Kiingereza kinachoandikwa kwenye blogs za Kitanzania

Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,486
3,472
Kama kuna kitu kinachonikera kwenye blogs zetu ambazo huandikwa[kutafsiriwa kwa kiingereza] ni ni oborongaji wa lugha hiyo kiasi hata nikisoma mimi ambaye ni mtanzania sielewi na mara nyingi hujiuliza 'kwa nini wenye blogs hizi hawatafuti watu ambao wanaifahamu vizuri lugha hiyo? Nionavyo ni bora waandike kwa kiswahili tu kuliko aibu ambayo uandikwa kwenye blogs hizo.
 
Hiyo ni kweli mdau na hizi blog sinasomwa na watu wengi tu, lakini mm naona kuna tatizo moja; mtanzania ukimwambia ajui kingereza na yy amesoma form 4 au 6 hata chuo, anakuwa ataki kuwambiwa kitu anaona kama anapondwa au unamponda. Mawazio yako uliyosema ni mazuri sana, kwani unaona watu au wana blog wa nchi nyingi tu wanatafu mtu hili aweze kurekebisha lugha mbali mbali sio lazima kingereza tu, kwa mfano nina mjua mtu ana andika blog ya kifaransa na yy ni anatoka Haiti lakini anaona kwamba hana ufasaa ktk lugha hiyo kwa hivyo anatafuta mtu kuangalia makosa mbali mbali kabla ya kupablish.
 
Duuu kweli
Mimi nina mfano ambao hupo nyumbani kwangu, mke wangu kamaliza form 4 amekuja hapa UK miaka 6 iliyopita ss na mm nina miaka 20 hapa ss na sio nasema kwamba ninaju lugha ya kingereza kwa ufasaha apana, lakini ukimwambia umekosea hapo weeeeeeeeeeeee, hatari kwa hivyo wabongo ndo matatizo yetu. kwa hivyo mbongo unamwacha anachapia hivyo hivyo mradi mnakwenda. ahaaaaa.
 
Inaonekana na wewe hujui kiswahili. Mfano tunasema hataki siyo ataki. Na kwa kingereza tuna publish.
 
Mimi nina mfano ambao hupo nyumbani kwangu, mke wangu kamaliza form 4 amekuja hapa UK miaka 6 iliyopita ss na mm nina miaka 20 hapa ss na sio nasema kwamba ninaju lugha ya kingereza kwa ufasaha apana, lakini ukimwambia umekosea hapo weeeeeeeeeeeee, hatari kwa hivyo wabongo ndo matatizo yetu. kwa hivyo mbongo unamwacha anachapia hivyo hivyo mradi mnakwenda. ahaaaaa.

Kwahiyo mkuu hapo UK wewe unajua Kizungu au Kiswahili? Manaake naona katika lugha ulizoandika kuna makosa kibao.

UK=ukonga???
 
Back
Top Bottom