete alipotoka nje ya duka hilo alianza kusalimiana na mtu mmoja ambaye alionekana kufahamiana naye.

Hatua hiyo ilimpa fursa ya kuwasalimia watu wengine waliokuwa karibu na tawi la benki moja.

Baada ya hapo msafara wake uliondoka na kuelekea Barabara ya Sam Nujoma.

Tangu achaguliwe kuwa rais mwaka 2005 itifaki na majukumu yake ya urais yalikuwa yakimbana Rais Kikwete na hivyo kushindwa mambo yake binafsi kama walivyo raia wengine.

Pamoja na kwamba Kikwete sasa ni raia, lakini kutokana na wadhifa aliowahi kuushika wa urais bado halingani na raia wengine wa kawaida, ingawaje majukumu ya urais yamepungua na hivyo kumpa fursa ya kutembea katika maeneo ya wazi na kufanya matumizi ya kawaida kama alivyofanya jana.

Tangu alipoachia kiti cha urais na kumkabidhi Dk. John Magufuli baada ya kuapishwa Novemba 5, Kikwete amekuwa akiishi nyumbani kwake Msoga, mkoani Pwani.

Rais Kikwete aliondoka rasmi Ikulu na familia yake Ijumaa iliyopita Novemba 6 na kuanza maisha mapya kijijini kwake huko.

Chanzo: Mtanzania
 

Attachments

  • k.jpg
    k.jpg
    28.8 KB · Views: 9,510
aaah asijisahau sana maana PK lile biti lake bado hatujamwelewa alikuwa na maana gani na ujasiri gani kumpiga biti raisi wa nchi kubwa kama TZ na hali yy ka nchi kake kadogo

Raisi mstaafu,Jakaya Mrisho Kikwete,jana aliingia mtaani na kufanya shopping Mliman City.

Chanzo:Magazetini leo
 
Haa haaa Vasco anakumbukia safari za Nje kaamua kuziamishia nyumbani.
 
Mbona ghafla, kutoka shopping za Mississippi,Michigan,London,Dubai na Shanghai mpaka mlimani city? Duh, hapo ni wiki mbili tu, naona mwezi mtukufu tutakutana pale Tandale kusaka futali!
Nilivyosikia hii habari nikajikuta naishia kucheka kimoyomoyo tu.
 
Acha aingie maana tetezi ni kwamba analipwa 80% ya Tshs.400m , sasa kutoka msoga kwa ndege kuja kufanya shopping na kurudi kawaida sana.
 
Nafikiri amemaliza muda wake, tumemlaumu sana sasa yuko Uraiani
tumuache apumzike, maana kupumzika ni pamoja na kuachana na lawama
nzito za kiuongozi ambazo zilimuelemea
 
Ngoja tuone kwanza mgogoro wa zanzibari utakavyoisha ndiyo tujue kama kweli anapumzika kwa amani
 
Haa haaa Vasco anakumbukia safari za Nje kaamua kuziamishia nyumbani.

Hivi na hilo biti la safari za nje nalo linamuhusu.....?......maana sielewi kinachoendelea mpaka sasa.........
 
Hakuna kwenda nje ya nchi, na yeye inamuhusu.
 
Mbona ghafla, kutoka shopping za Mississippi,Michigan,London,Dubai na Shanghai mpaka mlimani city? Duh, hapo ni wiki mbili tu, naona mwezi mtukufu tutakutana pale Tandale kusaka futali!

hahahaa! Jf bhana raha sana
 
Lowassa makufuru kutembea mitaani na kwenda Kariakoo.na kupanda daladala.Double standards.
 
Back
Top Bottom