Kikao cha kero za muungano kiliishaje?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikao cha kero za muungano kiliishaje??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by King Zenji, Oct 13, 2008.

 1. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ,,,,,Ndugu wana JF,kile kikao cha KERO za muungano,kiliisha isha vipi???,Manake wakati tulikua tumekaa kutolea MISO yetu huko kwa akina CHACHA,mpaka CCM ikaporomoka,tungependa kujua na huku upande wa pili kile KIKAO MUHIMU kiliisha vipi,kwa yeyote mwenye taarifa pls atupatie,au kama kuna thread ya hii ishu,mwaweza nishika mkono pia,mimi ntafurahi,lakini kwa picha hii hapa,naona hali ilikuwa si mchezo,Manake kidole na macho baba SHAMHUNA.

  [​IMG]
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Waliishia....kuweka pending...hadi kikao..cha baraza mawaziri.....maana kero ni kubwa hawaziwezi waliokaa hicho kikao
   
 3. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wow. Ungekuwa unasoma course ya Journalism ningekupa A katika photo- Journalism. Unaweza kuiandikia kitabu hiyo picha. Hongera.
   
 4. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2008
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 340
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  picha moja tafsiri elfu moja!
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wamekubaliana mafuta yapo Pemba mengi kuliko ya Saudia na Iraq kwa pamoja...
   
 6. _SiDe_

  _SiDe_ Member

  #6
  Oct 16, 2008
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mzozo wa umilki wa BOT kutatuliwa kwa nyaraka kati ya Z'bar na Tanzania Bara
  Na Salma Said, Zanzibar.

  SAKATA la hisa za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) sasa limechukua sura mpya, baada ya kikao cha kamati ya kero za Muungano kukubaliana kila upande uwasilishe ushahidi wa nyaraka ilizonazo kuhusina na suala hilo.


  Akijibu swali katika baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema katika kikao cha mwisho cha kamati hiyo kilichofanyika mwanzoni mwa

  wiki hii, SMZ na Serikali ya Muungano walikubaliana kila upande uwasilisha nyaraka zinazohusiana na suala hilo kama ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.


  Waziri Hamza alisema kwa upande wa Zanzibar wana nyaraka hizo ambazo zitatumika kama ushahidi jinsi benki hiyo ilivyoanzishwa na hati za kila mwanachama kwa pande zote za muungano.


  ''Napenda kueleza kwamba SMZ iko makini sana kufuatilia suala hili kupitia Wizara ya Fedha na Uchumi, Ofisi ya Waziri Kiongozi na Uratibu wa Uchumi na Uhusiano wa Kimataifa,'' alisema waziri huyo.


  Alisema mara baada ya kuthibitishwa kwa hisa za SMZ BoT, hatua nyengine zitafuata na kuwahakikishia wajumbe wa baraza kwamba SMZ inafuatilia suala hilo kwa makini.


  Hamza aliwaahidi wajumbe kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi katika kikao kijacho cha kamati ya pamoja inayoshughulikia kero za muungano.


  Alisema katika kikao kilichopita cha kuzipatia ufumbuzi kero za muungano wamekubaliana kwa pamoja kwamba Katibu Mkuu Kiongozi atoe kibali kwa Benki Kuu kutoa nyaraka zinazoonyesha mmiliki wa taasisi hiyo.


  Swali la msingi liliulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Magogoni (CCM), Daud Hassan Daud aliyetaka kujuwa hatma ya suala la hisa za Zanzibar BOT.


  ''Tulikubaliana kwamba Katibu Mkuu Kiongozi atoe kibali cha kupatikana kwa nyaraka zinazoonyesha mmilikii wa taasisi hiyo,'' alisema Waziri Hamza.


  Alithibitisha kwamba kuna mgogoro wa umiliki katika taasisi hiyo, huku Zanzibar ikidai kwamba ina hisa zake katika benki hiyo na kwamba wana uhakika SMZ imechangia uanzishaji wa benki hiyo.

  Source: Mwananchi
   
 7. S

  Sabri-bachani Member

  #7
  Oct 16, 2008
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nawe nawe. Acha kudek-shia na hizo tashtiti zako. Kwani na kule kijijini kwenu yapo?
   
 8. F

  Falconer JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2008
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  wacheni porojo. Wazanzibzri wamechoka kutawaliwa. Wakati umefika kujikomboa na siasa za chuki na kunyanyaswa. Miaka 44, muungano wakulazimishwa. Tumeuliza suala dogo tu, toeni ushahidi wa karatasi alipotia saini Nyerere na Karume kuunganisha nchi mumeshindwa. Tumetaka mutuonyeshe ushahidi katika BOT, kwani Zanzibar walitoa fedha ya kuanzisha Benki jee, nyinyi munao ushahidi wa fedha mulizo toa kuanzisha BOT, hamuna kwa ufupi mulicho nacho n USANII tu hamuna mpya.
   
Loading...