Kijana Ally Salum na wana CCM wengine wanavyovuruga mambo kwenye jamii kumbe wameandaliwa!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Kijana Ally Salum ameteuliwa na rais Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Kwakweli nimeshangazwa sana na uteuzi huu.

Kijana Ally Salum huwa ana sifa moja kuu na kamwe hawezi kuiacha hata lishuke jua! Sifa ya usaliti.

Sifa hii iliwahi kumfanya kuwa ndumilakuwili wa hali ya juu sana pale UDSM.

Nakumbuka katika migomo kama miwili hivi ya kupinga kuchangia ada ya elimu ya juu na ule wa kudai nyongeza ya hela ya kujikimu (boom) Kijana huyu alikuwa na ndimi mbili za ajabu! Kwanza ule mgomo wa kwanza aliwasaliti wanafunzi kwa kuambiwa na utawala wa chuo aanzishe mgomo mwingine nje ya ule mkubwa ili baadaye aingie chimbo na mgomo uwe umeisha! Kijana akavuta akaja kwa wanafunzi akaanzisha kamgomo kake hakufanikiwa na baadaye ikabidi arudi kujiunga na mgomo wa wenzake.

Cha ajabu mgomo wa pili wa kudai nyongeza ya hela ya kujikimu aliingia tena kwenye jambo lilelile na kuteka adhima kuu ya ujumbe wa mgomo akaanzisha mgomo mwingine tofauti kabisa hapa sijui napo alitumwa na nani? Sisi tunafanya mgomo wa kudai nyongeza yeye ananitosha mgomo wa kumng'oa spika wa bunge la chuo! Yan usalitiusaliti tu!

Ajabu ya hawa vijana wanaoitwa na TISS-CCM huko mashuleni wengi wao walipata kufeli jumla lakini mnakuja kukutana mbeleni kwenye muda uleule na hapo unabaki kushangaa tu! Huyu kijana kulikuwa na ishu kuwa hakuwahi kusoma History o-level ila akaja kuisoma Advance hapo unajiuliza inakuwaje? Pia yupo mmoja naye ni kigogo fulani hivi serikali hii hii ya Magufuli, yeye aliwahi kupata zero form six tena masomo ya PCM kwenye shule moja ya serikali ila baadaye tulikuja kukutana pale UDSM mwaka uleule! Huyu naye alikuwa bingwa wa kupindisha malengo ya wanafunzi kwenye migomo na kila jambo yupo kwenye front line! Wakishaingia wanabadili dhumuni la mgomo then baada ya muda mnajikuta kufeli kama mtamsikiliza!

Hawa ndo type ya kina Makonda na wengine! Kwenye hii nchi wana full maigizo.
 
hujakosea mtoa post, uteuzi wa pole pole umefunika watu kumtambua hapi lakini huyu dogo hapi sio kabisa maisha yake pale UDSM yalikuwa ni ya kusaliti watu kweli kweli huku akijipambanua kama mtetezi, aliwahi kuwa mbunge kutoka facult of law na nadhani kina Julius Mtatiro, Silinde David, Joshua Nassari, Steven Owawa wanamtambua vyema namna alivyomsaliti mpambanaji Odong kutoka uganda ila ni suala la muda tu coz ndo siasa za Tz hizi.
 
Kijana Ally Salum ameteuliwa na rais Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Kwakweli nimeshangazwa sana na uteuzi huu.

Kijana Ally Salum huwa ana sifa moja kuu na kamwe hawezi kuiacha hata lishuke jua! Sifa ya usaliti.

Sifa hii iliwahi kumfanya kuwa ndumilakuwili wa hali ya juu sana pale UDSM.

Nakumbuka katika migomo kama miwili hivi ya kupinga kuchangia ada ya elimu ya juu na ule wa kudai nyongeza ya hela ya kujikimu (boom) Kijana huyu alikuwa na ndimi mbili za ajabu! Kwanza ule mgomo wa kwanza aliwasaliti wanafunzi kwa kuambiwa na utawala wa chuo aanzishe mgomo mwingine nje ya ule mkubwa ili baadaye aingie chimbo na mgomo uwe umeisha! Kijana akavuta akaja kwa wanafunzi akaanzisha kamgomo kake hakufanikiwa na baadaye ikabidi arudi kujiunga na mgomo wa wenzake.

Cha ajabu mgomo wa pili wa kudai nyongeza ya hela ya kujikimu aliingia tena kwenye jambo lilelile na kuteka adhima kuu ya ujumbe wa mgomo akaanzisha mgomo mwingine tofauti kabisa hapa sijui napo alitumwa na nani? Sisi tunafanya mgomo wa kudai nyongeza yeye ananitosha mgomo wa kumng'oa spika wa bunge la chuo! Yan usalitiusaliti tu!

Ajabu ya hawa vijana wanaoitwa na TISS-CCM huko mashuleni wengi wao walipata kufeli jumla lakini mnakuja kukutana mbeleni kwenye muda uleule na hapo unabaki kushangaa tu! Huyu kijana kulikuwa na ishu kuwa hakuwahi kusoma History o-level ila akaja kuisoma Advance hapo unajiuliza inakuwaje? Pia yupo mmoja naye ni kigogo fulani hivi serikali hii hii ya Magufuli, yeye aliwahi kupata zero form six tena masomo ya PCM kwenye shule moja ya serikali ila baadaye tulikuja kukutana pale UDSM mwaka uleule! Huyu naye alikuwa bingwa wa kupindisha malengo ya wanafunzi kwenye migomo na kila jambo yupo kwenye front line! Wakishaingia wanabadili dhumuni la mgomo then baada ya muda mnajikuta kufeli kama mtamsikiliza!

Hawa ndo type ya kina Makonda na wengine! Kwenye hii nchi wana full maigizo.
Katika filamu endelevu (series), huwa kuna season na ndani yake kuna episode, sasa hapa tupo season one lakini sejui ni episode IPI.

Sent from my XT1080 using JamiiForums mobile app
 
Kwani ulikuwa hujui siasa za ccm, hata wao kwa wao huwa wanasalitiana sana, wapo kimaslahi zaidi
 
Usihofu mkuu, nafasi bado zipo wewe piga mzigo uonekane! Mwenzio Humfrey Polepole alitoa rasimu inayopendekeza ma DC na maRC wasiwepo tena akaahidi kuisimamia na tukamuunga mkono! Ajabu leo anaenda kuapa kwa Mulongo kuutetea na kuulinda uDC! Hivyo nyie ni wavurugaji tu na tunawapuuza kwa nguvu zote!!
 
Ukawa acheni chuki jama,hamchoki tu,mlianza kwa mwigulu,mmesakama wee,akatusua,
mkaja kwa nape,akawini,mkaja kwa Lemutuz nae sasa anaelekea kuwa mmiliki wa redio,mkaja kwa makonda amewini,mkaja kwa polepole kawini,
kila mnaemsakama anawini,hata hamjiuliza Mungu anajaribu kuwapa message,hamtaki kuelewa,
acheni siasa za kinyongo,hizi siasa za kihasama zinachangia watu kuwaogopa,hawawezi kuwapa kura,mtaishia kuambulia kura za masela tu miaka nenda rudi
 
Polepole alisema sifa ya mwanaume akienda chumbani hageuki nyuma. Akidai EL alikua kigeugeu kuhusu serikali 2 ama 3. Ila yeye ana msimamo. Hayumbi.
This time karma is taking him.
Kwenye udisii.
 
Hilo la History O level ni sahihi alisoma shule GA mchepuo wa ufundi O level ambayo ni Bwiru boys huko nako Ali engineer Mgomo mkubwa sana akiwa ni HP. Shule za ufundi huwa hazina history kwa hiyo history aliikuta mbeleni
 
Alikuwa anajitahidi atambulike kama "mtetezi wa wanyonge" na hapo hapo mtetezi wa maslahi ya nchi. amefanikiwa maana alijua kuna upande mmoja utamlipa hakuweka mayai yote kwenye kikapu kimoja. Ndivyo walivyo viongozi wetu wengi wapo kwa ajili ya maslahi yao.
 
Back
Top Bottom