Kikao gani kiliamua Nyerere awe 'Baba wa Taifa'?

....
JE IPO KWENYE KATIBA na hivyo kuwa Sharia kuwa lazima kuwe na Picha ya Rais wa JMTz (hili lipo kwenye sharia) na pembeni yake ya baba wa Taifa?

Tunaomba ufafanuzi kwa wenye ujuzi wa sharia za Muungano.

I can assume you had no time to read thoroughly the thread before commenting as you were in the flight. Did you read this below?

 

Kwani Tanganyika mlipataje uhuru wenu? mlipigana vita au mlipewa tu afisini?
Je kabla ya uhuru wenu Tanganyika ilikuwa hakuna amani?
Je kulikuwa na vita vya makabila au kiukoo kabla uhuru?

Kama hayo yoote yalikuwwepo kabla uhuru wenu na baada ya uhuru yakasitishwa basi hapo tutasema JK Nyerere alileta amani Tz. Na kama nchi ilikuwa poa hata kabla ya uhuru tutasema amani ni tuzo toka kwa Muumba kwa Tanganyika.

Na ulanguzi wa Bidhaa ulikuw haupo wakti wa Mkoloni. Ulanguzi wa bidhaa muhimu, wtu kujilimbikizia mali, na maduka ya kaya yalianza baada ya uhuru wenu. Na ni wakti wa nani akiwa kiongozi.

Nafikiri tukionana tutaongea mengi sana. Nitakuwepo Tz kwa wiki mbili na nitatembelea Mtwara baada harusi kuangalia fursa za uwekezaji huko.

 
Nashukuru kwa mwaliko Barubaru. Hii sharia Namba 15 Ibara 9 nimeikosa kwenye Katiba yetu. Tunayo katiba moja tu ya mwaka 1977. Hii ya mwaka 1984 sio yetu.
 
Lakini hata DRC, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Zanzibar,..., wakati wanatawaliwa na wakoloni hapakuwa na vita ya makabila. Jiulize ni nini kilitokea baada ya nchi hizi kuwa huru. Swali lako la kwanza nitamwachia Mzee wetu Mohamed Said alijibu.
Karibu Tanzania uwekeze kwenye rasilmali alizotuachia Mwalimu.
 
Suala zuri sana hili.

Binafsi jana nimeingia Tanzania hususan Dar es salaam nikiwa safarini kesho Insh'Allah naelekea Mwanza na Al'khamis nitakuwa Bukoba kuhudhuria harusi ya mwanangu mlezi huko kamachumu hapo l'jumaa.

Barubaru: Awali ya yote karibu sana Bongo. Kumbe mwenyeji wa Kamachumu? Vipi utalala pale Kamachumu Inn. (Hotel ya Marehemu Mzee Ngaiza kabla ya kifo chake alishajiunga na wapambanaji CDM).

Hivi Mzee Seif bado ana mabinti? Walaahi wote mmewahamishia uarabuni (tongue in chick). Ninahisi wewe kutoka uarabuni lazima huyo mwanao atakuwa anamuoa binti wa mzee Seif (no pun intended).
 
Nashukuru kwa mwaliko Barubaru. Hii sharia Namba 15 Ibara 9 nimeikosa kwenye Katiba yetu. Tunayo katiba moja tu ya mwaka 1977. Hii ya mwaka 1984 sio yetu.
.

WildCard.

Je na wewe unaweza kuchangia mabadiliko ya Kkatiba yenu wakti hiyo iliyopo huijui na wala hujawahi kuiona. Haya nimebainisha kutokana na suala lako.

Lakin nitakusadia zaidi. Kuwa Fungua Katiba yenu. Imeandikwa SURA YA PILI, imeandikwa Serikali ya JMTz. Kifungu cha 34. Hapo utaona pembeni imeandikwa Sharia namba 15 Ibara 9 ya mwaka 1984. Hiyo ipo ndani ya hiyo hiyo katiba yako ya mwaka 1977.

Na hata Jina la Katiba yenu hiyo unayoitaja na lini itaanza kutumika limetajwa katika Sharia namba 15 ibara 52 ya mwaka 1985, kifungu cha 152 .
152 .-(1) Jina kamili la Katiba ya Jamhuri ya Muugano waTanzania, ya mwaka 1977.
(2) Katiba hii itaanza kutumika tarehe 26 Aprili, 1977.
(3) Katiba hii itatumika Tanzania Bara na vile vileTanzania Visiwani.
_____
 


Muache Mwalimu apumzike kwa amani, haikupunguzii wala kukuongezea mkate mezani kwako kwa mwalimu kuitwa Baba wa taifa, ni kweli Mwalimu ni muasisi wa taifa hili, aliongoza mapambano ya taifa hili hadi kupata uhuru na akawa kiongozi wa taifa hili kwa miaka 23 kwa uadilifui mkubwa, bila kujilimbikizia mali wala kufisadi mali na pesa za wananchi, Mwalimu atabaki kuwa baba wa taifa letu upende usipende period. udini hauna nafasi katika vichwa vya watu wanaofikiri kwa kutumia UBONGO.
Leta post tujadili viongozi waliopo madarakani sasa hivi wachumia tumbo kwa sababu hawa ndio wana athiri maisha yetu katika wakati uliopo.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; Baba wa taifa, eeh Mungu mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani Baba wa taifa.
 

Bobuk,

Mie si mwenyeji wa Bukoba, Mimi ni mwarabu wa Oman mwenye asili ya Znz na nimezaliwa Znz. Ninayekuja kumpa jiko ni Mtoto wa Dereva wangu wakti nikiwa RDD mwanza marhum Julius Rweikiza. Ambaye watoto wake wote wanne niliwachukua toka 1992 alipofariki na ninaendelea kuishi nao mpaka leo.

Kwa kuwa wamekulia kwangu na amepata binti kutoka huko Kamachumu, ndio mimi na familia yangu wote tunakuja huko Kumpa jiko. Sheikh Ahmed Seif ndio mwenyeji wetu hapo.

Karibu sana kwani kesho kutwa al'Khamis tutacheza sana Nkurukumbi.(Hapa nimekikumbuka kikundi cha Taarab nilichokiasisi nikiwa Mwanza kiliitwa Mwanza Taarabu (MUTA) ambao walipiga wimbo huu maarufu sana wa Nkurukumbi (akisifiwa binti hapo).

Ok, sie tutakuja na Culture taarab kutoka Znz ambao wataingia Leo jioni saa 12 inshallah wakitokea Znz na kesho wataondoka kwa njia ya barabara kuelekea Kamachumu kutumbuiza.


Nyegera waitu



 
Kikao kilifanyika nyumbani kwako, mbele ya baba yako na mama yako....baada ya kukubaliana wakakutuma wewe
kuutangazia umma pale barazani kwenu kwa kutumia vuvuzela kama zile za kwenye world cup SA. Je, unalingine?

Toa hoja, kama huna nenda kwenye pombe kama kawaida yako, hayo ni matusi hayaruhusiwi humu wewe dogo.
 

Barubaru: Ahsante sana, ndiyo maana ninaipenda JF. Ingawa huwa tunatofautiana kwa kila kitu hapa JF hasa linapokuja suala la MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar lakini kwa hili umenikosha. Ninaomba uni PN ninaweza kukuona vipi ili angala tuongee mawili, matatu. Mimi naogopoa kujiweka hadharani maana wapo hapa akina ACP Msangi wanaweza kuni-Ulimboka!

Sasa kila siku unasema muungano mbaya! kumbe ulishawahi kuwa RDD Mwanza? Hivi Msukuma wa Mwanza anaweza kuwa RDD Pemba?

Well, naomba contact zako.
 



Unadhani Nyerere alikuwa anafikiria nini? Kuitwa Baba wa Taifa?

George Washington Wanamwita Hivyo kwasababu aliiunganisha USA

Lakini James Madison yeye ndio alikuwa kiongozi wakati wa katiba ikitengenezwa

* George Washington wanamwita Father of the nation, Hakuna kikao kilichokaa kumuita hivyo ni Historians ndio

Huwa wanaangalia na kuamua; na sio Vikao Vya Chama...
 
Amewasaidia sana mkuu ndo maana wanamfanya mwana heri .Wewe huoni wakatoliki walivyokaa vizuri.Mimi kama kiongozi dhaifu huyu nyerere ni @DHAIFU namba moja.Nahisi hajapumzika kwa raha
 
Hebu angalia Mkapa na Sinde Waryoba enzi za Mwalimu. Linganisha Mkapa wa sasa baada ya kifo cha Mwalimu. Hata nguo zao walikuwa wananyoosha kwa pasi ya mkaa!
 

Mimi ni mtu huru sana hususan nikiwa Tz ambako ni muda mchache tu swahibu wangu mkubwa ambaye ni khasimu wangu mkubwa sana hapa JF tumekutana nae leo wakti naelekea Tabata Sanene kuangalia maendeleo ya Petrol station ya mtoto wetu hapo Sanene. Na tulifika mpaka kwa Mfojo lakin tukakosa mishikaki.

Kifupi mimi nitakuwa Al Bashar Restaurant (Lebenese Hotel) mkabala na Herritage Hotel (opposite Exteleccoms) zamani tulikuwa tukiita Magoti. Hapo nitakuwepo kuanzia al'asr mpaka magh'rib nikisubiri wageni kutoka Znz wanakuja na Boti.

Lakin vile vile usitie khofu namba yangu ni +974 4457 4888.
Na hapa unaweza nipata kwa local number ya driver wangu 255 684 221077 au 255 777 420000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…