Kikombe hiki ni kwa ajili yetu tu ?

Kikombe hiki ni kwa ajili yetu tu ?

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Kikombe hiki cha machungu ya mgao wa umeme , eee Mwenyezimungu tuepushie .
Leo Mwanza City imekosa power zaidi ya 30hrs !

Nimekosa specific name huu mgao niupe jina gani ?
Kwengineko nimeuita "mgaodume" but still naona ni jina jepesi .

Haina ubishi kua watanzania wote tu'wadausugu na mahiri wa mgao , lakini walau migao iliyopita ilikua ya maeneo , hapa upo pale hawana .

Huu wa safari hii ni hawana - hawana! Hakunapo pa kukimbia walau uchaji hata simu .

Prof. Sospeter SHKAMOO !
Wenzako waliopita ni kama walitupenetrisha Kifinga !
Wewe umekuja kumalizia full- mkono! Tena hadi kwenye kiwiko!

Khaa!! nimeghadhabika hadi nikajikuta Thrade ya kwanza kulalamikia hili suala nimeipeleka kwenye jukwaa la "mambo ya kikubwa!" wadau wa kule wakanishtua " Judgement umebugi zizi ," kuitoa kule nikajikuta nimeipeleka kwenye "Jokes , Utani , Udaku , Gossips"
eee Mungu tuepushe na kikombe hichi .
 
Last edited by a moderator:
Hivi nyinyi my fellow members wa Chtcht , ina maana hiki kikombe hamkinywi ?
Coz tangu sisi tumeanza kugida haya manywaji , sijasikia hata member mmoja ananyekenya na hili .
Mmh ! Labda wenzangu mambo safi !
Mavimbwanga yosee! Baariidaa .
 
Poleni sana.....lete cm nikuchajie huku umeme hatuna kazi nao.
 
Poleni sana.....lete cm nikuchajie huku umeme hatuna kazi nao.

Basi huko ndiyo nadhani kutakua Tanzania , tulipo sie Tanganyika .
Kama una redio hapo karibu , skiza Clouds Fm utamsikia Mike Mushi , mmiliki wa Jamii forums ataongea live , muda huu anaongea madame Ritha
 
Last edited by a moderator:
P0leni sana njoo kwetu umeme hadi tunawagawia watu kule madongo kuinama maana tumeshauchoka ni mwingi balaa
 
P0leni sana njoo kwetu umeme hadi tunawagawia watu kule madongo kuinama maana tumeshauchoka ni mwingi balaa

Ni wapi ulipo shemeji Ladymasa ?
Itakua ni nchi ya ahadi ya kula Asali na Maziwa !
 
Last edited by a moderator:
yani huku kwetu ni majanga tupu na huu mgao wa umeme inabidi nitafute mkoa wa kwenda kuji:shocked:
 
Yaaani inaboaa bas tuu

Shem Chocs ! Inauma - inauma! My first bon youngboy yuko form two , nimemnunulia fridge yake maalumu ya biashara ya Barafu (ice cream) na ameajiri kijana wa kufunga/kuuza .
Max per day anapata Tsh 16,000
Check pigia 20 days per month 10 days zitoe (weekend)
16,000 x 20 = 320,000
Then kupata hesabu ya mwaka pigia miezi 10 hiyo miwili iache kwa likizo (kwakua muuzaji wake anazungusha kunako mashule)
320,000 x 10 = 3,200,000 .
Majukumu aliyonayo fees yake ya shule , na takataka zake zote in general vinatoka hapo, anamlipa mshahara muuzaji, amenunua baiskeli ya kuzungushia ana madeli ma 3 , analipa umeme wa nyumba nzima , aidha sometimes nakuta amenisaidia majukumu madogomadogo yasio yake mf. Mara kadhaa nakuta amekimu demand za wadogo zake wa primary .
Leo wamemwaga Barafu pakti 300! Zimechacha !
Kisa Prof. Sospeter !
 
Last edited by a moderator:
Shem Chocs ! Inauma - inauma

Hivi Judgement huyu Muhongo aka Prof Muongo si alisema watz wavivu wa kufikiri? ujue nimeingia jf baada ya kazi zangu kukusimama, nina kijiwe cha kuziba pancha, kujaza upepo mataili na welding! kweli inakera!
 
Last edited by a moderator:
Ni wapi ulipo shemeji Ladymasa ?
Itakua ni nchi ya ahadi ya kula Asali na Maziwa !

Nataka nifanye uchunguzi maana nahisi huu mgao unahusu majimbo ya makamanda tu (cdm), hivi kweli dodoma, moro, pwani, tanga kuna mgao pia?
 
Last edited by a moderator:

hahahaaaaa!!!shemeji pole
weka japo kajisola tu
prof.sospeter hataki mchezo!!
 
Hivi Judgement huyu Muhongo aka Prof Muongo si alisema watz wavivu wa kufikiri? ujue nimeingia jf baada ya kazi zangu kukusimama, nina kijiwe cha kuziba pancha, kujaza upepo mataili na welding! kweli inakera!

Yaani kiongozi nahisi kulia!
Swahiba wangu wakaribu nae ana berbar shop , na kijiwe ya carwash , salon kumedinda na maji mji mzima hayatoki kama ilivyo kawaida no power no water!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom