Kikwete adhibiti posho za wabunge

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
23 MARCH 2012




Rais Jakaya kikwete

*Ni baada ya kilio cha wananchi,wastaafu
*Ni kile cha kupinga nyongeza za posho zao

Na Grace Ndossa

HATIMAYE dawa ya wabunge na watumishi wengine wa umma kujipangia mishahara na marupurupu makubwa kiasi cha kulalamikiwa na wananchi, imepatikana baada ya Rais Jakaya Kiwete, kuunda Bodi ya Mishahara na Marupurupu katika Utumishi wa Umma.

Rais Kikwete ameunda bodi hiyo huku ndani ya jamii kukiwa na mvutano mkubwa wa kupinga wabunge kujiongezea posho kutoka sh. 70,000 kwa siku hadi sh. 200,000 kwa kile kilichoelezwa na Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda kwamba ni kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilieleza kuwa bodi hiyo itakuwa ni kwa ajili ya mishahara na marupurupu katika utumishi wa umma.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu Utumishi Bw. George Yambesi, ilieleza kuwa uteuzi wa bodi hiyo ulianza tangu Februari 20, mwaka huu.

"Rais Kikwete ameunda Bodi ya Mishahara na Marupurupu katika Utumishi wa Umma na kumteua mwenyekiti wa bodi hiyo kuwa Bw. Vicenti Mrisho," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Katibu Mkuu wa bodi hiyo ni Bi Tamika Mwakahesya wajumbe ni Bi. Assumpta Ndimbo, Bi Celina Wambura, Balozi Charles Mutalemwa, Bw.Yahya Mbila, Bw. Hussein Seif na Bw.Arthur Mwakapugi.

***Wachambuzi wa mambo

Wachambuzi wa mambo wanasema kuanzishwa kwa bodi hiyo kutasaidia kuweka uwiano sawa wa marupurupu na mishahara kwa watumishi wa umma, hivyo kuondoa malumbano kama yaliyotokea wakati Spika wa Bunge, Bi. Makinda alipothibitisha posho za wabunge kupanda kutoka sh. 70,000 hadi 200,000.

Pia baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani walisimama imara kupinga nyongeza ya posho hizo, hatua iliyoonesha kuwagawa wabunge.

***Msimamo wa Sumaye

Hatua hiyo pia ilimfanya Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, kuongelea suala na kukaririwa na vyombo vya habari akipinga posho hizo.

Alionya kuwa nyongeza za posho zisizofuata utaratibu kwa watumishi wa umma ni hatari na ni utawala mbaya kwa nchi.

Alisema suala la posho ni jambo ambalo sasa limekuwa tatizo kwa Serikali na kuwa imefika wakati ofisi za Serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana posho.

"Ndiyo maana watu wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wanakusanya fedha nyingi, lakini ni fedha kidogo sana zinazokwenda kwenye huduma za jamii. Nadhani hili ni tatizo na ni utawala mbaya kabisa, lazima kuwepo mabadiliko kama kweli tunataka kuisaidia nchi yetu," alisema Sumaye.

Kuhusu posho za wabunge, Sumaye alisema ni jambo la hatari kwani ikiwa wabunge watalipwa viwango vya posho vilivyotangazwa, linaweza kuvuruga amani ya nchi.

***Ndungai ajibu mapigo

Akijibu kauli iliyotolewa na Bw. Sumaye Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai alilifananisha posho hiyo na tone la maji ikilinganishwa na mamilioni ambayo alidai vigogo wa mihimili mingine ya dola wanalipana.

Alisisitiza kuwa posho hizo hazilingani kwa namna yeyote ile na posho wanazopewa viongozi wastaafu serikalini na wale wa Mahakama.

Alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa posho wanazolipwa wabunge ni kidogo ikilinganishwa na mihimili mingine ya dola.

Alisema pia mishahara ya wabunge ni tone tu la mshahara wa ofisa wa kawaida wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisa wa ngazi ya chini wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

"Wenzetu wa Kenya na Mauritius wana tume ambayo ni huru na ina watu ambao wanaaminika kuwa ni waadilifu, ndiyo wanaangalia mishahara ya viongozi wa juu kama hapa kwetu labda ni kuanzia kwa mkuu wa mkoa mpaka hata Rais. Ukienda kwenye mtandao unaona kila kitu, hakuna usiri, tupate chombo huru ambacho kitatupangia sisi wote ambao tunapata pesa kutokana na kodi za wananchi... nasema Watanzania wangejua maeneo mengine kukoje wangeachana kabisa na suala la posho za wabunge."

Kwa sasa inakadiriwa kuwa kila mbunge analipwa zaidi ya sh. milioni 7 kila mwezi, ikiwa ni mshahara pamoja na posho nyingine.



 
Hana lolote huyo mpaka wananchi watishie kuandamana na upinzani wazipinge,bora 2015 ifike ili tuwatoe yeye na Chama chake legelege CCM.
 
Hakuna kitu hapo...! Kwani ile Tume iliyoundwa kushughulikia masuala ya mishahara ya watumishi mwaka 2006; mapendekezo ya tume ile yalifanyiwa kazi? Kama yupo anayejua hili aeleze hapa.
 
Hao watu wa utumishi nao wanaongoza kwa kujiipa maposho makubwa chini ya mwamvui wa miradi. Ulizia utumishi kuna miradi mingapi. Kuna wafanyakazi pae ni wa ummma lakini wanakula mkwanja si mchezo.

KUla mkwanja si tatizo tatizo ni kujipendelea . Kama ni miradi basi neema zake ziwafike na wale wafanyakazi wa umma wa kigoma . Lindi na tabora.
 
Hiyo board in "CHARISTMATIC BOARD" au "PAID BOARD"? Maana wataanza na kujipangia mishahara na posho zao kabla ya jambo lingine. The person who could control this is the Minister of Finance and Planning by imposing highest tax brancket for amount exceeding certain threshold forexample ...amount exceeding 4 million tax rate 70%; no body will pay above 4 million
 
Hongera sana Wana-JF kwa kuona kwamba jambo hili alilolipigia kelele sasa UWEZO TUNAO pamoja na wanajamvi kibao sasa yaelekea kupenya kwenye madirisha ya jumba letu kuu Magogoni.

Mhe Kikwete, hongera zangu katika hili bado nazihifadhi mpaka nije nione jinsi gani Balozi Ombeni atakavyokamilisha jambo hili kwa manufaa yetu walipa kodi, kulinda morali ya watumishi wote, kuongeza tija kiutendaji na kuokoa kodi zetu kusiko na ulazima wa kufujisha ovyo hela za wavuja jasho.

Hata hivyo Mhe Kikwete kidoooooo umetaka kunikuna kwa kupokea CONSTRUCTIVE CRITICISMS tunazotoa hapa jamvini na kuzifanyia kazi kwa faida ya taifa letu sote.

Je kwa vyombo vya habari kweli ni lazima vyote viendelee tu kuimba CCM hata pale ambapo chama hiki hakipo jukwaani? Hebu muite kijana wako Nchimbi faragha abadilishe mwelekeo pale TBC na jinsi anavyomshinikiza Mzee Mengi kufanya visivyo kawaida yake kule ITV.
 
Uamuzi wa Rais si FINAL ni wa kuogopa... ameacha hadi Maji yamemwagika hayazoleki ndio anatoa Uamuzi Usio na Bakuli wala Maji... Unyonge upo pale pale

Leadership is the desire and ability to inspire individual achievement, while a leader is just a guy at the top of the heap worried about his own...
 
Kuna watu wamekaririshwa kuwa JK hajawahi kupatia hata siku moja tangu kawa mwanasiasa,mimi si mmoja wao na sitakuwa mmoja wao,Hongera Dr Jakaya Kikwete kwa jambo hili!
 
kipanya_19-12-2011_20111221_1230693020.jpg
 
Hii Bodi ianze kwanza na Mishahara ya zile taasisi za serikali zinazosema zinakusanya Ushuru hivyo wana Uwezo wa kujilipa Mishahara Minono wakati wengine humo humo serikalini tena Wizara Moja hawalingani Mishahara. Wengine wanajifaharisha kwa Pesa za Umma wakati wengine wanaonekana kama Hayawani ofisini na hata katika jamii. Zipo taasisi ambazo serikali imeziruhusu kulipana wanavyotaka kama vile TRA, THA, TCAA,TCRA, SUMATRA eti wanaweza kuzorota kukusanya kodi ikiwa watalipwa kidogo, na nyinginezo. Mishahara ya ofisa wa kawaida inaizidi hata ya Mawaziri, CEOs na Makatibu wakuu.
 
Hivi nchi hii huwa hatuna watu wengine kabisa wa kufanya kazi? Miaka nenda miaka rudi MAJINA ni yale yale tena bahati mbaya yaliyosheheni ubadhirifu.

Huyu ARTHUR MWAKAPUGI si ndiyo aliyepatikana na hatia ya RICHMOND?! Tume ya Bunge ikapendekeza afukuzwe kazi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Lakini JK badala ya kumfukuza akamulea hadi alipostaafu kwa mujibu wa sheria.

Sasa leo hata bado SAKATA la RICHMOND/DOWNS to settle its dust, maana Downs wanatudai bilion 111 (Sijui sasa zimefikia ngapi, maana interest ni kila mwezi). Tumeletewa tena huyu fisadi Mwakapugu kwa malango wa nyuma.

Nikisema bora hata MKOLONI mtasema ninakufuru. Mwakapugu was supposed to behind bars. Huko ndiko anakositahili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom