Kijana ahukumiwa miaka 20 jela, ajitetea mahakamani - "mimi ni yatima, nipunguzieni adhabu"

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
765
1,954
Mahakama ya wilaya ya Kigoma imemuhukumu kwendajela miaka 20 mkazi wa Kijiji cha kidawe, Nuhu Edward mwenye umri wa miaka 28 kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi la kukutwa na vipande vitano vya meno ya tembovyenye thamani ya shilingi milioni 68,000,220 pamoja nakujihusisha na biashara ya meno ya tembo bila kibali.

Hakimu Eva Mushi, akisoma maelezo ya mwenendo mzima wa kesi namba 05 ya mwaka 2019 kabla yakutoa hukumu amesema upande wa jamuhuri ukiwa na mashahidi nane waliowasilishwa mahakamani hapo waliiambia mahakama kuwa walipokea taarifa kutoka kwa msiri wao kuwa kuna mtu anajihusisha na biashara hiyo na kuandaa mtego kwa mmoja wa maafisa wa Wanyama pori kujifanya mteja wa meno hayo kisha kufanikiwa kumnasa majira ya saa saba kuelekea saa nane usiku tarehe 25 /05/2019 mshtakiwa akiwa na vidhibiti.

Chanzo: Global tv

Maisha tokea 2015 - 2020 yamezidi kuwa magumu kwa raia wote, hasa kwa vijana wasio na elimu. Ndio kinachopelekea vijana wengi kujiingiza katika biashara haramu.
 
Vipande 20 vya meno ya tembo miaka 20 jela adhabu kubwa Sana kuliko kosa lenyewe ...

Angekuwa na hela angeambiwa aongee na DPP...

tunaozidi kujaa jela ni sisi maskini.

Deo Mwanyika aliekuwa anashirikiana na mabeberu kuhujumu nchi leo anagombea ubunge pamoja na kukutwa na kosa la uhujumu uchumi.

Huu utawala una upendeleo sana kwa wenye pesa.
 
Kina deo mwanyika wanaenda bungeni huku wameshirikiana na wazungu kuiba rasilimali za taifa.. vijana maskini wanaenda jela
 
Ukute huyu alikuwa kibarua tu, mabosi wanaendeleza show kama kawaida.
Yule mbunge Mwarabu wa kule kanda ya ziwa alikamatwa na Nyara za serikali+Silaha za kuwindia za kutosha kamalizana na DPP chap chap,mdogo wake rostam walimkuta na silaha za kutosha za kuwindia hazina hata vibali akamalizana na DPP kwa mil 200 huko yuko zake kitaa.

Vifungo ni kwa ajili ya maskini
 
Huyu dalali tu anawawakilisha madon bila kujua madhara na utetezi wake wa kindezi.Nilichopenda amestick na code ya NO SNITCHING.
 
Ukiwa sio kada wa CCM kama wale mdogo ake Rostam na yule mbubge wa Kishapu ile option ya kuonana na DPP hata upewi kweli CCM inatakiwa iondoke kabisa
 
Wamemuonea
Ninyi mnaojilimbikizia mali kwa pesa za walipa kodi mnadunda
Mtoto wetu Yatima Mungu atakutetea
Ni swala la muda.....
 
Yule mbunge Mwarabu wa kule kanda ya ziwa alikamatwa na Nyara za serikali+Silaha za kuwindia za kutosha kamalizana na DPP chap chap,mdogo wake rostam walimkuta na silaha za kutosha za kuwindia hazina hata vibali akamalizana na DPP kwa mil 200 huko yuko zake kitaa.

Vifungo ni kwa ajili ya maskini
Hii adhabu haiwahusu waarabu au wageni. Halafu tunaambiwa Lissu anatumiwa na mabeberu.
Mnakumbuka yule beberu wa Vodacom aliyeelewana na mamlaka husika ndani ya siku chache akaachiwa aende kula nchi.
 
Tatizo huyu atakuwa ni ACT-Wazalendo,serikali haijataka mambo mengi,sijui aongee na Dpp,au alipe la hasha!
Mvua 20 chap.
 
Mahakama ya wilaya ya Kigoma imemuhukumu kwendajela miaka 20 mkazi wa Kijiji cha kidawe, Nuhu Edward mwenye umri wa miaka 28 kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi la kukutwa na vipande vitano vya meno ya tembovyenye thamani ya shilingi milioni 68,000,220 pamoja nakujihusisha na biashara ya meno ya tembo bila kibali.

Hakimu Eva Mushi, akisoma maelezo ya mwenendo mzima wa kesi namba 05 ya mwaka 2019 kabla yakutoa hukumu amesema upande wa jamuhuri ukiwa na mashahidi nane waliowasilishwa mahakamani hapo waliiambia mahakama kuwa walipokea taarifa kutoka kwa msiri wao kuwa kuna mtu anajihusisha na biashara hiyo na kuandaa mtego kwa mmoja wa maafisa wa Wanyama pori kujifanya mteja wa meno hayo kisha kufanikiwa kumnasa majira ya saa saba kuelekea saa nane usiku tarehe 25 /05/2019 mshtakiwa akiwa na vidhibiti.

Chanzo: Global tv

Ila WaChina wanaojihusisha na biashara hii wanakatiwa na diplomatic passport kabisa ili wachote meno ya tembo bila bughudha
 
Back
Top Bottom