Kikeke ambana Maalim Seif

nyie kila chombo cha habari mnakituhumu..............anzisheni vyenu muwe mnajiuliza maswali mnyotaka.
 

Stayfar,
Soma hapo juu kwenye bandiko lako nimekuwekea wino ulokoza,
yaani bold.

Umeeleweka hili halina tone la shaka.

Shaka ni uwezo wako wa kujadili mambo makubwa na mazito kama
haya.

Jikite kwanza katika kujifunza kuandika kisha ndiyo utaweza kuingia
katika mijadala.
 
Maswali y kijinga sana maalim angejibu kwa kuwa uchaguzi ulikosa uhalali kikatiba sikuwa na sabab ya kushiriki haramu

Anapiga kelele kumuondoa katika mstari maalim

Kwanini alikataa kushiriki wakati alishinda??

Kulikuwa na sabab zipi za kisheria kutengua ule uchaguzi wa awali??
 
Nimefurahishwa sana Salimu Kikeke alivyomuhoji Seif
Kwasababu Seif hakuwa na hoja za msingi kwanini hwakushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar
Kwani hujui kama ulikuwa uchaguzi haramu
 
Kizibao,
Mambo haya ya mijadala yanataka ujuzi na elimu ya kutosha katika
kile unachotaka kujadili.

Mimi si ninaesema kuwa Wazanzibari wasome kipindi kipi cha historia
yao.

Kanuni za kisomi katika hizi ''social science,'' ndizo zinavyosema hivyo.
Kuna kitu kinaitwa, ''demarcation,'' yaani mpaka.

Ikiwa unajadili mathalan, ''political parties in Zanzibar,'' yaani vyama
vya siasa Zanzibar na ukatoa rejea nje ya hapo utaonekana kuwa huna
ulijualo.

Utaonekama kichekesho kwa kuwa vyama vya siasa Zanzibar vilianza
mwishoni 1950s wewe unaleta rejea ya mwaka wa 1498...

Unaojadili nao watakupuuza.
Watajua huna taaluma ya historia na ndiyo maana hujui kanuni ya ''mipaka.''

Ushahidi wa kushinda CUF katika chaguzi zote upo kama wewe hujui ndiyo
kama nilivyosema huna taaluma kukuwezesha kujadili jambo hili.

Rejea nyuma kwenye post zangu utaona nimeweka ushahidi.
 
Ni vizuri watu mkaelewa kuwa muandishi wa habari anavyokuhoji anajifanya hajui chochote..
Hivyo basi anakutaka wewe kimuelezea ili apate kujua..

Kwa hali hiyo kikeke alikuwa sawa kabisa na ukizingatia kipindi kile ni cha muda mdogo..
Seif alipaswa atoe majibu yanayoeleweka na kwa haraka!
 
​
Leo wakati akimhoji Maalimu Seif juu ya uchaguzi wa Zanzibar, Salim Kikeke mtangazaji wa BBC, aliishia kupigishana makelele na Maalimu Seif kwani kila mmoja alikuwa anaongea kwa sauti.

Huu ndio utaratibu wa kuhoji watu Salim?

Wanamajlis,
Hiyo hapo chini nimeitoa FB:

Sitapenda kuingilia "style" ya mwanahabari katika uulizaji wa masuali lakini interview inapimwa kwa misingi yake. Kinachokera hasa kwa sisi wasikilizaji ni pale muulizaji anapokosa kutoa muda wa kutosha kwa anaeulizwa, au kumkata na kuzuia majibu ya muulizwaji. Waandishi wajikite kuuliza masuala magumu, lakini wazifanyie haki taasisi zao kwa kutoa nafasi kwa muulizwaji kuweza kujibu. Taswira ya kuvamia majibu na kukatisha uwezekano wa upande wa majibu kusikika huonyesha Bias na huondosha umuhimu wa masuala magumu yanayohitajika katika interviews. Uandishi wa habari usiwe na woga wa masuali magumu na mazito lakini kuwe na haki katika nafasi ya majibu.

Pili nimefurahi kwamba wa kwetu aliulizwa masuala waandishi walioyaona magumu, na tunategemea pia kwa wengine watapopata nafasi hasa upande wa utawala waandishi wajikite kwa masuala magumu. Jina la Salim Kikeke lieleweke kwa yeyote mwengine kuwa lenye kukidhi kiu ya masuali kwa pande zote. Masuali kwa mfano wa interview ya Pinda na Kikeke, au ya Makamba na Kikeke na wengi upande wa utawala yamekuwa ya urafiki urafiki na ya kuegemeana. Jana kulikuwa na "hostility" kubwa kwa anaeulizwa masuala kiasi ya kuondosha ladha ya kipindi chenyewe, na bias kati mwanahabari na anaeulizwa.

Kuhusu suala la kwa nini hatukushiriki uchaguzi wa marudio?

Majibu anayo Che Mkapa alioyatoa katika kipindi cha hard talk cha BBC na Sebastian. Aliulizwa kwa nini chama chake kinaogopa kurudia uchaguzi kutokana na ripoti za waangalizi zilizoonyesha uchaguzi kutokuwa huru na kuwa na makosa mengi. Akajibu ni suala la principle, kwamba uchaguzi ulishafanyika na hakukuwa na sababu ya kuingia katika gharama kwa makosa ya uchaguzi uliopita. Watawala walitoa sababu hizi hizi, principle ya uchaguzi ukishafanyika haurudiwi. Na ndio hali ilivyo kwa muda wote wa uchaguzi wa vyama vingi, hakukubaliwa kurudia kwa uchaguzi isipokuwa huu tena kwa kauli ya mtu mmoja, kinyume na katiba na weledi wa chaguzi huru na haki. Labda angeuliza vile vile kwa nini sasa uchaguzi ukarudiwa lakini si nyuma wakati malalamiko yanafanana?

Mtazamo wangu
Hoja ya uhalali wa kushiriki uchaguzi wa marudio usiokidhi matakwa ya katiba ni dhaifu kuliko hoja ya kufutwa uchaguzi ambao waangalizi wa ndani na nje wameueleza kuwa uchaguzi bora katika historia ya visiwa vyetu. Linalokosekana kwa hoja ya kushiriki kwetu ni sababu za kufutwa zenyewe pamoja na kukosekana kwa uhalali wake kikatiba na hata maridhiano kwa pande zote zinazohusika. Binafsi nimeona SK jana aking'ang'ania hoja na masuala ya kitoto. Ningefahamu kama suala lingelenga kwa nini hivi sasa opposition inataka kurejea uchaguzi tena wakati tulishasusa wa marudio? Nafikiri hapo darsa na hoja zingeendana na hadhi ya Kikeke, taasisi anayoiwakilisha na msingi mpana zaidi wa hoja.
 
Hahahahaha ewee mzee wangu...hujatoa ushahidi bali umetoa porojo za watu.. na huyo Ali Ameir amelalamika tu na hakutowa takwimu..Hivi hassan Nassor moyo ni mjumbe wa tume ya uchaguzi.
Na hivi mbona unajifanya unajua sana? "A person who think know everything constitutes the majority of one"
Yale yote yaliyotokea 1950's pale ilikuwa siyo mwanzo bali ni tumeanza kuvuna matunda ambayo yameotoshwa tangu 1498.. Sasa hicho kilichotokea kati ya hapo 1498 mpaka 1950s.kimezaa mtoto mpaka leo ndiyo anawahangaisha watu.. kwa hivyo mzee wangu wacha kuwa masikini wa mawazo siyo peke yako uliyesoma...vijana wanakuambia TULIZA boli
 
Tuambie ya kuwa muandishi wa hii habari ni Foum ALI kimara au Farrel na tunamjua ya kuwa ni kada na mmoja wa kamati za propaganda za CUF
 
Tuambie ya kuwa muandishi wa hii habari ni Foum ALI kimara au Farrel na tunamjua ya kuwa ni kada na mmoja wa kamati za propaganda za CUF
Kizibao,
Hakika ni yeye.
Nashukuru kwa kunifahamisha hizo sifa zake nyingine.

Mimi na yeye fikra zetu zinakubaliana sana ingawa
hatujuani ila katika mitandao.
 
Sasa unajifanya mjinga kwa faida ya nani?Umeweka swali aliloulizwa,mbona hujaweka alichojibu?Unakimbilia kusema anajichanganya!
Kajibu vizuri,kama waliweza kufuta uchaguzi halali wangeshindwa vipi kuiba kura au kutoa matokeo yasiyo halali?Kupeleka vifaru zanzibar ndio viashiria vyenyewe!
 

Kizibao,
Tunaweza tukawa na mjadala mzuri sana mimi na wewe lakini
ni muhimu tukachunga lugha zetu zisiwe za kejeli kwani hatari
yake tutawakaribisha watu mabingwa wa lugha chafu.

Hukuwa na sababu ya kusema natoa ''porojo.''
Ungeweza ukanipinga kwa kutumia lugha yenye staha.

Mimi nimetoa ushahidi lakini ikiwa wewe hukubaliani na ushahidi
wangu sawa.

Ikiwa Ali Ameir aliandika barua ya kukataa uchaguzi bila takwimu
hilo ni tatizo la Tume ya Uchaguzi vipi lilimkubalia?

Mimi sijifanyi najua.
Mimi ninajua.

Wala sijasema kuwa mie pekee ndiye niliyekaa darasani vizuri.
Fanya utafiti kidogo kunifahamu hilo litakudhihirikia na mengi zaidi.

Ikutoshe tu kuwa kama ulivyoniita mimi sasa ni mzee tena wa miaka
64.

Hayo mengine ya ''tuliza ball,'' ''masikini wa mawazo,'' hayana maana
tena baada ya kukupa indhar katika utangulizi wangu.
 
Mimi naona Kikeke alikusudia kufanya "hard talk" na Maalim Seif. Ni njia nzuri hasa kama unahoji upande mmoja tu katika jambo fulani. Angefanya kinyume chake, mjadala haungevutia.
 
Ukawa, kila mtu mtamuona mmbaya sababu ya kutokufurahisha
 
Ukawa, kila mtu mtamuona mmbaya sababu ya kutokufurahisha
Shida yetu sio kufurahisha bali ni ukweli ambao ccm wanajaribu kuidanganya dunia kupitia mawakala wao waliopo kwenye hivi vyombo vya habari,ni nani asiejua kuwa ccm zanzibar imeshindwa uchaguzi?uchaguzi hurudiwa iwapo kumeripotiwa mattzo je niwapi uchaguzi wa zanzibar kumeripotiwa ttzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…