Jayspeed
Senior Member
- Feb 23, 2014
- 156
- 168
Kijana mmoja alikua na ndoto siku moja awe mwandishi wa filamu na muigizaji mkubwa nchini Marekani..
Alijaribu kuandika baadhi ya filamu nyingi na kuzipeleka kwa waongozaji filamu wakubwa kipindi hicho lakini kila alikua akipeleka inakataliwa.
Watu wengi walimuona anapoteza muda na fedha nyingi za kufatilia mambo ambayo anakataliwa yeye hakukata tamaa ilikua ni ndoto yake lazima aishi ndani yake...
Ilifika kipindi hela zilimuishia aliamua kumuuza mbwa wake kwa thamani ya dola za kimarekani $50 aliumia sana kumuuza mbwa huyo ambae alikua kama rafiki kwake ila alikua tayari kupoteza kila kitu ili aishi ndani ya ndoto zake.
Baada ya kumuuza mbwa yule na kwa hela ile alifanikiwa kupeleka filamu yake na mwisho wa siku ilikubaliwa lakini alikataliwa asiigize yeye aliambiwa hana muonekano mzuri wa kuigiza..alivoambiwa vile alichukua filamu yake na kuondoka alikataa kuwauzia sababu lengo lake ni kuigiza pamoja na yeye awe muigizaji bora duniani hakutaka kuuza tu ili apate pesa maana kama ni pesa hakushindwa kuzitafuta au kwenda kuajiriwa mahali na alkua ana shahada yake..lengo lilikua ndoto zake zitimie... Muongozaji mmoja alimuita kijana yule na kumuambia kama yupo tayari kuigiza bas asiuze ule muongozo wa filamu bali awape bure na yeye ataigiza hela yake atapewa baada ya mauzo ya filamu yake..kijana alikubaliana na hilo kwa mikono miwili alikubali hatimaye akacheza filamu ile na ikawa filamu bora kwa kipindi hicho aliingiza fedha nyingi sana alirudi na kumnunua mbwa wake yule mara mbili ya hela aliyomuuzia $100...kijana huyo ni mtu mkubwa na anaheshimika mpaka sasa ndani na nje ya marekani kutokana na kazi zake za filamu hapo namzungumzia SYLVESTER HALLONE jina maarufu kama RAMBO..
Tujifunze kuishi ndani ndoto zetu kama RAMBO vijana mara nyingi tunazikimbia ndoto zetu kwa sababu unahofia kupoteza muda..unahofia kuchekwa na ndugu au marafiki hapo ndo tunajikuta tunaishi ndani ya ndoto za watu wengine..ukiishi ndani ya ndoto ya mtu mwingine hutapata furaha ya maisha kamwe sababu wakati mwingine ndoto za mtu huyo ni mbaya na za kutisha. Ndoto za mtu zinaumiza sababu utafanya kitu ambacho maishani kwako hakikupi raha hata kidogo..
Huwezi kutamani kuwa msanii wa muziki mkubwa halafu uone raha ya kuwa mtangazaji.. Watu wengi hawana furaha maofisini sababu kazi wanazozifanya sio moja ya ndoto zao ila anafanya sababu anaitaka pesa tu... Pesa tamu ni ile unayofanya kazi unayoipenda na siku zote kazi unayoipenda unaifanya kwa makini zaidi..
Sikushauri uache unachofanya kwasasa hapana sababu kuacha ni maamuzi yako binafsi ila ukiamua kuacha mwenyewe na kufanya unachopenda pia ni vizuri zaidi
..
.
..
.
.
.
.
..
By Jay Speed