hydroxo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 2,808
- 5,585
Usanisinuru(photosynthesis);ni kitendo cha kikemia na kibaiolojia ambapo mimea ya kijani(green plants) hubadili nishati ya mwanga wa jua kuwa nguvu ya kikemia inayohifadhiwa na mmea katika sukari aina ya stachi.
Kitendo hiki cha usanisinuru hufanywa na mimea ya kijani(green plants) kwa sababu mimea ya kijani inamiliki kiwiti(chloroplasts) zenye chembe ndogo ndogo za kijani(chlorophylls) zenye uwezo wa kuvuta na kubadili mwanga wa jua kuwa nishati ya kikemikali.
Ili kitendo hiki kifanyike kinahitaji; maji,na gesi ya kaboni daioksaidi kutoka angani hivyo basi kitendo hiki pia usawazisha kiwango cha gesi hii ambayo ikizidi huwa sumu kwa mwanadamu.
Baada ya kitendo hiki kukamilika huzalisha; maji, sukari,na gesi ya OKSIJENI inayotufanya mimi, wewe na viumbe hai wengine tuweze kuishi kwani kila siku tunaitumia katika upumuaji na uvunjaji wa chakula mwilini (respiration) kitendo kinachotupa nguvu zinazotusaidia katika shughuli za maisha yetu ya kila siku.
HAKUNA MIMEA HAKUNA MAISHA.