Kikwete agoma kutoa misaada ya Ambulances; Ikulu yaboronga!

Machache:
Kwa kuwa kwenye maelezo, Ikulu iliwasiliana na Arusha kwa simu, nadhani ni rahisi sana mpokea simu wa Arusha kuchanganya maneno Loliondo/Longido.

Baada ya Mheshimiwa Rais kung'amua huo mchanganyiko, angeendelea kutoa hilo gari bila kutuambia lolote, bali angetoa fungu from anywhere kununua gari kwa ajili ya halimashauri nyingine.

Rais sio yeye mwenye kuajiri watumishi wa Ikulu, uozo wa wafanyakazi wa Ikulu ni inheritage ya uozo wa jamii ya Kitanzania.

Mheshimiwa Rais tunaomba uache hizo shughuli they have no value for money/time of the president of united republic of Tanzania.

Wako katika kulijenga Taifa.
Kasheshe

Kasheshe,
You might be right. Lakini Rais pia anao uwezo wa kuwachuja waajiriwa wa Ikulu na kuweka wale anao wataka especially kwenye private office yake ambayo ina watu wanaompangia ratiba ya shughuli zake na kusimamia shughuli za familia yake. Naamini Mnikulu aliyepo ni chaguo la Rais na pia Private Secretary aliyezuliwa janga na Mtikila naye ni chaguo la Rais mwenyewe.ingawa nadhani huyo siye anayeshughulikia ratiba za kazi za kila siku za Rais. Culprit katika sakata hili anastahili kuwajibishwa. Ni aibu.

Naam, hizo shughuli ndogo ndogo za kugawa ama kukabidhi magari haziko kwenye kiwango cha kufanywa na Rais unless kuna sababu maalum....
 
Hivi hicho kitengo cha habari Ikulu kina tatizo gani? Ni professionalism ndogo au ni mzaha? Kwa nini huyo mkurugenzi wake asijiuzulu tu? Mara nyingi migongano kibao ya habari na bado Mh. Rais anamvumilia tu. Hayo ndiyo matatizo ya kubeba vibaraka wa maswahiba huku uwezo hawana. Itabidi habari maelezo wachukue jukumu la kusemea habari za nchi maana hicho kitengo cha habari Ikulu bomu la nuclear kabisa.

wazo kwa wana JF, nivyema tukajua utaratibu wa utendaji unavyonda pale ikulu vizuri kabla ya kuchagua idara ya kubeba lawama... what if ni idara ya ulinzi na si habari? what if ni protocol na si habari? kwanini isiwe utawala (owners wa inventory) na sio habari?
 
This show how government officials lack credibility since they were trying to foul the president.they have to be accountable
 
Kasheshe,
You might be right. Lakini Rais pia anao uwezo wa kuwachuja waajiriwa wa Ikulu na kuweka wale anao wataka especially kwenye private office yake ambayo ina watu wanaompangia ratiba ya shughuli zake na kusimamia shughuli za familia yake. Naamini Mnikulu aliyepo ni chaguo la Rais na pia Private Secretary aliyezuliwa janga na Mtikila naye ni chaguo la Rais mwenyewe.ingawa nadhani huyo siye anayeshughulikia ratiba za kazi za kila siku za Rais. Culprit katika sakata hili anastahili kuwajibishwa. Ni aibu.

Naam, hizo shughuli ndogo ndogo za kugawa ama kukabidhi magari haziko kwenye kiwango cha kufanywa na Rais unless kuna sababu maalum....

Actually rais mpya akija huwa anachuja upya watendaji muhimu wote wa nchi, kuanzia wakuu wa mikoa, wakurugenzi wakuu wa makapuni ya umma mpaka mawaziri, makatibu wakuu na mabalozi.

Mkapa alifanya hivyo, Kikwete sijui hata kama alikuwa na muda maana alikuwa aasherehekea sana.
 
..mhh!!

..hivi haiwezekani kwamba Raisi ndiyo amechanganyikiwa, na wasaidizi wake walikuwa sahihi?

..kuna mlolongo wa watumishi wa serikali wanaoweka kumbukumbu za maandishi za ahadi anazotoa Raisi akiwa mikoani. napata wasiwasi kwamba process hiyo ili-fail na tunabakia kuamini kauli za Raisi.

NB:

..nadhani Raisi angetumia busara zaidi kuliko kukurupuka na kususa kama alivyofanya.

..katika mazingira hayo naamini kulikuwa na ulazima wa Raisi kugawa magari mawili moja kwa Loliondo na lingine kwa Longido.
 
..mhh!!

..hivi haiwezekani kwamba Raisi ndiyo amechanganyikiwa, na wasaidizi wake walikuwa sahihi?

..kuna mlolongo wa watumishi wa serikali wanaoweka kumbukumbu za maandishi za ahadi anazotoa Raisi akiwa mikoani. napata wasiwasi kwamba process hiyo ili-fail na tunabakia kuamini kauli za Raisi.

NB:

..nadhani Raisi angetumia busara zaidi kuliko kukurupuka na kususa kama alivyofanya.

..katika mazingira hayo naamini kulikuwa na ulazima wa Raisi kugawa magari mawili moja kwa Loliondo na lingine kwa Longido.

Hapo mjomba alitaka kuonekana katika news ni mchapa kazi na mtu wa kukaripia na kukemea pake penye tatizo. Si huwa mnamsema kuwa ni mpole na hawezi chukua maamuzi makali basi hapo nia yake aonekane kwenye press kuwa ni mkali kwa watendaji wake acha watu wanaitwa politicians bwana they know how to swing people's mind
 
jamani hii inaonyesha raisi ni msanii na walomzunguka ni wasanii.
pili inaonyesha rais ni mpenda sifa ndomana vigari 2 tu lazima waandishi wa habari au nikampeni.
tatu ataangewatuma wasaidizi wake visingefika kwa walenga ushahidi upo wazi kapigwa changa la macho live
 
Inawezekana pia yale matatizo ya "nerves" ya Kikwete yanachangia, one never knows with these things. He may very well be running out of his wits.
 
kikweteawaka.jpg


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na mmoja wa Wasaidizi wake Luambilya Fyataga baada ya Rais kushindwa kukabidhi msaada wa magari ya wagojwa Ikulu Dar es Salaam jana kutokana na kuja watu ambao sio walengwa wa kupokea msaada huo. Picha na Fidelis Felix

*NI MKURUGENZI WA WILAYA YA NGORONGORO ALIYEANDALIWA KUKABIDHIWA GARI LA WAGONJWA LA WILAYA YA LONGIDO
Tausi Mbowe

RAIS Jakaya Kikwete jana aligeuka mbogo na kumtimua Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kubaini kuwa wasaidizi wake wamemdanganya.

Mbali na kumtimua mkurugenzi huyo, Rais Kikwete ambaye alitakiwa kukabidhi magari ya wagonjwa kwa halmashauri za wilaya za Mbozi na Longido, aliondoka katika hafla hiyo kwa hasira bila kugawa magari hayo.

Ingawa baadaye jioni ya jana taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilieleza kuwa Rais alimkabidhi Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Jeremiah Chilewa kwa ajili ya wakazi wa eneo la Kamsamba, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, gari la wagonjwa ili kupunguza shida ya usafiri wa wagonjwa katika eneo hilo.

Rais Kikwete alifika katika viwanja vya Ikulu saa 7:30 kwa ajili ya kukabidhi magari hayo ya wagonjwa, lakini, kabla ya kuanza kazi hiyo, alimhoji mmoja wa wakurugenzi ambao wilaya zao zilipaswa kupata mgawo huo.

“Wewe bwana unatoka wapi? alihoji Rais Kikwete na mkurugenzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kayange Jacob alijibu ametoka wilaya ya Ngorongoro. “Unasema unatoka Ngorongoro?" aliendelea kuhoji Rais Kikwete. "Hapa umefikaje, umekuja kufanya nini na nani kakualika? Aliendelea kuhoji huku akiwageukia wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Rais Ikulu.

"Huyu amekuja kufanya nini hapa? Nani kamwalika", alisema Rais Kikwete ambaye sura yake ilionekana wazi kukasirika na kulazimia kuvua miwani.

“Hatuwezi kukupa gari hii. Hii ni kashfa kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kwa wananchi wa wilaya ya Longido wakati nilipofanya ziara kijiji cha Engalinaibo kipindi cha ukame ambapo nilifika Kituo cha Afya wakazi wa Engalinaibo wakaniambia hawana gari la wagonjwa na nikawaahidi nitawaletea: “Nakumbuka nilipofanya ziara wananchi wale waliniambia wanayo dispensary (Zahanati ) lakini, hawana gari la wagonjwa na sio nyinyi! Hatukupi bwana, sio lako hatukupi."

"Hatuwezi kukupa gari, watafuteni wanaopaswa kupewa gari hili, hii ni kashfa kubwa, document zote zimeandikwa kwa kijiji cha Engalinaibo iweje tuwape watu wa Ngorongoro?" alihoji.

“Waombeni radhi hawa mabwana (waandishi) mliowaalika kwa ajili ya kufanya coverage hii (kuandika habari hii) kwa kuwasumbua, siwezi kutoa gari hapa waende tu, ”alisisitiza Kikwete na kuondoka eneo la tukio kwa hasira bila kukabidhi magari hayo. Baada ya tukio hilo Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga aliwaomba radhi waandishi wa habari kwa kuwasumbua kuhudhuria tukio hilo.

“Hii ni bahati mbaya tu jamani, kilichotokea hapa ni Confusion (mchanganyiko) huyu mkurugenzi amefika hapa baada ya kupewa taarifa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye yeye ndio alipelekewa barua ya mwaliko na Ikulu,”alisema Kibanga na kulazimika kuisoma barua hiyo mbele ya waandishi wa habari.

Barua hiyo imeeleza kuwa ilienda kwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha na sio mkuu wa mkoa kama alivyosema Kibanga sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa na Katibu wa rais Ikulu ilisomeka:


“Husika na kichwa cha habari hapo juu, Rais wa Jamhuri ya Muungano , mheshimiwa Jakaya Kikwete ameagiza gari moja ambalo limetolewa na Kampuni ya CMC Automobile kwa wananchi wa Tanzania litolewe kwa kijiji cha Engalinaibo Wilaya ya Longido hivyo unatakiwa kuteua madereva wawili watakaohudhuria mafunzo ya jinsi ya kuendesha gari hilo na mkurugenzi wa kuja kukabidhiwa gari hilo.”

Alipotakiwa kueleza kama barua hiyo imeandikwa kwa kijiji hicho cha Engalinaibo Wilaya ya Longido, iweje waje madereva na Mkurungenzi wa wilaya nyingine na Ikulu isigundue, Kibanga alikiri udhaifu katika hilo.

“Ni kweli walipofika, walipokelewa huwezi kujua walijielezaje lakini, naamini huko walipotokea ndio kulikuwa na mkanganyiko katika mkoa wao badala ya kutumwa wa wilaya ya Longido wamewatuma wa Ngorongoro,”alisisitiza Kibanga.

Baadaye Mwananchi ilimtafuta Mkurugenzi kupata ufafanuzi ambaye alisema, “Mimi nilipigiwa simu na Mkuu wangu wa wilaya kuwa nije Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhiwa gari la wagonjwa kama msaada kutoka kwa rais siku ya leo (jana) na kupeleka madereva wetu wawili kwa ajili ya kupewa mafunzo ya namna ya kuendesha gari hilo la wagonjwa (Ambulance) na kujiandaa kwa safari." “Tuliteua madereva na kuwaleta wakafanya mafunzo maalumu na hatimaye mimi mwenyewe nikafika ili kukabidhiwa msaada huo, Kwa kweli hata mimi nimeshangazwa baada ya kusikia kauli ya Rais kuwa Wilaya yangu hatupaswi kupewa msaada huu, mimi nimepigiwa simu tu na mkuu wangu wa wilaya,"alisisitiza mkurugenzi huyo.

Source:Mwananchi

MY TAKE: Naona barua inajieleza vizuri kabisa sasa inakuwaje huyu mkuu wa mkoa anachanganya wilaya zake au hajui tofauti kati ya wilaya ya Ngorongoro na Longido? Naona huu ni uzembe wa hali ya juu kabisa.
 
Actually rais mpya akija huwa anachuja upya watendaji muhimu wote wa nchi, kuanzia wakuu wa mikoa, wakurugenzi wakuu wa makapuni ya umma mpaka mawaziri, makatibu wakuu na mabalozi.

Mkapa alifanya hivyo, Kikwete sijui hata kama alikuwa na muda maana alikuwa aasherehekea sana.


  • Niliposikia kwa mara ya kwanza eti kagoma kupanda mtumbwi, nikaguna mmh !
  • Nikasikia kagoma kugawa pikipiki, nikajiuliza kunani - maajabu gani haya !
  • Nikasikia tena kagoma kupanda helikopta, nikang'aka aka - hili sasa bomba, haiwezekani !
  • Niliposikia sasa kagoma kugawa ambulensi, sijashangaa hata kidogo - yaonekana imekuwa tabia.
  • Lakini nitakaposikia kagoma kuteuliwa kugombea Uraisi, hakika sitaweza kujizuia tena - nitapiga vigelegele !
 
Why Arusha? Pikipiki Arusha,Hotel kubomolewa ukuta Arusha, sasa Ambulance???? Kaka EL lazima yu KAZINI...
 
Hivi maafisa wote Ikulu hawakugundua tofauti kati ya Longido na Loliondo hadi Rais mwenyewe!? Mnajua huko aliko mwenyewe anajipongeza kuwa amesevu na gazeti la Daily News na mengine ya serikali yatatoa pongezi kubwa kwa Rais huku yakilaumu watendaji wake.
 
Tatizo la JK anaaibisha Ikulu yetu. Kutaka publicity sana kuna mgharimu. Tumechoshwa kusikia failures zinazoihusu ikulu hata kwa masuala madodo madogo kama haya.

vitu vingine vidogo vidogo kama hivi angelikuwa anawaachia wasaidizi wake wahusike navyo. Anajaribu kujiaibisha na intelligence yake/yetu bureeee!!. Wakati fulani, hata kama kuna udhaifu kwenye nyumba, mama au baba hujaribu kujistiri kidogo!

JK hajifunzi tu? Juzi juzi tu hapa katuacha hoi na ile hotel ya Arusha, hatujakaa sawa mkenge na CMC.

Uozo wa CMC tunaufahamu. Wahindi hawa, wanadhurumu mali ya wa TZ kwa kukwepa kodi, halafu wanatumia pesa walizokwepa kodi nk, kujifanya wanatoa misaada. Huu ni uhuni!

Kwa JK
Mh Rais unatuaibisha. Kwa nini kujihusisha husisha na uzinduzi wa vitu vidogo vidogo ambavyo hata havijawekwa sawa??. Kama, ndiyo njia ya kutaka mass support, poa! Ngoja nimalizie kajumba kangu, nami nianze kuwasiliana na wakuu wa itofaki; wakulete uje ukazindue. Huku utashangiliwa sana!

Ila ujapo uje na majibu ya swali hili: Wewe hauoni unatuaibisha kwa kujihusisha husisha na uzinduzi wa shughuli ndogo ndogo ambazo zingefanywa na wasaidizi wako wakiwemo wakuu wa wilaya?????

Mkuu heshima kwako,
Muungwana anajifanya ku mind issue ndogo kama hiyo ilhal kuna watu ambao hawezi hata kuthubutu kuwagusa..
Sion sababu ya Muungwana ku mind katika hili..
La busara ambalo lingetumika hapo ni kwamba huyo mkurugenzi wa Ngorongoro angekabidhiwa gari hilo na aagizwe ampelekee mkurugenzi mwenzake wa Longido maana hata karatasi zote za gari hilo natumaini zimeandikwa Longido na si Ngorongoro
Ila kweli,may be Muungwana ametaka kuonesha kuwa anaweza kuchukua maamuzi magumu kwa dagaa
 
Yote yapaswa kuwepo, lakini kwa hili, Rais ameonesha ukomavu katika kumbukumbu. Hongera Rais!! usikubali vipovu hawa wanaokusaidia kila leo wakuingize katika matatizo.
 
  • Niliposikia kwa mara ya kwanza eti kagoma kupanda mtumbwi, nikaguna mmh !
  • Nikasikia kagoma kugawa pikipiki, nikajiuliza kunani - maajabu gani haya !
  • Nikasikia tena kagoma kupanda helikopta, nikang'aka aka - hili sasa bomba, haiwezekani !
  • Niliposikia sasa kagoma kugawa ambulensi, sijashangaa hata kidogo - yaonekana imekuwa tabia.
  • Lakini nitakaposikia kagoma kuteuliwa kugombea Uraisi, hakika sitaweza kujizuia tena - nitapiga vigelegele !
Mkuu verse hii imetulia hasa. Ungewasiliana na Mrisho Mpoto akaitengenezea katika kinanda,Inauzika
 
- Ingekuwa nchi za wenzetu, hapa Rais angetafuta independent Councellor ili apitie shughuili zake zote toka ashike power, ili kujua ni mara ngapi kumekuwepo na ishu kama hizi za yeye kubambikiwa tu, na kama ni kwa makusudi au ni uzembe wa wasaidizi wake? Maaana don't gimme that B/S kwamba hii ni mara ya kwanza kutokea!

- And then ngoma ingehamia kwa uwt, walikuwa wapi wakati yote haya yanafanyika, tena mpaka ndani ya Ikulu, ofisi kubwa na the powerful na inayolindwa kuliko zote in our land!

- Jawabu lingekua wasaidizi wa Rais na maofisa wa Protocol, na wengine huko uwt, kuanza kuondoka mmoja baada ya mwingine, lakini kwa vile ni bongo nothing will happen, WHY? Ni kwa sababu tumezoea mediocre kila mahali na kila kona ya serikali yetu, mpaka taifa! Inasikitisha sana!

- Wellcome to the mediocre nation! hata Haiti imesingiziwa tu!

Respect.


FMEs!
 
Back
Top Bottom