Kijana hamad ali kaimu aliyeuwawa mikononi mwa vyombo vya dola

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
100_1007kk.jpg Baba wa marehemu anasimulia mtoto wake alikamatwa siku ya sikukuu mosi akipeleka ng'ombe wake malishoni na akiwa na pesa shilingi elfu 80 ambazo shilingi elfu 30 alichangiwa na baba yake. Pesa hizo alikusudia kwenda kununua godoro baada ya kumaliza kufunga ng'ombe wake. Baba mtu alipomuona mtoto wake nje ameshikwa na polisi wasiopungua 20 alikwenda kusikiliza kumezidi nini? La haula baba mtu alipigwa na kutakiwa aondoke mara moja. Baba mtu baada ya kushuhudia mtoto wake akipata kipigo hakua na cha kufanya aliondoka na kumwacha mtoto wake mikononi mwa askari hao. Baada ya kufika jioni na kuona mtoto wake hajarejea, baba mtu alikwenda kituo cha polisi Mwanakwerekwe kumtafuta mtot wake lakini alimkosa ndipo alipokwenda kito kikuu cha polisi Madema na kumkosa pia. Ndipo baadae akapokea simu kuwa mtoto wake ameshafariki na yupo chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mnazi mmoja na kumkuta akiwa katika hali kama hiyo.

Zanzibar
 
View attachment 69730Baba wa marehemu anasimulia mtoto wake alikamatwa siku ya sikukuu mosi akipeleka ng’ombe wake malishoni na akiwa na pesa shilingi elfu 80 ambazo shilingi elfu 30 alichangiwa na baba yake. Pesa hizo alikusudia kwenda kununua godoro baada ya kumaliza kufunga ng’ombe wake. Baba mtu alipomuona mtoto wake nje ameshikwa na polisi wasiopungua 20 alikwenda kusikiliza kumezidi nini? La haula baba mtu alipigwa na kutakiwa aondoke mara moja. Baba mtu baada ya kushuhudia mtoto wake akipata kipigo hakua na cha kufanya aliondoka na kumwacha mtoto wake mikononi mwa askari hao. Baada ya kufika jioni na kuona mtoto wake hajarejea, baba mtu alikwenda kituo cha polisi Mwanakwerekwe kumtafuta mtot wake lakini alimkosa ndipo alipokwenda kito kikuu cha polisi Madema na kumkosa pia. Ndipo baadae akapokea simu kuwa mtoto wake ameshafariki na yupo chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mnazi mmoja na kumkuta akiwa katika hali kama hiyo.

Zanzibar

Bwana Yesu, angalia damu isiyo na hatia imemwagwa. Laana ya polio iwakute wote waliohusika na vizazi vyao na wote walioshabikia na wote watakaoshindwa kisimamia HAKI. YESU uliye wa wote fanya Bwana.
 
Mbona jeshi la polisi linapoua linakaa kimyaa, lakini alipouawa kamanda wao waliapa kuwa aliyefanya hivyo lazima apatikane na achukuliwe hatua. Ina maana damu ya huyo kamanda ndo yenye thamani kuliko ya watu wengine? Yana mwisho!
 
Hii ndiyo Tanzania. Je kamanda wa polisi waache kuuawa? Polisi waache kuuawa? Tumefika mahali viongozi wa nchi hii wapunguze safari na kutafakari upya tunakoelekea. Mungu uturehemu!
 
this is really bad. rip. haya manumba nenda na huko kaweke kambi uchunguze km kule mwanza majuzi.
 
ninaichukia Tanzania ya sasa ninawachukia watanzania ikiwa ni pamoja na mimi kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa uonevu kama huu dhidi ya wananchi unaofanywa na watu wanaotumia kaodi zetu kutuangamiza, eeeee mwenyezi mungu nionyeshe Tanzania ijayo yenye unafuu kuliko huu udhalimu wa sasa
 
Kuna source zingine zinasema kwamba marehemu kauawa na wananchi wenye hasira baada ya kukwapua simu,na polisi walienda kuchukua maiti yake na kuwa baba mtualisharidhika na maelezo ya polisi na kuwa tayari kuchukua maiti yake kwa kujua marehemu alikuwa ni mtundu lililotokea lawezekana kuwa kweli, daktari alimfanyia uchunguzi na kuthibitisha kuwa aliuwawa kuchomwa na vitu/kitu chenye ncha kali si vipigo.
Sasa wajomba zake na ami zake hawakuridhika na maelezo ya polisi nawakaomba ufanyike uchunguzi tena ikabidi apasuliwe kila sehemu kama umwonavyo pichani ili kuondoa utata(post mortem).
Baada ya hapo wakapewa maiti wakazike ndipo wakaitwa waandishi wa habari !
sipingi kama polisi hawawezi kufanya hivyo ila ninachokielezea pia kinazungumzwa mitaani na kuna watu wanatakakuliunganisha suala hili na opereheni za kijeshi zinazoendelea sasa hapa vsiwani japokuwa nakiri zinahitilafu nyingi tu..
Sikiliza hapa AUDIO | DW.DE
 
CCM wanawatumia vibaya polisi kwa maslahi yao, polisi nao wanatumia mwanya huo kutekeleza mauaji yasiyokuwa na msingi wowote!
so sad! so bad! I can't imagine!
 
Jamani! Kwani alikuwa na kosa gani? Labda siku polisi watakapoua mtoto wa kigogo ndio hatua zitachukuliwa.
 
Back
Top Bottom