Kijiwe cha politiki......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kijiwe cha politiki.........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M'Jr, Mar 20, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Jana nilipita kidogo kijiwe cha politiki ambacho kama vilivyo vijiwe vingi kwa sasa gumzo ni uchaguzi wa Arumeru Mashariki. Katika mengi yaliyokuwa yakizungumzwa hili likanigusa nikaona sio vizuri likapita bila kulileta hapa. Nalo ni lile la kumteua Rais Mstaafu BWM kuwa kiongozi wa kampeni za CCM kule Arumeru.

  Katika mjadala kuna waliosema CCM walikosea kwakuwa siasa za enzi zake ni tofauti na za sasa ambazo zimejaa vijana ambao hawaongei kwa tafisida hali ambayo Mzee BWM hajaizoea hivyo hakuwa anafaa kuwekwa kwenye kinyang'anyiro hicho.

  Wengine wakasema kuna watu wengi tu ambao kimsingi wangeweza kuwa katika nafasi hiyo kama kina Wasira (ambaye tayari amejiunga huko sasa) Chiligati, Nape na mmoja akahoji hivi kazi ya Katibu wa CCM ni nini?

  Sasa mi nikaona nililete hili hapa, hivi ni kweli kuwa CCM walikosea kumpa kazi hiyo mzee BWM? Karibuni
   
Loading...