Kiingereza cha Kimarekani chamkanganya Ruto

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,387
7,371
Bora tu imetokea kwa Mkenya! Ingelikuwa ni Mtanzania angekiona cha moto kwa mashambulizi ambayo angeyapata mitandaoni😄😄😄

Kiingereza si tatizo kwa wasomi wa Kenya, Rais Ruto akiwemo. Lakini awamu hii kakutana na Mkenya aliyeizoea American accent. Alipoona hamwelewi, alimwuliza kama anaweza akaongea kwa Kiswahili.

Yaani Kiswahili kilionekana chepesi kukielewa kuliko Kiingereza cha huyo mwanamke.

Hii iwatie moyo wale wote wasiojiamini katika hii lugha! Ukishindwa kuielewa, usione haya kuuliza hata kama utachekwa. Lakini pia usiache kuendelea kujifunza.

Mimi mwenyewe ukiongea kiswahili cha kizanzibari sitokuelewa.

Ukiongea kile kiswahili cha kamusi ya bakita sitokuelewa.

Nina rafiki yangu muingereza anaishi marekani anasema yeye mwenyewe kunawakati hawaelewani kimazungumzo!

Kutokujua kiingereza sio ajabu sana maana ni lugha ina lahaja zake, ina rejesta zake, n.k

Mh. Ruto yupo sahihi sana na anajiamini.

Hapa kwetu ukionekana hujui basi ni nogwa
 
Wengi wameuingia mtego wa Rais Luto na video imeenda viral,so Lengo limefanikiwa.

Kiukweli Alikuwa anamwelewa vizuri tu,ila Luto ni mjanja na smart sana.

Kaona akipromote kiswahili hasa ukizingatia huko mambele kiswahili kinaonekana kama lugha wakenya na si Tanzania.

Kwa haraka unaweza kuingia huo mtego wa "Rais Luto hajui kingereza cha kimarekani"

Hapo hakuna cha lahaja Wala accent, alikuwa anamwelewa vizuri tu. Ila akamtoa kwenye reli kwa kumtaka aongee kiswahili,Huku akijifanya haelewi hiyo slang.
 
Lahaja ya kiingerza cha marekani ni ya kipekee sana, hasa mtu unaeongea nae akiwa umbali kidogo na ulipo, afadhalli awe sambamba au jirani sana na wewe unaweza elewa, kuliko kama umbali wa ile conversation ya Ruto kutumia mic alokua anafanya Ruto na yule mbantu muwekezaji kule kenya 🐒
Mimi kanitia moyo!

Kuna mwaka nilipata wageni kazini wanaoongea hiyo lahaja. Wakati wa mazungumzo, kuna mmoja aliniuliza kitu kumbe mimi sikumwelewa, nikajikuta natoa majibu ambayo siyo waliyoyahitaji. Bahati nzuri nilikuwa na mtu ambaye ameshaishi huko kwa miaka mingi, kwa hiyo alipoona nimeenda chaka, aliniambia sicho ulichoulizwa.

Nilijisikia vibaya sana siku hiyo. Lakini kumbe sikupaswa kujihukumi kwa kihivyo!

Kama imemshinda Mwalimu wa Chuo Kikuu cha nchini Kenya, kuna uajabu gani kwa mimi kuteleza kidogo?
 
Kamaa

Ikiwa kazi zako zinahitaji ujue kiingereza basi endelea kujifunza Sana.
 
Back
Top Bottom