Mocumentary
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 769
- 1,959
Mahakama ya wilaya ya Kigoma imemuhukumu kwendajela miaka 20 mkazi wa Kijiji cha kidawe, Nuhu Edward mwenye umri wa miaka 28 kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi la kukutwa na vipande vitano vya meno ya tembovyenye thamani ya shilingi milioni 68,000,220 pamoja nakujihusisha na biashara ya meno ya tembo bila kibali.
Hakimu Eva Mushi, akisoma maelezo ya mwenendo mzima wa kesi namba 05 ya mwaka 2019 kabla yakutoa hukumu amesema upande wa jamuhuri ukiwa na mashahidi nane waliowasilishwa mahakamani hapo waliiambia mahakama kuwa walipokea taarifa kutoka kwa msiri wao kuwa kuna mtu anajihusisha na biashara hiyo na kuandaa mtego kwa mmoja wa maafisa wa Wanyama pori kujifanya mteja wa meno hayo kisha kufanikiwa kumnasa majira ya saa saba kuelekea saa nane usiku tarehe 25 /05/2019 mshtakiwa akiwa na vidhibiti.
Chanzo: Global tv