KERO Kijiji cha Mayonje (Sumbawanga), tangu Novemba 2025 hatuna maji baada ya bomba kupasuka

KERO Kijiji cha Mayonje (Sumbawanga), tangu Novemba 2025 hatuna maji baada ya bomba kupasuka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ndugu zangu, hali ya upatikanaji wa maji katika Kijiji cha Mayonje, Kata ya Milepa katika Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini, imekuwa ya kusikitisha sana, tangu mwezi wa 11, 2025 mwanzoni baada ya Uchaguzi Mkuu mpaka sasa, tumekuwa tukiishi bila huduma ya maji safi.
1770549369736_021917.jpg
Chanzo cha tatizo ni bomba kubwa linalosambaza maji kijijini kwetu ambalo limepata hitilafu na kupasuka, lakini hadi leo halijatengenezwa.

Kibaya zaidi, kuna maneno yanayoenea kuwa tatizo hili linatokana na siasa za chuki; inasemekana baada ya diwani aliyepita kushindwa kwenye uchaguzi, ametuma vijana wake kukata bomba hilo kwasababu yeye ndio alisaidia bomba hilo kuunganishwa, akisema huyo diwani aliyeshinda (wa upinzani) ndio arejeshe huduma hiyo.

Hivi sasa, hali ni mbaya sana, tunaishi kwa kutegemea maji ya mvua, jambo ambalo sio sio sawa. Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) mje mtusaidie.

Mamlaka za chini zinasema zimefikisha suala hilo ngazi za juu, lakini kutokana na uhasama huo wa wakisiasa hata wao wanasema hakuna kingine wanachoweza kufanya zaidi ya kusubiri, na kila kitu ndio imeishia hapo, hakuna tena juhudi zinazofanyika kuhakikisha huduma hiyo inarejea.

Sisi Wananchi tulikuwa tayari hata kuchangia ili turejeshewe huduma hiyo lakini hatuoni juhudi zozote kutoka kwa viongozi wetu.

Tunaomba Serikali itusaidie, maji ni uhai na hatuwezi kuendelea hivi kwa sababu ya malumbano ya kisiasa.

Pia soma ~ Waziri Aweso atoa maelekezo mabomba ya Kijiji cha Mayonje - Sumbawanga yatangenezwe na huduma ya maji irejee
 
Deal na idara ya maji itakua huko idara ya maji sio wawajibikaji mbona huku mijini wakisikia bomba limepasuka chap Kwa haraka
 
Sumbawanga tena? Logeni mpate maji
 
Kinukishe kama Lissu, piga kiberiti ofisi za idara ya maji
 
Wananchi wa Kijiji cha Mayenje, kilichopo Kata ya Milepa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (DC), hatuna huduma ya maji safi kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu.

Chanzo cha tatizo hili kinadaiwa kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa diwani wa kata ya Milepa kukata mpira wa bomba linaloleta maji kijijini, wakieleza kuwa ni kutokana na hasira baada ya mgombea wao kukosa kura za kutosha katika uchaguzi mkuu uliopita. Inasemekana waliamua kufanya hivyo wakidai diwani mpya (wa chama pinzani) atumie gharama zake mwenyewe kurejesha maji, wakisisitiza kuwa maji yaliyokuwa yakitumika yaliletwa na chama chao.

Hali hii imekuwa mzigo mkubwa kwa wananchi, kwani wanalazimika kutumia maji ya mtoni ambayo si salama kiafya. Hadi sasa mamlaka husika zimekaa kimya, japokuwa kuna taarifa kuwa baadhi yao wametishiwa kuwa wakichukua hatua za kurejesha huduma ya maji watapoteza ajira zao.

Aidha, madai yanaeleza kuwa suala hili linahusishwa na Mbunge Deusi Sangu, akidaiwa kuzuia maji yasirejeshwe kwa sababu kijiji hiki kilichangia kumuangusha diwani wa awali, ambaye inasemekana ni swahiba wake.

Migogoro ya kisiasa inaumiza hata wananchi wasiokuwa na vyama vya siasa. Wito wetu ni kuomba huduma ya maji irejeshwe haraka kama ilivyokuwa awali.

1770549369736_021917.jpg
1770549369725_021850.jpg
 
Back
Top Bottom