Kikao cha kamati ya fedha jijini Arusha chavunjika tena leo Julai 21, 2017

tokyo1sofala

Member
Nov 12, 2010
23
7
City%2BAr.jpg

MBUNGE LEMA NA NAIBU MEYA WAMUONYA MKURUGENZI.

Kwa mara nyingine madiwani wa kamati ya fedha jijini Arusha leo wamegomea kuendelea na kikao cha robo ya nne cha kamati hiyo kwa madai kuwa hadi wafanye kikao cha robo ya tatu kwanza ambacho pia walikigomea mwezi April mwaka huu. Wajumbe hao wakiongozwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema walisema wapo tayari kwa lolote litakalowatokea lakini hawapo tayari kuendelea na kikao. Walisema kikao cha robo ya tatu kiligomewa na wajumbe kwa kuwa serikali ilimkamata meya wao Kalisti Lazaro akitoa rambirambi kwa kukusanya watu bila kibali.

Hata hivyo meya huyo hakuwepo katika kikao hicho cha leo na haikufahamika alipo tangu alipovuliwa madaraka ya ukatibu wa chadema mkoa wa Arusha wiki iliyopita. Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw. Athumani Kihamia pamoja na wakuu wa idara wote walishangazwa na mgomo huo wa madiwani kwa kuwa vikao vya kamati hiyo vya miezi ya April na mei vimefanyika kama kawaida. Diwani wa viti maalum katika kamati hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Sabina amemdokeza mtoa habari hizi kuwa watafanya hivyo hadi mkurugenzi huyu atakapoondolewa au posho zetu alizozikata kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya zitakaporejeshwa na hayo ni maagizo maalum ya mbunge na viongozi wa chama. " Katika baraza la madiwani la mwezi huu mei tutamkataa mkurugenzi huyu ili watafute pa kumpeleka , tangu afike hali imekuwa mbaya kwa watumishi na madiwani.

Tumemjulisha Katibu mkuu ofisi ya raisi tawala za mikoa na selikali za mitaa mara kadhaa tunaamini atatuelewa. Wampeleke wanapotaka ni dikteta sana hata Kaliua waliwahi kumkataa. Anamsikiliza DC na RC sisi anatuona kama watu wasiokuwa na maana, Safari hii tumemchoka na mbunge Lema ameapa kutorudi nyuma kwenye hili" alisikika naibu meya akilalama muda mfupi baada ya kikao kuvunjika. Alipotafutwa Mkurugenzi aelezee hili jambo hakupatikana ingawa mkuu wa kitengo kimojawapo katika jiji la Arusha amedokeza kwamba mvutano huu hautakwisha kwa kuwa madiwani hawa wa Chadema hawayatambui mamlaka na majukumu ya DC na RC kuhusu usimamizi wa jiji na mkurugenzi huyu hapendi kupelekwa pelekwa yeye anacheza na kanuni tu. Hadi sasa hakuna shughuli yoyote ya jiji iliyowahi kusimama licha ya madiwani hawa kumgomea mkurugenzi huyu mara kwa mara karibu vikao 5 sasa kwa nyakati tofauti vimevunjika.

NI KUSUBIRI NA KUONA NINI KITATOKEA TAREHE 28 MEI SIKU YA
BARAZA LA MADIWANI
 
Back
Top Bottom