Kikombe cha Babu chashindwa kutibu ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikombe cha Babu chashindwa kutibu ukimwi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohammed Shossi, Aug 4, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kikombe cha Babu chashindwa kutibu ukimwi

  Paul Sarwatt
  Arusha
  3 Aug 2011
  Toleo na 197

  [​IMG]


  • Waliokunywa wapimwa baada ya siku 90
  • Matokeo yaonyesha bado wana virusi
  • Wailaumu Serikali ‘kubariki’ kikombe cha Babu


  MACHI 20 mwaka huu, Mwenyekiti wa Mtandao wa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (TANOPHA+), Julius Kaaya alikuwa safarini na wenzake 14 wanaoishi na virusi hivyo kwenda kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro, kupata tiba ya “kikombe” cha Mchungaji Ambilikile Masapila; maarufu kwa jina la Babu wa Loliondo.
  Kaaya na wenzake walikuwa na imani kubwa kuwa huenda tiba hiyo ikawa ndiyo mwisho wa mateso na mahangaiko ya muda mrefu yanayotokana na kusumbuliwa na virusi vya ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa dunia haijapata tiba yake.
  Watu hao walikuwa wamesafirishwa kwa msaada wa shirika la (EACNASO) ambalo pia ni muungano wa mtandao wa mashirika yanayojishughulisha na ugonjwa huo kwa nchi za Afrika ya Mashariki lenye makao yake mjini Arusha.
  Imani ya waathirika hao ilijengwa juu ya msingi kuwa dawa ya kikombe cha Babu kwa wakati huo ilikuwa gumzo kubwa nchini na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka kada mbalimbali, kama mawaziri wa serikali, majaji wa Mahakama Kuu, wenyeviti wa vyama vya siasa, wakuu wa mjeshi na wananchi, walipigana vikumbo katika kijiji hicho kupata uponyaji wa maradhi yanayowasumbua kupitia tiba hiyo.
  Baada ya safari ngumu ya siku moja na nusu kutokana na ubovu wa barabara, Kaaya na wenzake walifika Samunge na kupata tiba ya kikombe cha Babu; huku wakipewa siku 90 kama muda ambao virusi vitakuwa vimetoweka katika miili yao.
  Aidha, majibu ya vipimo vya watu hao pia vilikuwa vinasubiriwa kwa hamu na makundi mbalimbali katika jamii kutokana na watu hao kujitangaza kuishi na virusi hivyo na kuwa tayari kuweka hadharani majibu ya vipimo vya hali zao.
  Lakini miezi minne sasa tangu muda uliotolewa “kisayansi” na Mchungaji Masapila kuwa virusi vitakuwa vimeisha miilini mwao, Kaaya na wenzake wote waliotumia tiba hiyo wamevunjika moyo baada ya kupimwa upya na kuonekana kuwa bado wana virusi vya ugonjwa huo hatari.
  Taarifa za wagonjwa hao kutopona virusi hivyo ilithibitishwa mwishoni mwa wiki na Kaaya mwenyewe alipohojiwa na Raia Mwema ambapo alieleza kusikitishwa kwake na hali hiyo.
  “Ni kweli, baada ya siku tisini tumepima virusi mara tatu na majibu yanaonyesha kuwa wote bado tuna virusi vya ugonjwa wa ukimwi, na wala kiasi cha virusi bado hakijapungua mwilini”, alieleza Kaaya.
  “Matokeo hayo yamewavunja moyo baadhi ya wagonjwa ambao walikuwa na imani kuwa huenda wamepata tiba ya virusi vilivyokuwa vimewasumbua kwa muda mrefu pamoja na magonjwa nyemelezi”, aliongeza Mwenyekiti huyo.
  Hata hivyo, Kaaya ameitupia lawama serikali kwa kushindwa kuwalinda wananchi na kile alichokiita “uchezewaji wa afya za watu” uliofanywa na Mchungaji huyo mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
  “Ni jambo la kusikitisha sana. Ilikuwaje Serikali ikaruhusu tiba ya aina hiyo ambayo haikufanyiwa utafiti wowote wa kisayansi na matokeo yake waliotumia hawajapona; huku wakiwa wameingia gharama kubwa sana kuifuata dawa hiyo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi”, alieleza Kaaya.
  “Kilichowashawishi watu wengi wenye matatizo mbalimbali ni ile hatua ya viongozi wa serikali; hasa mawaziri, majaji,wakuu wa majeshi na viongozi wa vyama vya siasa kwenda Samunge kupata kikombe cha Babu.
  Alisema kuwa jambo baya zaidi ni kwamba walikubali kupigwa picha na kuonyeshwa katika vyombo mbalimbali vya habari wakipata kikombe cha dawa hiyo. “Hiyo ilikuwa ni sawa na wao kutoa ushuhuda kuwa dawa hiyo inafaa.”
  Mara baada ya tiba hiyo ya Babu kutangazwa, mawaziri, baadhi ya wakuu wa mikoa, makamanda wa jeshi na wananchi, walifurika kwa mzee huyo wa Loliondo. Aidha, watoa tiba wengine wa vikombe waliibuka huko Tabora, Morogoro, Mbeya na Iringa na watu waliwaendea kupata dawa.
  Baadhi ya mawaziri waliokunywa dawa hiyo ya mitishamba ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wassira, na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige.
  Viongozi wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa na wabunge ni pamoja na Nimrodi Mkono (Musoma Vijijini), Augustine Mrema (Vunjo), Rose Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yohana Balele na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro.
  Aidha, viongozi kadhaa wa madhehebu ya dini kama maaskofu pia walikwenda Samunge kupata kikombe hicho cha Babu hali iliyotia hamasa wananchi wengine kumiminika kwenda Samunge.
  “Ilikuwa makosa makubwa kwa viongozi wa serikali kwenda kunywa dawa hiyo wakati haijafanyiwa utafiti wowote wa kisayansi wa kuthibitisha kuwa ilikuwa na nguvu za kuponya”, aliongeza Kaaya.
  Mwenyekiti huyo wa mtandao wa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi aliongeza kusema kuwa, ni ukweli ulio wazi kwamba dawa ya kikombe cha Babu haiponyi, na uthibitisho huo unaonekana kwa wagonjwa wote waliopata tiba hiyo wanaosumbuliwa na magonjwa mengine kama kisukari, shinikizo la damu, pumu na kifafa, na hakuna hata moja aliyepata kupona kabisa.
  “Naendelea kutoa wito kwa Watanzania wenzangu wanaosumbuliwa na virusi vya ukimwi, hata kama wamekwenda Samunge kunywa dawa ya kikombe, wasiache kutumia dawa zao za hospitali; kwani wanaweza kupoteza maisha, na hali hiyo imeshawatokea wengi”, alionya Kaaya.
  Akizungumzia tiba hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Salash Toure, alikiri kuwa kisayansi hakuna uthibitisho wowote kuwa dawa hiyo inaponya maradhi yanayotajwa na Mchungaji Masapila.
  “Bado taasisi za kiserikali zinazohusika zina fanya utafiti kuchunguza iwapo dawa hiyo inafanya kazi, lakini kwa sasa bado hakuna uthibitisho wa kisayansi kuwa dawa inaponya”, alisema Dk.Toure.
  Hivi karibuni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda alikaririwa pia na gazeti moja la wiki akieleza kuwa hakuna utafiti wowote wa kisayansi uliothibitisha kuwa dawa za asili, ikiwemo tiba ya kikombe cha Babu wa Samunge, haina uwezo wa kutibu ukimwi.
  Dk. Mponda alitoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati anazindua Kituo cha Matibabu ya Wagonjwa wa Ukimwi na Mafunzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
  Dk. Mponda alisema wagonjwa wa ukimwi wanatakiwa kutumia dawa za kurefusha maisha (ARVs) na kuwataka waende kwenye vituo vya afya kupewa dawa hizo na kuongeza kuwa vituo vyote vya afya vinatoa dawa za ARVs lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania mwenye tatizo la ukimwi anapata dawa hizo mahali alipo.
  Akijibu madai yanayotolewa kuwa dawa yake haina uwezo wa kuponya maradhi yanayotajwa, Mchungajji Masapila akizungumza na Raia Mwema, juzi, kwa njia ya simu kupitia kwa mmoja wa wasaidizi wake, Paulina Lukas, alieleza kuwa wanaolalamika kuwa hawajapona ni wale wasiokuwa na imani.
  “Tangu mwanzo Mchungaji alieleza wazi kuwa watakaoponywa ni wale wenye imani na Mungu. Kwa hiyo ambao hawajapona hawana imani, na pia hawakufuata masharti ya dawa; mojawapo ikiwa ni kuacha tabia ya ngono”, alieleza msemaji huyo wa Babu.
  “Kama hawajapona si makosa yetu. Tuliwaambia kabla kuwa katika tiba hii kigezo cha kwanza ni kuwa na imani, na hapa tuna uthibitisho wa kutosha wa watu walioponywa na maajabu ya dawa hii wakiwemo wagonjwa wenye virusi vya ukimwi”, aliongeza.
  Alisema watu hao wanaoishi na virusi vya ukimwi si wakweli; kwani kuna uwezekano kuwa wamepona, lakini wanashindwa kuweka wazi hilo kwa malengo ya kukosa fedha wanazopewa na wafadhili wa ndani na nje ya nchi.
  “Unajua hawa wengi wanapata misaada ya kifedha kutoka kwa wafadhilimbalimbali wa ndani na nje ya nchi, sasa wakisema ukweli kuwa wamepona watakosa misaada hiyo. Sisi tunajua kuwa ukimwi ni mradi kwa baadhi ya watu”, alisema.
  Msaidizi huyo wa Mchungaji Masapila aliongeza kuwa kwa sasa wanaendelea kutoa huduma kama kawaida ingawa idadi ya magari imepungua sana tofauti na miezi ya mwanzo ya mwaka huu. “Ni hali inayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu wabaya kupiga propaganda kuwa dawa hii haiponyi.”
  “Kwa sasa tunahudumia kati ya gari 30 hadi 50 kwa siku hasa kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda na mikoa ya Kanda ya Ziwa tofauti na miezi ya mwanzo wa mwaka ambapo tulikuwa tunapokea wagonjwa kati ya 5,000 na 8,000 kwa siku,”alisema.
  Mchungaji Masapila alianza kutoa tiba hiyo kuanzia Agosti mwaka jana baada ya kudai kuwa ameoteshwa na Mungu, na kuwa dawa hiyo inayotokana na mizizi ya mti aina ya “mugamuryaga” kwa lugha ya wa watu wa kabila la Wasonjo ambao ni wenyeji wa Samunge, ilikuwa ina uwezo wa kutibu virusi vya ukimwi.
  Dawa hiyo inauzwa kwa kiasi cha Shilingi 500 kwa dozi ya kikombe kimoja ambacho mgonjwa anapaswa kunywa na hairuhusiwi kurudiwa. Wagonjwa wote hulazimika kuhudumiwa na Mchungaji huyo kwa mkono wake mwenyewe.
  Baada ya kuonekana kuwa idadi kubwa ya watu wamejitokeza kupata tiba hiyo, Mchungaji Masapila aliwatangazia watu kuwa ameoteshwa tena na Mungu na kuongeza idadi ya magonjwa mengine sugu yanayotibiwa kwa dawa hiyo ambayo ni kisukari, shinikizo la damu, kifafa na pumu.
  Hata hivyo, pamoja na umaarufu mkubwa aliopata Mchungaji Masapila na tiba yake ya kikombe, hadi sasa hakuna uthibitisho wowote wa kisayansi uliowahi kutolewa kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kutibu maradhi yanayotajwa na Mchungaji huyo.
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, mbona siku nyingi babu kaishaonekana msanii!
  Hakuna mtu alipona kwa ugonjwa wowote, mimi na jamaa yangu alikuwa anaumwa kansa ya damu kaenda huko kwa babu karudi hoi kafikia Arghakan Hospital yupo hoi
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Hivi chuo Kikuu cha DAR, MUHAS, Mkemia Mkuu, TFDA na vituo vya utafiti hawana uwezo wa kuifanyia hii dawa utafiti na kutoa taarifa kwa uma? Au mpaka wafanye wazungu ndipo matokeo yatakapoaminika? Sasa hao wanaojiita wanasayansi/madakitari/watafiti umahili wao ni upi? Kunukuu kazi za wenzao wazungu? Mimi nafikiri hii ilikuwa fursa nzuri kwa mtu au watu kujitengenezea jina kitaaluma. Au ni bongolala kama kawaida?
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Mama mkwe wangu alifariki wiki mbili baada ya kupata kikombe. Alirudi kutoka Loliondo akiwa hoi kuliko alivyokwenda. Na kama ni imani alikuwa nayo ya kutosha.
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  "mungu" wa babu na wafuasi wake humu JF inabidi watuombe radhi hadharani. Tuliwatahadharisha wakatupuuza na ku-propagate "healing power" za huyo "mungu" wao. Pia bado tunamdai pesa zetu za DECI hajarudisha!
   
 6. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Imani haba hiyo,mbona wako waliopona babu angejulikana vipi kama siyo wagonjwa waliopona kwake wacheni hizo kama mlikwenda kupata tiba mkiwa na imani haba au na matumaini pasipo imani mtaponaje?badala ya kusali kuongeza imani nyie mnakwenda kwa ajili ya kupona tena mnajiambiza afadhali mungu amemleta huyu mtumishi sasa nitapona bila kuweka sala mbele na kunyenyekea mtaponaje,mwenyewe alishasema yeye siyo hospitali ya rufaa na kama umezidiwa usiende kwake utakufa huko sasa nyie mmeenda wakati ndiyo mmefikia mwisho mnategemea nini.
   
 7. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  aliyepona aje hadharani ajiseme...hayupo hata mmoja.
   
 8. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]
  HEBU SOMA HII HAPA CHINI TOKA GAZETI LA MWANANCHI LA LEO UONE MAAJABU

  Utafiti: Waliopata kikombe cha Babu wengi wamepona [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 03 August 2011 22:59 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Leon Bahati
  ASILIMIA 78 ya watu waliotibiwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila, walipona magonjwa yao.
  Hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate kuanzia Mei 2 hadi 19, mwaka huu na kuwahoji watu 1,994 wenye umri zaidi ya miaka 18 maeneo mbalimbali nchini.Utafiti huo uliotolewa na Synovate kwa gazeti hili jana, unaeleza kuwa ni asilimia saba waliosema hawakupona wakati asilimia 15 walisema hawajui.
  "Asilimia 78 ya waliotibiwa kwa kikombe cha Babu wa Loliondo, walisema wamepona magonjwa yaliyokuwa yanawakabili," inaeleza sehemu ya ripoti hiyo ya utafiti.
  Utafiti wa Synovate umekuja wakati ambapo utafiti wa awali uliofanywa na serikali juu ya dawa hiyo ya Babu kuinyesha kuwa ina uwezo wa kutibu magonjwa sugu kama vile kisukari, saratani, moyo na Ukimwi.
  Serikali ilisema bado inaendelea na utafiti zaidi juu ya dawa hiyo, ambao unaweza kuchukua muda wa hadi miaka mitatu ikizingatia kuwachunguza waliotibiwa na kiwango cha dozi, kulingana na aina ya ugonjwa.
  Ripoti ya Synovate inaonyesha ingawa ni watu wengi wanaotamani kuponyeshwa dawa ya Babu, ni Watanzania wachache wenye uwezo wa kumudu gharama za kwenda Loliondo.
  Asilimia 83 walisema ni vigumu kupata dawa ya mchungaji huyo maarufu kama Kikombe, huku asilimia 17 wakaonyesha hakuna tatizo la kumfikia.Hata hivyo, kati ya waliokwenda asilimia 25 hawakuwa tayari kutaja magonjwa waliyokwenda kutibiwa, wakati asilimia 24 walisema ni kisukari.
  Magonjwa mengine na asilimia ya watu walioenda kutibiwa kwenye mabano ni moyo (22), Ukimwi (13), saratani (12), vidonda vya tumbo (7), pumu (5), magonjwa ya ngozi (4), maumivu ya miguu (4), kifua kikuu (3), maumivu ya tumbo (3), maumivu ya uti wa mgongo (2), maumivu ya kifua (2), macho (1) na waliokwenda bila tatizo maalumu (3).
  Mchungaji Masapila alijijenga umaarufu mkubwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu baada ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini na nchi jirani kujitokeza kwa wingi kupata tiba hiyo.
  Hali hiyo ilisababisha baadhi ya ndugu kuwachukuwa wagonjwa wao waliolazwa hospitalini kuelekea kwa Babu, yapata kilomita 400 kutoka mjini Arusha.
  Misururu mirefu ya magari ilijipanga kwenda kwa babu na kufanya watu kutumia hadi siku saba kupanga foleni ya kupata dawa.
  Pia, utafiti wa Synovate ulizingatia kuwa kulikuwa na waganga wa jadi waliojitokeza kutoa tiba sawa na Masapila, lakini licha ya hali hiyo, asilimia 60 walikiamini Kikombe cha Babu.
  Wengine waliojitokeza na asilimia za kuaminika kwa watu kwenye mabano ni Dogo Jafferi wa Mbeya (9), Magret maarufu kama Bibi wa Tabora (8), Subira Ali (4), Majimarefu (2), Sinkala wa Mbuyuni (2) na babu wa Moma Mtwara (2).

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  Babu kala vichwa kiulaiiiini,du wasanii wapo wa kila aina
   
 10. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Tafiti ya synovate na yenyewe integrity yake iko katika swali
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Hata mimi nataka nianzishe tiba yangu halafu nitawapanga watakao sema wamepona ili nipate nyomi na mwisho wa siku nitawakatia mafao.
   
 12. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Babu ni msanii tu,
  Hamna asiyelijua hilo.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sossi,

  Ilipoanza tiba hii unakumbuka kuna watu walisema wengine tunaumwa na nguvu za shetani kisa ati hatuamini ufunuo. Nakumbuka Miss Judith alishambuliwa kama mbogo alipoihoji tiba ya babu. Nachoweza kusema ni poleni sana mlioenda kwa babu mkapoteza mamilioni yenu kwenye usafiri wa tabu na kadhia kufika huko. Mkalala kwenye udongo na baridi kali na wengine kuishia kupoteza uhai kabisa. Tiba za ufunuo hazitibu mpaka kuwepo na scientific proof. Biashara ya mtu mmoja kuamka na kudai anatibu magonjwa fulani huo ni usanii. Mie nina majirani zangu na ndugu zangu tulibishana sana mpaka wengine wakanisusia kwa kuwapinga na nia yao ya kwenda kwa babu. Wameenda hakuna mmoja aliyepona maradhi yake. Moja nusura atoke roho kwani aliacha kunywa dawa za kisukari hali ikawa mbaya sasa hivi anatumia sindano badala ya vidonge.

  Siku nyengine mtusikilize dawa za ufunuo hazitibu!!!!!
   
 14. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ishu kubwa siyo babu ni imani zetu wenyewe lakini babu alisema kama unaamini njoo na kama hauamini usijaribu halafu mtu ankuja hapa kulalamika dawa ya babu haiponyi na ukiangalia hawa shidefa+ walienda kuuza sura ndo yakawakuta..

  My take: kati ya shidefa+ na synovate nani tumuamini?..
   
Loading...