Kikosi kilichomuua Osama chajiadaa kumwondoa Dikteta Kim Jong

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,966
Kikosi maalumu cha Kijeshi cha jeshi la Marekani kijulikanancho kama "Navy Seal Team Six" Kinadaiwa kujiandaa katika kumwondoa Kim Jong un wa Korea Kaskazini toka madarakani.
Navy Seal Team six ikishirikiana na wanajeshi wengine WATAALAAM wa vikosi vingine wamekuwa wakifanya Mazoezi kujitayarisha pindi watakapohitajika wakati wowote.

Kikosi hicho cha Navy Seal Team six ndicho kilichoweza kumuua Osama bin Laden baada ya kuingia nchini Pakistani usiku wa manane. Kikamuua yeye na walinzi wake na kuubeba mwili wake na kuutupa baharini.

habari kutoka gazeti la Australia na the Sun la Uingereza likinukuu habari za gazeti lingine la Korea Kusini Joog Ang newspaper likisema matayarisho ya kumwondoa Kim yako mbioni.

Hii inakuja wakati Marekani inafanya mazoezi makubwa ya WANAJESHI ZAIDI YA 17,000 wa ardhini
Angani
Maji
na
Nchi kavu
pamoja na jeshi la Korea Kusini.
Maafisa wa serikali walipohojiwa walikanusha wakisema mazoezi hayo si ya kumwondoa Kim Jong Un.
Japokuwa well placeD sources zinasema mpango huo uko na waweza kutekelezwa wakati wowote ili kumzuia Dikteta huyo kumiliki zana hatari za Kinyukilia ambazo Marekani inadai Korea ya Kaskazini imo mbioni kutaka kuwa nazo.ili ziweze kuipiga Marekani.

Nayo Marekani imesema haitairuhusu Korea ya Kaskazini kumiliki zana hizo. Ni juzi juzi tu wa kati rais Trump wa Marekani aliposema Anaweza kuchukuwa HATUA YEYE MWENYEWE bila msaada wa mtu mwingine.
Chanzo: news.com.au
The sun/ uk
Joong Ang newspaper/South Korea
 
Marekani naona imekuwa kiranja wa dunia kila kitu wanaona wanafaa kuamua wao ila kumtoa Kim madarakani watachagua mawili.

1: Kumtoa mtu mmoja kwa maelfu ya roho za watu. Hasa wamarekani.

2: Kumtoa Kim kwa kukubali kuanzisha mtafaruko wa Nuclear duniani kote
 
Wamarekani wanatafuta kick!

Wakorea sio waarabu. Na dunia tunajua kuwa Movie ya Osama Bin Laden ni ya kutengenezwa. Hamna kikosi hasa cha kufanya maajabu kwa nchi zilizobobea ktk vita kama Korea, Israel, Russia n.k. vikosi vyenu ni kwa Africa na Uarabuni tu.
 
Bila Marekani,hii dunia kuna watu tungeteswa sana!hasa watu maskini,Bila shaka hata tungekuwa watumwa!Maana hii dunia,mwarabu alivyo na roho mbaya,wachina walivyo manunda,mkorea anavyofanya kama koboko anayetisha binadamu.Na mbaya zaidi viongozi wetu ni tishio!Naiombea Marekani,imtoe huyu mshenzi kwani anaua sana watu wake
 
Marekani naona imekuwa kiranja wa dunia kila kitu wanaona wanafaa kuamua wao ila kumtoa Kim madarakani watachagua mawili.

1: Kumtoa mtu mmoja kwa maelfu ya roho za watu. Hasa wamarekani.

2: Kumtoa Kim kwa kukubali kuanzisha mtafaruko wa Nuclear duniani kote
Mkuu ugunduzi wa mabomu ya nuclear ulilenga kwenye matumizi na wala si vitisho.
Kwa muktadha wa "kila nafsi itaonja umauti" ukijumlisha na "kifo cha wengi ni harusi" naomba wayavurumishe na kuyavugumika.
Na huo mwisho upate kuja.
 
Uishukuru tu USA, bila ushawishi wao kingekuwa na vita karibu kila nchi

Wamarekani wanatafuta kick!

Wakorea sio waarabu. Na dunia tunajua kuwa Movie ya Osama Bin Laden ni ya kutengenezwa. Hamna kikosi hasa cha kufanya maajabu kwa nchi zilizobobea ktk vita kama Korea, Israel, Russia n.k. vikosi vyenu ni kwa Africa na Uarabuni tu.
 
Usiseme hivo boss. Hii tunaiita "stepping into no man land" kiukweli hii ni ngumu sana kwa nature ya pyongyang. Ili waweze kufanya hicho kitu wanahitaji intelligence za kutosha lakini kwa pyongyang tusijidanganye hawana intelligence za kutosha kiasi cha kuweka "boots on the ground" Hili swala mimi na uelewa wangu na uzoefu wangu wa hizi mambo its practically impossible for now.
 
Back
Top Bottom