Kikao gani kiliamua Nyerere awe 'Baba wa Taifa'?

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Kikao gani cha serikali na chama walikaa na kuamua kumwita Mwl.Nyerere kuwa aitwe baba wa taifa? Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge mmoja simkumbuki jina alisema"kwakuwa Nyerere anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa apewe mh.Mkapa!" akaongeza "kwakuwa utawala wa Mkapa ulikuwa mzuri basi napendekeza bunge liridhie tubadili katiba ili mkapa agombee tena ili aweze kutawala kwa miaka 10 mingine?".

Mytake:
Huu ni mlolongo wa sintofahamu ndani ya Tanzania ambazo zimepaliliwa tangu enzi! Kwani Nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi kuchanganya dini na siasa?

Naomba tujadili hoja hii nyeti kwa ueledi nasio matusi na kejeli.
 
Kikao hiki kimeamua kwa sauti moja kukupa Bornvilla title ya ubaba wa Taifa. How do you see that?
 
Hii hoja umeibua ni nzito lakini kimsingi hata mataifa mengine kiongozi mkuu wa nchi hasa Rais wa kwanza wengi huamua kumpa heshima hy like marekani George washngton na kwingineko hvy kwa kigezo hicho hata Tanzania tukaamua kumpa Mwl Nyerere heshima hy si mbaya na wala haina tija yoyote!na ni kweli alichukia kuchanganya dini na siasa plus ukabila na ndivyo vitu vivyavyopelekea mataifa mengi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe alitambua hilo lakini pamoja na mapungufu yaliyojitokeza katika uongozi wake si vyema kumdhihaki au kejeli Tumpe heshima yake coz viongozi wengi sana wa nchi hii wamesoma kupitia maarifa yake aliyoyaweka kwa sababu wengi wetu hatukuwa na uono huo mwisho wa siku Mwl Nyerer atabaki kuwa Baba wa Taifa.
 
Najua unaelewa kwamba kiongozi kuitwa baba wa taifa fulani kunatokana na mchango wake mkubwa wa kuasisi taifa husika,umoja na maendeleo. Hakuna kikao kinakaa,bali ni matendo yake yanajionyesha kwa wananchi wake. Natambua kwamba wewe ni shabiki mkubwa wa siasa za udini na mpenzi wa chama cha CUF hapa jukwaani. Nakuomba wewe na wenzako mjikite ktk kutafuta maendeleo ya familia yako na jamii yako badala kila siku kuanzisha sredi za kipuuzi hapa jukwaani!
 
Hapa inaonesha ni jinsi gani watu wa JF walivyo mabogus katika kujibu hoja.Namshukuru CEMENT kwa kujitahidi kupanga hoja za msingi! Lakini kati ya wale wote walio comment hapojuu kumuondoa cement ni mabogus na hawafai kuwa GTs bali hao ni GSs.
 
maswali mengine siyo lazima kuayuliza, ukitaka kubadilisha mababa wa taifa utabadilisha mbaka utachoka, hebu fikiria kidogo tu, kama ulikuwepo kipindi cha kujifunga mkanda kisha akaja mzee ruksa basi ungekuja na hoja ya kuwa mzee ruksa anastahili kuwa baba wa taifa, na ukiendelea kuishi akija mmja wapo bora kuliko mkapa basi utapendekeza huyo awe baba wa taifa, nahisi we hujui ubaba wa taifa nini, siku zote mababa wa taifa ni wale waliozitoa nchi kwa wakoloni. hiyo ni heshima ambayo watanzania walikubaliana kwa ridhaa yao kumpa na alistahili kupewa kwa kutuongoza kupata uhuru, kanisa katoliki nalo lina mabo yake na linajua kuyaratibu kwa utaratibu wake, unashangaa mwanasiasa kutangazwa mwenye heri? pia kanisa limeishawahi kumtangaza mtawa wa kibudha wa kale kuwa mtakatifu japo hakuwa muumin wake ila waliangalia matendo yake akiwa duniani.
 
Hapa inaonesha ni jinsi gani watu wa JF walivyo mabogus katika kujibu hoja.Namshukuru CEMENT kwa kujitahidi kupanga hoja za msingi! Lakini kati ya wale wote walio comment hapojuu kumuondoa cement ni mabogus na hawafai kuwa GTs bali hao ni GSs.

Ni kweli cement amejibu vizuri hata mie nimempa like ila na wewe ulivyorudisha mipasho kwa kuwaita wali-comment mabogus na wewe umeangukia kulekule kwa walio wengi. Unajua majina kama haya huwa yanakuja automatically kutokana na mchango wako katika jamii na mara nyingi watu wengi wanavutiwa na jina unakuta linasambaa na mhusika analikubali hivyo ushofu hilo ni jina tu, ndio maana hata mwenyewe alikuwa hana complication akawa anajiita mwalimu ila wananchi wakawa wanamwita baba wa taifa. Kuna kipindi walimpa majina mengi akasema majina yote mmenipa lakini hili la mchonga------- sikubaliani nalo na enzi zake pia neno mheshimiwa lilikuwa halipo kwa viongozi kila mtu alikuwa anaitwa Ndugu yaani Ndugu Kingunge, Ndugu Bornvilla
 
Last edited by a moderator:
Wewe kama una chuki nae sisi hatuna chuki yeye kuwa baba wa taifa, kwanza kumchukia mtu aliekufa ni upungufu wa akili!. Baba wa taifa mimi namweshimu kwa sababu amelifanyia mengi taifa langu, hulazimishwi na wewe kumpenda! Au kumwita baba wa taifa!

Kuhusu wacatholic
kumpendekeza ili awe mtakatifu nadhani huo ni utaratibu wao waliojiwekea kwenye kanisa lao, kama wewe huamini hayo masuala ya utakatifu tuwaachie wenyewe wacatholic. Hiyo ni imani yao wenyewe.
 
kikao gani cha serikali na chama walikaa na kuamua kumwita mwl.nyerere kuwa aitwe baba wa taifa? Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge mmoja simkumbuki jina alisema"kwakuwa nyerere anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa apewe mh.mkapa!" akaongeza "kwakuwa utawala wa mkapa ulikuwa mzuri basi napendekeza bunge liridhie tubadili katiba ili mkapa agombee tena ili aweze kutawala kwa miaka 10 mingine?".

Mytake:
Huu ni mlolongo wa sintofahamu ndani ya tanzania ambazo zimepaliliwa tangu enzi! Kwani nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi kuchanganya dini na siasa?

Naomba tujadili hoja hii nyeti kwa ueledi nasio matusi na kejeli.

usiwe una kurupuka, fanya home work yako ili ujue sifa za kumfanya mtu afikie kutangazwa mtakatifu na kanisa katoliki, kuhusu siasa na dini alisema nchi haina dini ila watu wake ndo wenye dini, so yeye hakuwa mtu wa tz????

Kuhusu baba wa taifa hiyo ni maamuzi yako tu kumuita baba wa taifa au mzee nyerere kama wengine wanavyofanya.
 
Kikao gani cha serikali na chama walikaa na kuamua kumwita Mwl.Nyerere kuwa aitwe baba wa taifa? Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge mmoja simkumbuki jina alisema"kwakuwa Nyerere anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa apewe mh.Mkapa!" akaongeza "kwakuwa utawala wa Mkapa ulikuwa mzuri basi napendekeza bunge liridhie tubadili katiba ili mkapa agombee tena ili aweze kutawala kwa miaka 10 mingine?".

Mytake:
Huu ni mlolongo wa sintofahamu ndani ya Tanzania ambazo zimepaliliwa tangu enzi! Kwani Nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi kuchanganya dini na siasa?

Naomba tujadili hoja hii nyeti kwa ueledi nasio matusi na kejeli.

Kikao gani kilikaa mpaka baba yako akaamua kukuzaa kichwa maji kama wewe??
 
Back
Top Bottom