Pamoja na mambo mengine Nia na Malengo ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere ni kumuenzi na kuyaenzi yote mazuri yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa, kukemea maovu, kutetea wanyonge wanaogandamizwa na viongozi, vyombo vya dola au serikali iliyopo madarakani, kuhakikisha utawala wa sheria unafuatwa.
Tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu limegusa Taasisi nyingi zikiwemo taasisi za nje, sijaona wala kusikia Kigoda kikikemea, yuko wapi Mzee Josefu Butiku, yuko wapi Mzee Waryoba yuko wapi prof. Shivji na wengine machachali kukemea uovu huu unaolinyemelea taifa, au kazi ya Kigoda ni kuandaa matamasha tuu.
Kukaa kimya ndio kumuenzi Nyerere?, mbona Baba wa Taifa hakuwa hivyo alikuwa mwepesi kukosoa na kukemea ovu lolote hata likitokea nje ya mipaka yetu. Kukaa kimya maana yake ni kukubali maovu yanayoendelea kutokea nchini.
Kigoda kijitokeze kukemea wasichague matukio ya kukemea vinginevyo wakae kimya milele waone kama tutawasumbua, waache unafiki kujifanya wanamuenzi Mwalimu, Baba wa Taifa hakuwa hivyo.