Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,565
- 188,769
Habari!
Kuna wimbi kubwa la vijana kujaribu kuishi maisha yenye standard za juu huku maisha yao bado kabisa hayana msingi imara kuishi hivyo.
Kijana usikurupuke katika haya maisha kutokana na maisha ya wengine au msukumo wa hisia bila kufanya tafiti yako binafsi, kweli ni jambo zuri sana na jema kuishi katika standard ambazo kila siku unatamani kuishi kulingana na upambanaji wako.
Wengi wanafanikiwa kupambana na utafutaji, tatizo linakuja kwenye mipango baada ya yote(Upambanaji). Hapo ndipo imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wa sasa kurukia maisha ambayo hatoweza kuishi kwa muda mrefu.
Na kama atafanikiwa kuishi hayo maisha ambayo yapo juu ya hali uliyonayo basi cashflow za IN pamoja na OUT zitabalance na hatoweza kukua zaidi ya hapo alipo kwa sasa ndani ya miaka kadhaa. Au moja kwa moja kijana akaishi kwa madeni ya muda mrefu.
Wengi wao utawakuta wakilaumu kwa sababu mbalimbali ikiwepo shughuli wanazofanya halizipi.
La hasha! Kumbe mchawi ni yeye mwenyewe kwa kuchagua maisha yenye standard za juu/ lifestyle huku hakuna miamba ya kushikilia hayo maisha aliyochagua kuishi.
Hivyo basi kijana kuwa makini sana hapo kwenye maisha unayochagua ishi fanya kulingana na ulichonacho huku ukiweza kujipanga kujenga nguzo imara za kusaidia kuishi maisha ya ndoto zako kwa kipindi kirefu bila kuyumbayumba.
Nawasilisha Mzee Mkoloni
Cc: Kichwa Kichafu