Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,932
- 31,178
Heshima kwenu wanajamvi.
Leo Jumapili ya tarehe 17 March 2019 nilitembelea viunga vya wilaya ya Arumeru kwa uchache labda nivitaje viunga vyenyewe Ngurdoto,Ngongongare hadi gate la Arusha National Park na Majibya Chai.
Katika pitapita yangu nilifanya udadisi juu ya kikao cha Washili na athari zake kwa Mbunge mtimuliwa (nsataafishwa) Mh Nassari.
Nilifanya mahojiano na zaidi ya wananchi 50 wa rika mbali mbali wazee,Vijana,Wanawake na wanaume.
Mrejesho wa mahojiano yangu na wana Meru ni kama ifuatavyo,
Gari lililotumika kutoa matangazo ya Mkutano ni mali ya CCM.Lillitangaza Mkuu wa mkoa Mh Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya wangehutubia.
Katika mkutano Mshili Mkuu na baadhi ya wakereketwa wa CCM wakawa vinara wa kuongea.Mkuu wa Mkoa na Wilaya walijiweka kando.
Kwa mujibu wa taratibu wa mila za wameru Vikao vya Washili kinafanyika chini ya mti wa Mringaringa na wanawake hawaruhusiwi kushiriki wala kuhudhuria.
Mshili Mkuu Mzee Sumari ndugu yake wa ukoo alishindwa katika uchaguzi na Mh Nassari.
Vikao vya washili ni marufuku kuingiza masuala ya siasa.
Washili waliohudhuria ni chini 2% ya Washili wote wa Meru.Mh Nassari pia ni Mshili kwa mujibu wa nafasi yake ya ubunge alipaswa kuitwa kwa nafasi yake.
Washili wa Meru wamegawanyika wale wa CCM wanafurai wa CDM wamenuna wanataka katiba ifuatwe.