Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,072
Tunamshukuru Dkt. Hamis Kingwangalla kwa kutoa maoni yake akikiri ukweli kuhusu Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji kuwa ni mwanasiasa mzuri, msomi mzuri na msemaji mzuri.
Hapo hapo kwa makusudi ya kutumwa au kujituma mwenyewe, katika maoni yake hayo ambayo ameandika na kuyasambaza mitandaoni, Kingwangalla amefanya upotoshaji kwa nia anayoijua yeye.
Kingwangalla ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amedai kuwa Katibu Mkuu Mashinji hakuwahi kuwaokoa yeye na watu wengine walioshiriki mgomo wa madaktari mwaka 2005 wala hakuwahi kuongoza mgomo huo, lakini hapo hapo anajikanganya kwa kukiri kuwa Katibu Mkuu ALISHIRIKI mgomo huo huo.
Ili asilazimike kujikanganya kwa sababu tu ametumwa au amejituma kupotosha, Kingwangalla awaambie Watanzania ni akina nani waliowaokoa interns (akiwemo yeye Kingwangalla) waliogoma mwaka huo mwezi Februari?
Kumbukumbu zinaonesha kuwa baada ya interns hao kugoma ilikuwa imeamriwa wafukuzwe na wanyang’anywe leseni, hivyo seniors wao kama akina Erasto Ngonyani, Dkt. Mashinji na wengine, nao wakaamua kugoma ili kuwaokoa interns wasifukuzwe.
Kingwangalla kwa namna ile ile ya kujituma au kutumwa kupotosha, ameandika kuwa Katibu Mkuu Dkt. Mashinji alinyanyaswa na supervisor wake (ambaye hamtaji jina, Prof. Mwafongo).
Kama Naibu Waziri haujui ukweli kuhusu Dkt. Mashinji na supervisor wake, asikimbilie kuandika kitu asichokijua na kujishushia hadhi.
Tumsaidie. Wala asiende mbali. Amtafute Katibu Mkuu wa Wizara yake, atamsaidia kupata ukweli ili siku nyingine aandike kwa usahihi. Kama hataweza kumfuata Katibu Mkuu wa Wizara yake, basi tunamsaidia kumwambia kuwa taarifa zinaonesha wawili hao (mwanafunzi na msimamizi wake) ni watu wenye mahusiano mazuri wala hakukuwahi kuwa na tukio kama alivyopotosha Kigwangalla.
Kuhusu msimamo usiotetereka, Kingwangalla kajikanganya zaidi. Siku nyingine akiamua kujituma au akikubali kutumwa kupotosha mambo ni vyema afikirie mara mbili au awe na kumbukumbu sahihi.
Madaktari waliogoma mwaka 2005 pamoja na masuala mengine, walitaka upatikanaji wa vifaa hospitalini na maslahi ya madaktari. Mambo ambayo hadi leo miaka 11 baadae bado ni kilio kikubwa katika sekta hiyo nyeti kwa maendeleo ya jamii.
Anasema eti walimtenga na kumwepuka kumwalika katika vikao vya CC ya migomo. Vyema. Kwa ujasiri huo anaojivika wa kusema anayotaka kuwaaminisha watu kuwa ni kweli, Je Kigwangalla yuko tayari kuwaambia Watanzania, ni nani aliyekwenda kumbembeleza na kumpigia magoti Waziri Mkuu Fredrick Sumaye, aki-surrender?
Kama atashindwa, basi asiogope pale atakaposaidiwa kwa kupewa picha ili amuone huyo mtu akiwa amepiga magoti ya kujisalimisha.
Kigwangalla leo yuko anafanya kazi ndani ya Serikali ya CCM ambayo mwaka 2005 aliigomea kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake, Dkt. Mashinji bado yuko upande wa mabadiliko akiendeleza kudai haki hizo na nyingine kwa ajili ya wananchi.
Hadi hapo nani mwenye msimamo, kuyumba au kutetereka, Dkt. Mashinji au Kigwangalla? Ni Dkt. Mashinji au yule aliyekwenda kupiga magoti?
Tumshauri tena Kigwangalla, kama daktari wa binadamu kwa taaluma aheshimu taaluma yake. Pia ajikite katika majukumu aliyopewa. Bado kuna ‘vilio vingi’ katika wizara yake, ambavyo haviwezi kumalizwa kwa staili ya kutumbua majipu bali uongozi wenye dira na maono (MABADILIKO). Lakini pia aheshimu kaka na dada zake waliomtangulia katika taaluma hiyo, ambalo ni jambo zuri tu.
Makene