Kijerumani ni kama Kiswahili

Sep 12, 2018
32
27
kwanini?
Lugha ya kijerumani ni lugha yenye herufi sawa na za kiswahili kasoro chache tu na hazifiki 5.

Hakuna kitamkwa kilichopo katika lugha ya Kijerumani ambacho hakipatikani katika kiswahili.

Ndio lugha rahisi zaidi kwa mswahili zaidi ya lugha nyenginezo barani Ulaya.

Kwanini ujifunze kijerumani?
Ni lugha unayoweza kuitumia sehemu yeyote barani Ulaya, ukaeleweka. Wajerumani ni watu wanaopenda kuranda, wacheshi, wachangamfu na nirahisi kukuzoea. Wajerumani wanatajika kuwa na hisia za utu, wanajali.

Ukiacha Wamarekani ni Wajerumani ambao wageni wake hutoa baghashishi nzuri. Nikiwa kama Mtembeza Wageni (tour guide visiwani Zanzibar) Wajerumani si wageni wanaolaumu kama mambo yakienda kombo; kuna mataifa ukiyatembeza utajuta mfano Wafaransa ni wageni wanaopenda kulaumu sana, Wataliano ni wasumbufu kiasi.

Kijerumani lugha rafiki sana kwa mwanafunzi ambaye ndoto zake ni kusoma Ulaya, Wajerumani wengi ni wasomi unaweza kujifunza mambo mengi unapoijua lugha yao kwa vile lugha ya kisayansi na shahada ya chuo cha ujerumani inaweza kukuwezesha kufanya kazi duniani sehemu yeyote.

kwa wale wanaopenda wanawake wa kizungu, basi kuna habari njema kwao ya kwamba Wanawake wakijerumani ni rahsi zaidi kuanzisha mahusiano na Muafrika kuliko wanawake wengine wa barani ulaya.

Kuna nchi chungu nzima kama vile Japan, Urusi na USA wanakuzingatia zaidi ukienda kuomba kazi huku ikiwa kijerumani ni lugha unayoifahamu.

Kama nilivozungumza awali Wajerumani wengi ni wenye utu hivo wanapenda kutafta taasisi na mashirika wasaidie, ukiwa unaelewa kijerumani basi ni fursa kwako kuwa mkalimani
___________________________________
ITAENDELEA Part 2
#G-less Antonopoulos
ZANZIBAR..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza inawezekana wewe unafahamu Kijerumani, lakini katika lugha rahisi sana kusomekana na inayofanana katika kusoma maandishi yake kama yalivyo au kama yalivyoandikwa ni lugha ya kihispani.

kiasi kwamba ukimpa Mhispania asome kiswahili ana tiririka kama maji, ila kwa upande wa bakshishi labda wewe kidogo una nyota na wajerumani,hawa jamaa huwa wgumu sana hadi unaweza wafananisha na yule mtawala wao aloangushwa wakati wa vita ya pili dunia.
 
Kwanza inawezekana wewe unafahamu kijerumani,lakini katika lugha rahisi sana kusomekana na inayofanana katika kusoma maandishi yake kama yalivyo au kama yalivyoandikwa ni lugha ya kihispani,...
Kwa bahati kihispain sikijui lakini marafiki zangu wengi wanazungumza kwaiyo huezi kunidanganya ,bado mspain hawezi kutoa lafudhi ya kiswahili kama utakavompa mjerumani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitaliano mswahili hawezi kusoma kama ilivoandikwa lakini kijeruman unaweza

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni lazima ukaze koo. La sivyo matamshi yako hayataeleweka. Ndiyo maana inaitwa lugha ya kiume. Kiswahili,Kiarabu, na kiitaliano ni lugha laini.

Rahisi mno kujifunza. Mkuu, tunazungumzia tulikopitia, hatufurahishi genge ili mradi umesema. Malugha haya tumeyavuruga kwa vinywa vyetu na kuwafundisha wengine pia. Experience is the best teacher.
 
Kwa bahati kihispain sikijui lakini marafiki zangu wengi wanazungumza kwaiyo huezi kunidanganya ,bado mspain hawezi kutoa lafudhi ya kiswahili kama utakavompa mjerumani

Sent using Jamii Forums mobile app
Fanya utafiti wa harakakabisa,mchukue mhispania,muandikie kiswahili halafu mwambie asome kama ulivyoandika,halafu mchukue mjerumani muandikie kiswahili halafu mwammbie asome kama ulivyoandika, utakuja kuniambia.

Usitumie marafiki sana katika tafiti za lugha jitumie mwenyewe,na kwa kuwa wewe ni muongoz wageni, bado siwezi amni kama hujui chochote hata salamu tu ya lugha ya kispania labda kama hujawahi kukuitana kabisa na hizo sura za Wahispania.
 
Tumekusikia. Nakubaliana nawe kwa mengi isipokuwa kuwa lugha rahisi. Kijerumani ni lugha ya kiume lakini hufi njaa ukiifahamu. Ni lugha ya fedha. Lugha rahisi ulaya ni kiitaliano. Ni kama kiswahili tu.
Sawa kabisa, hata hii lugha siyo ngumu, ndugu yake muhispania kabisa, hawa ni damu damu.
 
Fanya utafiti wa harakakabisa,mchukue mhispania,muandikie kiswahili halafu mwambie asome kama ulivyoandika,halafu mchukue mjerumani muandikie kiswahili halafu mwammbie asome kama ulivyoandika,utakuja kuniambia,

Usitumie marafiki sana katika tafiti za lugha jitumie mwenyewe,na kwa kuwa wewe ni muongoz wageni, bado siwezi amni kama hujui chochote hata salamu tu ya lugha ya kispania labda kama hujawahi kukuitana kabisa na hizo sura za waspania,
Lugha unaweza kujua maamkiz na maongez muhimu kama hayo Ila haimaanishi n fundi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lugha unaweza kujua maamkiz na maongez muhimu kama hayo Ila haimaanishi n fundi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja kubwa hapa hatujadili ufundi wa lugha,kwa sababu hata ingawa sisi tumezaliwa katika jamii ya wazungumzaji wa kiswahili lakini bado mfundi wa kiswahili ni wa kutafuta sana, hapa tunazungumzia urahisi wa lugha na lugha gani ambayo ni rahisi na yenye kufanania na kiswahili.
 
Sawa kabisa, hata hii lugha siyo ngumu, ndugu yake muhispania kabisa, hawa ni damu damu.
Spanish ni rahis sana, niliwahi kuanafatlia tamthilia flani ilikua nawamexico na waamerica weusi walikua wakitumia sana espanol, adi kuimaliza nilikua nimepata mawili matatu kama gringo na pandejo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Idd Ninga na G-less Antonopoulos , kila mtu aweke sentensi Kama 5 hivi (za kihispania na kijerumani, pia kwenye mabano jinsi ya zinavyotamkwa), wasomaji waamue wenyewe ipi inafanana na Kiswahili kwenye kusoma.

Zanzibar bado inalipa kwa kazi ya kuongoza watalii ? Najua porini (Arusha ilikuwa inalipa sana, tena sana ila watu wanabania sana kule, hawakupi pasi, Zanzibar haiko hivyo).
 
Idd Ninga na G-less Antonopoulos , kila mtu aweke sentensi Kama 5 hivi (za kihispania na kijerumani, pia kwenye mabano jinsi ya zinavyotamkwa),wasomaji waamue wenyewe ipi inafanana na Kiswahili kwenye kusoma.
Zanzibar bado inalipa kwa kazi ya kuongoza watalii ? Najua porini (Arusha ilikuwa inalipa sana, tena sana ila watu wanabania sana kule, hawakupi pasi, Zanzibar haiko hivyo).
HOLA(hola)
DONDE(donde)
DIGA ME(digame)
TE AMO (teamo)
YO HABLO MUCHO(yo hablo mucho)
HASTA LA VISTA (HASTALA VISTA)
maneno machache sana ndo husomeka tofauri kama clip inavyoonysha,ll-y mfano.
 
Fanya utafiti wa harakakabisa,mchukue mhispania,muandikie kiswahili halafu mwambie asome kama ulivyoandika,halafu mchukue mjerumani muandikie kiswahili halafu mwammbie asome kama ulivyoandika,utakuja kuniambia,

Usitumie marafiki sana katika tafiti za lugha jitumie mwenyewe,na kwa kuwa wewe ni muongoz wageni, bado siwezi amni kama hujui chochote hata salamu tu ya lugha ya kispania labda kama hujawahi kukuitana kabisa na hizo sura za waspania,
Hao watu nawapata wapi mkuu!?
 
Kma unajua english kispanishi kinakua rahis, ata matumiz ya grammar yanafanana pia. Tofaut nindogo sana kwenye matamshi hasa hayo maneno yenye ivo vialama kwa juu

Do you speak English? - Yes, I speak English, Spanish, and French.

¿Hablas inglés? - Sí, hablo inglés, español y francés.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingine kijerumani
Mwingine kihispania
Mwingine kiitaliano
Kila mmoja aweke maneno ya lugha yake ili tupime lugha rahisi
 
Kma unajua english kispanishi kinakua rahis, ata matumiz ya grammar yanafanana pia. Tofaut nindogo sana kwenye matamshi hasa hayo maneno yenye ivo vialama kwa juu

Do you speak English? - Yes, I speak English, Spanish, and French.

¿Hablas inglés? - Sí, hablo inglés, español y francés.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hap kwenye ñ ndo patasumbua kidogo, lakini mtu anaelekezwa na kuelewa muda mfupi kabisa na ni kweli ukijua kiingereza kihispania kinakua kirahisi zaidi.
 
Kma unajua english kispanishi kinakua rahis, ata matumiz ya grammar yanafanana pia. Tofaut nindogo sana kwenye matamshi hasa hayo maneno yenye ivo vialama kwa juu

Do you speak English? - Yes, I speak English, Spanish, and French.

¿Hablas inglés? - Sí, hablo inglés, español y francés.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mh.... Asili ya hizi lugha ni mbili tofauti, Kihispania na Kireno (zipo nyengine pia), zina asili ya Kilatini, kingereza sio Kilatini ila ina maneno mengi ya Kilatini lakini ukija mofolojia na sintaksi ni tofauti sana .... Ni hayo tu mkuu
 
Kwa bahati kihispain sikijui lakini marafiki zangu wengi wanazungumza kwaiyo huezi kunidanganya ,bado mspain hawezi kutoa lafudhi ya kiswahili kama utakavompa mjerumani

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unabisha tu lakini duniani lugha raisi kwa mswahili kujifunza ni Spanish na Italian. German na French ni lugha ngumu kuliko hizo mbili.

Anyways ni mtizamo wangu. Labda inategemea mtu na mtu.
 
Back
Top Bottom