Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 68
- 1,268
Kuanzia siku za hivi karibuni tumeshuhudia gharama za kutoa kontena bandarini zimepandishwa mara tatu zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Kwamba hapo awali gharama za kusafirisha kontena moja kutoka China mpaka bandari ya Dar ilikuwa milion sita. Lakini kwa sasa kontena hilo linasafirishwa kwa milion 23. Mamlaka za serikali zinadai gharama hizo kuongezeka zimesababishwa na uharamia baharini.
Sasa jambo la kushangaza ni kwamba gharama hizi kupanda ni kwa bandari ya Tanzania pekee? Mbona nchi zingine gharama zimebakia kuwa zilezile? Hapa chini nimeambatanisha ushahidi wa gharama za kusafirisha kontena kutoka China mpaka Mombasa Kenya ambayo ni takribani milion 5 kwa kontena wakati Tanzania ni milion 23.
Swali la kujiuliza je; huo uharamia wa baharini ni kwa ajili ya meli zinazokuja Tanzania pekee? Ama nchi za wenzetu wao wana bahari zao zisizokuwa na uharamia? Je; ni kweli kwamba huu ni mkakati wa serikali na DP World?
Mpaka jana makampuni matatu ya usafirishaji kutoka Zambia yanatafuta ofisi Kenya kwa ajili ya kutumia bandari ya Mombasa. Pia kuna kampuni kadhaa za Congo DRC nazo zipo katika mchakato huo kuhama bandari ya Dar na kwenda Mombasa kwa ajili ya kukwepa gharama hizi zilizoongezeka.
Tunaitaka serikali ije na majibu yanayoeleweka kuhusu jambo hili na majibu hayo yawe ya kurudisha gharama zilizokuwepo awali badala ya kuleta maneno ya kitapeli. Gharama zikiendelea kuwa hivi maana yake tutegemee vitu kupanda bei mara tatu zaidi, kama kuna Jeans ๐ ulikuwa unanunua elfu 30 jiandae kununua laki 1. Ugumu wa maisha utaongezeka mara dufu zaidi.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.