Kikulacho....!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,315
Reaction score
829,425
Kama kuna kitu cha kuogopwa kuliko vyote duniani basi ni binadamu....binadamu ni kiumbe wa kushangaza sana anaweza kucheka nawe machoni lakini rohoni ana lake baya kabisa analokusudia kukufanyia....mara nyingi watu tunaowapenda na kuwasaidia sana nakuwajali kwa kila namna ndio watu ambao huja kutufanyia mambo machafu kabisa.

Kwahiyo inapotokea ukakutana na situation kama hii basi uwe makini na kujua kuwa hawa ndo binadamu walivyo. Kuna mengi ya kujilinda nayo ukiwa na watu unaowaamini sana kwakuwa kama wakidhamiria kukufanyia mabaya basi wataanza na vitu vitu vinavyokuhusu kama nguo za ndani, nywele ulizonyoa kucha , pedi zilizotumika nk nk

Vema vitu vya jinsi hii ukajitahidi kuvitunza na kuvihifadhi sehemu ambazo hakuna mwingine anayeweza kuvifikia.

Wengi wameumizwa kwa njia hii kwahiyo ni vema kuwa makini sana.
 
mkuu mshana jr,kweli uchawi ni kitu halisi au myth?

Zamani ulikuwepo na ulikuwa una nguvu sana lakini kadiri dunia inavyozidi kubadilika na kuzama kwenye tech uchawi unapotea na kuzaliwa kitu kingine kibaya sana haya mambo ya satanism na freemason
 
Nimependa ulivyoanza mkuu kuhusu binadamu na mioyo yao. Na jinsi ambavyo wale tunaowasaidia ndio hugeuka kua sababu ya maumivu kwetu. Nilishaamua na kujiaminisha hivi..

" Binadamu yeyote, anaweza kufanya jambo lolote, wakati wowote bila kujali chochote"

Inanipunguzia sana supprises kwa sababu kuna vitu vinatokea hadi unaikumbuka signature ya the The Boss
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mshana Jr. Usemacho ni kweli kabisa, hilo lilitutokea kwenye familia yetu, tulipomjua mbaya wetu!!! hamna mtu alieamini ndie jinsi alivyokuwa close na maza!!!
 
Last edited by a moderator:
mshana jr katika ubora wako...asante kwa kutupa tahadhari.
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana nawe kabisa nilieahi skia hiyo kua nguo za ndan ficha mtu anaekuchukia akaja akachomoa kiuzi toka pale kwenye ile nguo Ana asilimia zote za kukufanyia ubaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…