Kikosi cha Polisi cha wanamaji kimekamata shehena ya mizigo isiyolipiwa kodi bandarini Dar

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Kikosi cha Polisi cha wanamaji kimekamata jahazi likiwa linatokea bandari ya Zanzibar kwenda bandari ya Dar es Salaam likiwa limesheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo spika za redio na friji wakati jahazi hilo liliondoka bandari ya Zazibar kibali chake kikionyesha kuwa limebeba mafuta ya marashi.

ITV ilifika makao makuu ya kikosi hicho na kukuta jahazi hilo linaloitwa Najat likiwa limejaa vifaa hivyo huku polisi na wafanyakazi wa jahazi hilo wakisaidia kushushwa kwa vifaa hivyo ambapo kamanda wa kikosi hicho Semboje Kanga amesema nyaraka za mzigo haziendani na kilichobebwa.

Katika hatua nyingine wenye mzigo huo wamejitokeza na kusema kuwa wananyaraka zote muhimu na wanashindwa kuelewa kwa nini polisi wanasema shehena hiyo wanamashaka nayo.

Naye mliki wa chombo hicho kilichokamatwa Bw Iddy Hadibu amesema kilichotokea ni kwamba wakati wanakuja bandari ya Dar es Salaam baharini wakakuta chombo kingine kimelemewa na mzigo na ndio wakawasaidia ili wasipate shida na hapo ndipo walipojikuta wanaingia katika dhahama hiyo.
 
Ni msigo halali ulikua unaenda bandarini...ila kila mtu sasa anataka aonekane katumbua jipu hata kama kwa dhulma..
 
Nahodha "tuna nyaraka zote za mzigo" mmiliki "sio wote mzigo wetu mwingine tumewasaidia wenzenu walielemewa"
Ilimradi maneno kugonga gonga meno!
 
Ni msigo halali ulikua unaenda bandarini...ila kila mtu sasa anataka aonekane katumbua jipu hata kama kwa dhulma..
Wahujumu Uchumi hamtapona Awamu Hii. Jifunzeni taratibu za kulipa Kodi bila SHURTI. La sivyo kila siku hivyo vyombo (Mashua) vitakamatwa kwa staili hiyo. Pole Aisee.
 
Miaka ya nyuma walikamatwa watu wa magendo katika pwani ya kimbiji wakitoka z'bar mzigo ulikuwa kama wa 100mill. ivi!, polisi kwa mikwala yao wakawapeleka Oysterbay mshua akaja akatema kama 1mill. Ha! Ha! Ha! TRA na Polisi ya Mkwere iliwatoa wale jamaa na kuwasindikiza na special team hadi kwao. Sasa sijui sasa ivi hii polisi ya sizonje.
 
magumashi tu kutafuta public attention mwisho wa siku polisi wanapewa chao mzigo unarudi kwa tajiri.....haya mambo yanatokea sana bandari bubu nyingi na polisi wanajua muda wa kuwasili majahazi wanakamata ili wanaonekana wanafanya kazi mwishoni dau linaangushwa mezani mzigo unarud kwa tajiri
 
Back
Top Bottom