Kijana akamatwa na kichwa cha mtoto akifyonza damu:::

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
Kijana akamatwa na kichwa cha mtoto akifyonza damu

2008-04-27 11:34:32
Na Karama Kenyunko


Ramadhani Musa (1 anayedaiwa kuingia Dar es Salaam juzi akitokea Mtwara, amenaswa akiwa na kichwa cha mtoto mdogo. Mtuhumiwa alikamatwa na walinzi wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam jana asubuhi akijaribu kukipitisha kwa staili.

Akiwa na kifurushi aliwahadaa walinzi kuwa anakwenda kumuona shangazi yake, hata hivyo walimshtukia baada ya kuona damu zimetapakaa mdomoni.

Walipokagua kifurushi walikuta kichwa cha mtoto wa kike aliyekuwa amesukwa mtindo wa `twende kilioni` kikichuruizika damu.

``Kijana huyo alikichukua mbele ya walinzi hao na kuanza kufyonza damu na kujilamba midomo, `` alidai mlinzi na kuongeza kuwa aliwauliza kwa ujasiri mnashangaa nini? ``Kwetu ni kitu cha kawaida kula nyama za watu.``

Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala wa Bw. Charles Chambo, alithibitisha kutokea kwa mkasa huo na kueleza kuwa kichwa hicho ni cha Salome Yohana (3).

Kwa mujibu wa mama Salome, Bi. Pendo Dutsan, binti yake alitoweka juzi usiku nyumbani kwa shangazi yake anayeishi Segerea na kwamba kabla ya kuishia alikuwa akicheza nje ya nyumba yao.

Waligundua kuwa hayupo wakati wa chakula cha jioni na kuanza kumtafuta lakini bila ya mafanikio hadi jana asubuhi, mgeni wa jirani yao aliyetajwa kwa jina la Lucas Kibaya, alipogundua kiwiliwili chake chooni.

Alidai Kibaya aliingia chooni na kukuta tofali limefunika tundu na alipoliondoa aliona kanga iliyokuwa na damu na kugundua kiwiliwili cha mtoto kilichonasa kwenye tundu hilo.

Baada ya kutoa taarifa, polisi wa kituo cha Stakishari Ukonga walifika na kuopoa kiwiliwili hicho na kutafuta gari ili kunyonya uchafu ili kutafuta kichwa ambacho kilikuwa hakionekani.

``Wakati tunaendelea kukisaka kichwa polisi walitueleza kuwa walipokea taarifa za kukamatwa kwa Musa akiwa na kichwa Muhimbili,`` alisema mwanamke huyo akilia kwa uchungu.

Aliongeza kuwa polisi walikichukua kiwiliwili pamoja kuwakamata watuhumiwa ambapo mwili huo ulikuwa chooni kwao hadi kituo cha Stakishari.

Baada ya taarifa za kupatikana kichwa hicho, watuhumiwa ambao kiwiliwili kilikuwa nyumbani kwao walipelekwa Muhimbili hospitali walikoonyeshwa kichwa pamoja na `miliki.`

Watuhumiwa hao Kibaya na mkewe Hadija Ali walimtambua kijana wao na kueleza kuwa alikuja Dar es Salaam Ijumaa, siku moja kabla ya tukio, akitokea Mtwara.

Hadija alidai walitengana na mzazi mwenzake (baba wa mtoto huyo) kwa miaka mingi na muda wote alikuwa akiishi Mtwara.

Alisema Ramadhan alitoweka juzi jioni na alipigwa na butwaa baada ya kuona kuwa aliyekamatwa na kichwa cha Salome ni mwanae.

Mhudumu wa chumba cha maiti Muhimbili Bw. Mizome Gogo, alisema kichwa hicho kilifikishwa jana asubuhi na polisi na muda mfupi baadaye askari wa Stakishari waliwaletea kiwiliwili.

SOURCE: Nipashe
 
watu kama hawa wanafaa kufanyiwa summary execution pale mnazi mmoja and their families invoiced for the bullet. hawa na wale wanao uwa albinos for the sake of uchawi.. Wawe SHOT dead.mchana wa jua kali. they are worse than animals.
 
Maafa haya ni matokeo ya Polisi na hospitali ya Muhimbili kutotekeleza wajibu wao ipasavyo.

Huyu kijana alipelekwa pale na Mch. Lwakatare baada ya kudai kuanguka kwenye ungo! Bila ya uchunguzi wa kutosha wakamwachia. Haijapita muda kaua mtoto wa miaka 3. Shame on u!!
 
Laiti Serikali Ingemsikiliza Mtumishi Wa Mungu Mch.g. Lwakatare!!!!!!!!!.

Badala Yake Mkamfanya Aonekane Muongo Na Mnafiki Mbele Za Watu. Mungu Amekudhirisha Kwa Walimwengu Mama. Endelea Na Kazi Ya Kuponya Roho. Maneno Yako Yangeweza Kuokoa Maisha Ya Mtoto Asiyekuwa Na Hatia Malaika Wa Mungu.
Praise Be To The Lorld. Amen!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom