Kikwete abariki nyongeza ya mishahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete abariki nyongeza ya mishahara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mdondoaji, Apr 22, 2011.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ASEMA HATA BINAFSISHA TENA TRL, BANDARI

  Patricia Kimelemeta RAIS Jakaya Kikwete ameahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi kupitia bajeti ya Serikali katika mwaka wa fedha, 2011/2012.

  Rais Kikweta alitoa ahadi hiyo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Mkutano baina ya Tucta na Rais ni wa kwanza tangu Kikwete achaguliwe kwa mara ya pili kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana.

  Katika mwaka wake wa mwisho wa ngwe ya kwanza ya uongozi wake, Serikali ya Kikwete iliingia katika malumbano makali kuhusu suala la stahili za wafanyakazi na mishahara midogo iisiyolingana na gharama za maisha.

  Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalumu jana kuwa, pamoja na mambo mengine, Rais ameahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi ili kuwapunguzia makali ya maisha.

  “Mishahara ya wafanyakazi ni midogo, ikilinganishwa na kipindi hiki cha kupanda kwa gharama za maisha. Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete ameihaidi kuongeza mishahara kwenye bajeti hii ya fedha ya mwaka 2011/12,”alisema Mgaya.

  Mvutano wa Serikali na Tucta
  Tukio la Tucta kukutana na Rais Kikwete juzi, linaweza kuwa dalili njema ya kuhitimishwa kwa mvutano baina ya shirikisho hilo na Serikali kuhusu masuala mbalimbali hasa stahili za wafanyakazi.

  Mvutano huo uliodumu kwa takriban mwaka mmoja kiasi cha Tucta kutoa tamko kwamba lingewashawishi wafanyakazi kote nchini kutompigia kura mgombea yeyote asiyejali maslahi yao katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010.

  Wakati mvutano huo ukiendelea Mei 4, 2010 Kikwete alilihutubia taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuyakataa hadharani mapendelezo ya Tucta ya kutaka kima cha chini cha mshahara cha Sh 350,000/- .

  Kikwete alisema hawezi kuwadanganya wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara wanayotaka na yupo tayari kuzikosa kura 350,000 za wafanyakazi.

  Baada ya mvutano wa muda mrefu, Agosti 21, 2010 Kikwete akiwa mgombea wa urais kupitia CCM alitamka wakati wa uzinduzi wa kampeni za kitaifa za chama hicho kuwa “mishahara ya wafanyakazi ilikuwa imepanda, ingawa si kwa kiwango kilichokuwa kikitakiwa na Tucta”.

  Katika nyongeza hiyo ya mishahara, Serikali ilipandisha kima cha chini kutoka Sh 100,000/- kwa mwezi hadi kufikia Sh235,000/-, tofauti na mapendekezo ya Tucta ya kima cha chini cha Sh315,000/-

  Licha ya hatua hiyo, Tucta kupitia kwa Mgaya walibeza kauli hiyo ya Rais wakisema kuwa tangazo hilo lilikuwa limechelewa, huku wakisisitiza msimamo wao wa kutompa kura mgombea yeyote wa kiti cha urais asiyejali masilahi yao au yule aliyezikataa kura zao.

  Reli, Bandari na ATCL Mgaya alieleza pia kuwa katika mkutano huo Rais Kikwete aliahidi kutobinafsisha tena Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), katika kipindi cha uongozi wake.

  Kwa mujibu wa Mgaya, Rais ameahidi kampuni hizo sasa kuendeshwa na wazawa ili kuondoa magogoro isiyokuwa na tija kati ya wafanyakazi na waajiri.

  Mgaya alisema Rais alieleza kuwa hatua hiyo imelenga kuondoa migogoro ya wafanyakazi na waajiri wao kama ilivyokuwa ikitokea katika kipindi kilichopita.

  "Mbali na hiyo rais amesema, hatua hiyo pia imekusudiwa kuwatumia watalaamu wa ndani ambao pia watasaidia kutetea maslahi ya watumishi wenzao," alisema Mgaya.

  “Kuna watalaamu wengi wa kizalendo ambao wamesomeshwa na fedha za walipa kodi lakini, walikosa nafasi ya kuendesha shughuli za mashirika makubwa kama hayo, kutokana na hali hiyo, maamuzi ya

  Serikali ya sasa ikiwa yatatekelezeka wataweza kuondoa migongano ndani ya maeneo ya kazi," alisema Mgaya.

  Mgaya alieleza kuwa Tucta imeamua kuunga mkono hatua hiyo ya Serikali kwa sababu pia inaamini kuwa inaweza kuimarisha mashirika hayo ya umma.

  Alisema, katika mkakati huo huo, Rais Kikwete aliwaambia kuwa, Serikali inakusudia kujenga Bandari ya Tanga ili iweze kutoa huduma bora ya usafirishaji katika maeneo hayo na jirani.

  "Rais alisema pia kuwa kutokana na ujenzi huo, Serikali pia itajenga reli yenye hadhi ya kimataifa katika bandari hiyo ili iweze kutoa huduma katika mkoa wa Tanga hadi Arusha na Musoma,"alisema Mgaya akimnukuu Rais Kikwete.

  Kwa upande wa Usafiri wa Anga, Serikali inakusudia kutafuta mwekezaji ili aweze kutoa huduma bora za usafiri wa anga nchini, hatua hiyo inafikiwa baada ya Serikali pekee kushindwa kutoa huduma hiyo.

  “Kuboresha usafiri wa anga ni gharama, hivyo Serikali lazima itafute mwekezaji ili aweze kuingia ubia na kutoa huduma hiyo kwa sababu fedha hizo zinaweza kutumika kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo, ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya elimu, afya na mengineyo, älisema.

  Source: Mwananchi.

  Mtazamo: Kuna tofauti kubwa baina ya mshahara wa kutosha na mshahara kujitosheleza. Wafanyakazi wa tanzania wanahitaji mshahara kujitosheleza na sio mshahara wa kutosha. Kama hakuna mipango madhubuti ya kudhibiti mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya shillingi na kulinda mfumuko wa bei ya mafuta hata kima cha chini kikiwa milioni 1 hakitatosha. Zaidi tutaelekea kuwa kama Zimbabwe. Kodi kubwa wanayokatwa wafanyakazi inawaumiza sana pamoja na gharama kubwa za maisha. Kuongeza mshahara ni kuchochea mzunguko mkubwa wa fedha katika uchumi na kusababisha kupanda kwa gharama in future tunarudi kule kule.
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,838
  Likes Received: 11,956
  Trophy Points: 280
  Huu ni usanii mwingine aliposema hata walie kwa miaka minane hawatapata alikuwa na maana gani, mtu mzima hovyo simwamini tena.
   
 3. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,811
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  hivi kumbe kima cha chini ni 235000. basi ntaifungulia serikali madai yangu, kwani wananipunja sana hawa mafisadi
   
 4. m

  mwalimu. Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kikwete ni msanii, mbona bei zimepanda muda mrefu tena kwa aslimia mia, alikua wapi, aongeze mshahara lkn adhibiti mfumuko wa bei. halafu kuna suala la madeni, mbona sisi waalimu tumepandishwa vyeo halafu hatujalipwa hadi leo? nashauri cwt tulianzishe tena.
   
 5. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kikwete anatafuta mwaliko kwenye sherehe za may mosi alijua anaweza kupingwa chini kama mwaka jana, zimebaki siku 9 kapandisha mishahara, huu ni ufisadi kwanza kile kima kingine watu bado hawajaanza kulipwa
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Shida na tatizo sio mshahara gani unalipwa bali shida ni je mshahara wako unaweza kukutosheleza na mahitaji ya kila siku. Haijalishi ukilipwa bei kama gharama za maisha ni zakupanda kama ilivyo sasa hata ukilipwa milioni 1 mkuu utaona wamekupunja kwasababu costs za everyday life are skyrocketing.
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kipindi cha lala salama........after all who cares!
   
 8. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mimi nashangaa sana Tanzania sijui tumetowa wapi hizi sera za kubinafsisha mashirika ya umma
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kodi ndiyo balaa!
  PAYE!!!
   
 10. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,159
  Likes Received: 1,162
  Trophy Points: 280
  tafuta hotuba ya nyerere ya 95 (cna uhakika na mwaka) akiwa mbeya kwny mei 1 utaona mzee huyo alichosema kuhusu ubinafsishaji
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,159
  Likes Received: 1,162
  Trophy Points: 280
  Kodi! kodi!kodi! Selikali inatoza kodi kubwa mno!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Anacheza ngoma ya CDM...
   
 13. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,237
  Trophy Points: 280
  Yani huyo jamaa, hajaachaga kuimba ngonjera, zake. Ye badala akomae na thamani ya shilingi ya kibongo kushuka chini, bado anakuja na mawazo ya "abunuasi" eti sufuria inazaa. Huo mshahara hata ukipanda milioni kwa dizain ya huu uchumi we2 unavyoishi na kupumua = to mbuzi kumpigia marimba, avae gamba.
   
 14. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwa kumbukumbu zake hajawahi sema hilo.
   
 15. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huyo mdudu anayeitwa P.A.Y.E ananinyima raha kuliko hata mbu.
   
 16. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja sana Man!Hawa ni wanafiki wakutupa.Hiyo sijui 230,000 ya kima cha chini ni Maneno tu ya Kisanii.Sidhani km kuna mtumishi wa Kima cha chini anayelipwa hiyo 230,000.Binafsi silipwi hiyo.Wizi mtupu huo...VIONGOZI ACHENI USANII NINYI!
   
 17. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35

  Ni masharti ya world bank na IMF kwamba serikali zisijihusishe na biashara.Na ndio hapa ambapo Nyerere alikuwa anatofautiana nao.Siku zote hakupenda sera za kubinafsisha mashirika ya uma.
   
 18. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi ndo tumekuwa chanzo cha mapato ya serikali kupitia kodi huku wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wakipewa misamaha ya kodo is it fair? Wapunguze kodi hadi asilimia 9 ys mshahara
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Anabwabwaja tu katika kutafuta umaarufu ambao umeshapotea....kutoka chaguo la Mungu hadi kuwa chaguo la mafisadi si shughuli ndogo.
   
Loading...