Kijiografia/kihistoria ama kiutamaduni: mlima kilimanjaro unatakiwa kuwa Tanzania au Kenya?

Wewe huna unachojua......Rwanda na Burundi ulizotaja humo zilikuwa ni sehemu ya Tanganyika
 
Wadau mara kadhaa tumesikia wakenya wakisema mlima kilimanjaro uko kwao? Ninaomba kueleweshwa kwa undani kabisa kuhusu jambo hili. Karibuni.
Kihistoria pia pwani nzima ya Kenya ni sehemu ya Tanzania.
Huo mlima wanavyoungangania nahisi tukae kikao Kenya wapewe mlima na sisi tuchukue pwani nzima kuanzia Lamu, Malindi hadi Mombasa.
 
zamani kabla ya ukoloni hakukuwa na mipaka na mpaka leo kule rombo watu wanajivukia tu na bodaboda ukienda arusha kule wamasai wanavuka tu na ng'ombe zao hawajui cha mpaka wala nini. hawa wajaluo wa tanzania wengine wako kenya wakina raila odinga na kule vijijini kwao musoma wanajivukia tu kila siku tena kuna watanzania wanamshamba kenya wanaenda kulima asubui na wanaludi kulala jioni tanzania bila kujali mipaka.all in all mlima upo kote tanzania na kenya manake ukiwa kenya unauona na kuna mito inatiririsha maji kwenda kenya kutoka mlima kilimanjaro ila kwa kule kenya kumekaa vibaya huwezi kupanda
 
Uongo
 
Nadhani huna uhakika wa unaloliandika. Kama kabla ya wakoloni kuweka mipaka 1884-1886 Afrika ilitawaliwa kimakabila (chiefdoms) Kenya haina haki ya kudai Ml Kilimanjaro. Watu waliokuwa wanaishi maeneo ya mlima huo kuuzunguka pande zote ni wachaga. Na hao ndio walioko huko hadi leo. Nchi ya Kenya haina kabila la wachaga. Makabila ya Kenya yanayopakana na wachaga ni wasonjo na wakamba. Kirahisi ni kuwa kwa kuwa hakuna sehemu ya wachaga iliyoko Kenya na wachaga wote ni Watanzania, Mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania. Hakuna porojo nyingine yoyote inayoweza kupingana na hilo.
 
Wadau mara kadhaa tumesikia wakenya wakisema mlima kilimanjaro uko kwao? Ninaomba kueleweshwa kwa undani kabisa kuhusu jambo hili. Karibuni.
mimi naishi chini ya mlima. napakana na kenya kama mita 2. ule mlima bila shaka ni wa kenya. hata watu wa pale tulipaswa kuwa wa kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…