Kikwete afagia Posta: Mkurugenzi Mkuu, Katibu wake hatiani kwa ubadhirifu

Lisa

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
1,549
1,074
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Posta ( DEOS KHAMIS MNDEME) na katibu wa shirika (BW SAID) wamesimamishwa kazi kwa ubadhilifu wa mali ya shirika.

Waliuza nyumba za shirika la Posta zilizopo Masaki kwa sh milioni 900, badala ya Bilioni 3, imegundulika kuwa bilioni 2 hazijulikani zilipo na hizo milioni 900 zimelipa madeni ya waliokuwa wanalidai shirika hilo.
 
kasimamishwa lini maana nahisi kama ijumaa nilimuona mahali fulani akiwa na gari la serikali
 
Anakumbuka shuka asbh, Kwa maana miaka tisa na ushehe madarakani; anakuja kujua wabadhilifu dakika za majeruhi. kama ni kweli, basi hii yote ni usanii kwa wenyemali ( watanzania).
 
wakufutwa kazi anapaswa awe jk
_ATC
_TTCL
_zote zimefia kwenye utawala wake ba bado anacheka tu
 
kasimamishwa lini maana nahisi kama ijumaa nilimuona mahali fulani akiwa na gari la serikali

Iumaa hiyo hiyo , alipewa barua yake, nasikia alikuwa anatabia ya kwenda hata safari zisizo muhusu yeye za kikazi nje ya nchi, anawaweka mameneja ambao hawana elimu kwenye madaraka ili kusudi asipate challange kwenye vikao, ili aweze kuwatawala.
 
Back
Top Bottom