barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,819
Nimeipokea kwa namna "tofauti" taarifa ya kijana wangu Waziri Kigwangala juu ya kampuni za uwindaji zinazojihusisha na ujangili katika hifadhi na mapori yetu.Taarifa hii ni "nzuri" kwa upande mmoja kwa sababu Mh.Kigwangala amefanyia kazi yale mambo ambayo tuliyaleta hapahapa Jf(mimi barafu nikiwa mmoja wao) kuhusu wahusika wa ujangili na namna wanavyofanya kazi hiyo ya kufisidi wanyama wetu.
Baada ya Kigwangala kuingia katika wizara hiyo,nilimuandika "thread" hapa Jf ili aanze na majangili wa RUAHA NATIONAL PARK.Na hakika,katika watu au kampuni zilizotajwa,kampuni "sugu" ya ujangili katika eneo la Ruaha imetambulika,baada ya Kigwangala kuunda "Task Force" na kwenda kufanya uchunguzi katika vijiji na eneo la watu walio kando ya mbuga ya Ruaha.Uzi huo huko hapa Mh. Kigwangalla, karibu Maliasili na Utalii. Anza na hawa majangili wa Ruaha National Park
Kampuni nyingine iliyotajwa,inayomuhusisha kada na MNEC wa zamani wa CCM mkoa wa Kigoma,ilijadiliwa kwa mapana sana hapa JF,kabla hata Kigwangala hajawa Waziri wa Wizara husika.
Mjadala ule ulijadiliwa kwa kina sana na hakika watu wengi walitoa michango na mawazo yao na kuidokeza serikali mahali pa kuanzia juu ya hizi kampuni za "kihuni" zinazopukutisha mali-asili zetu kwa jina la utalii.Mtajwa na kampuni yake na mienendo yake juu ya shutma za ujangiri,zilijadiliwa kwenye uzi huu Hii ndege(5H-ZAI) ni ya nani na hufanya nini kwenye mbuga ya Selous?
Kampuni ya tatu iliyotajwa na Kigwangala,inamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF),hii ni kampuni ya kimarekani ambayo ina kampuni tanzu za uwindaji za Mwiba Holdings Tz Ltd,Tanzania Game Trackers Safaris Ltd na Wengerl Windrose Safaris Ltd.Kampuni hizi zote tatu zimetajwa na Mh.Kigwangala.Mjadala juu ya hawa FCF na ushiriki wao katika ujangili ulijadiliwa sana hapa JF kupitia uzi huu Nyalandu ahusishwa na Kampuni Inayotuhumiwa Kwa Ujangili
Sina shaka na tuhuma hizi za Mh.Kigwangala,na kila mtu aliye katika sekta ya utalii,anafahamu "tetesi" za ushiriki wa kampuni hizi katika masuala ya ujangili.
Kinachostua wengi,ni kwanini Mh.Kigwangala ameamua kutaja kampuni hizi tu katika tuhuma za ujangili?Je ni kweli hakuna kampuni nyingine "papa" zinazohujumu maliasili zetu huko porini zaidi ya hizi mbili?
Jf ikiwa ni sehemu ya mijadala huru na uchambuzi usio na mawaa,tunaweza kuanza kuangalia dhamira ya Mh.Kigwangala,ni kweli amekazana kabisa kuwamaliza hawa majangili?Maana kwa kinywa chake alituambia kufikia Januari 2018,kampuni ya OBC iwe imefunga virago na kuondoka,lakini mpaka sasa OBC wapo wanakula tu maisha kule Loliondo.Au ama ameanza na majangili tu ambao hawakuwa "upande wetu" wakati tunatafuta nafasi kielekea jumba jeupe?
FCF ambao wanamiliki hizo kampuni za uwindaji za Mwiba Holdings Ltd na nyenzake,ni kampuni ambazo zina "uhusiano" wa moja kwa moja na Lazaro Nyalandu,kampuni hizi zimekuwa kwa kasi wakati Nyalandu akiwa katika hiyo Wizara,chopa yao moja yenye rangi ya kijani ilitumiwa na Nyalandu katika kampeni za kuusaka Urais na baadaye Ubunge mwaka 2015,hawa FCF "walimdhamini" Nyalandu katika sehemu ya kampeni zake.Unapoitaja Mwiba Holdings Ltd na ujangili,unamtaja Nyalandu kwa njia ya nyuma ya pazia.Inawezekana hapa hatafutwi Mwiba Holdings Ltd pekee,hapa anatafutwa na "mwenyeji" wao.Mh.Kigwangala atuambie OBC ya Katibu wake imefikia wapi?
Unapoitaja Mkwawa Hunting Safaris Tz Ltd.Hii Mkwawa inamilikiwa na wale jamaa wenye Mkwawa Drinking Water na Mkwawa Rally Team kule Iringa,Hawa ndio wanamiliki kampuni ya ndege ya "Jambo Aviation",waliamua kujenga kabisa kakiwanja kao ka ndege huko Ruaha Nationala Park eneo la Madogoro ili wasafirishe nyara kwa urahisi.Kampeni za 2015,ndege yao ndogo aina ya C208 usajili wa 5H-AMH ilitumika kumsafirisha huku na kule "jasusi mkubwa" aliyekuwa anaisaka Ikulu ya Magogoni.
Unapoitaja Iringa na Ujangili,huwezi kumaliza orodha bila kutaja Wabunge wawili,mmoja Waziri kwa sasa na mwingine wa Jimbo la Mpakani mwa Iringa na Mbeya aliyejadiliwa hapa Mbunge wa Mbarali atuhumiwa kufukia pembe za ndovu eneo lake la uwekezaji na uzi mwingine huu Mbeya: Mtoto wa Mulla ambaye ni jangili amuua mtu aliyemhisi kumchongea, ajeruhi wengine na mwenzake akajadiliwa hapa https://www.jamiiforums.com/threads/iringa-katibu-wa-mbunge-wa-jimbo-la-isimani-akamatwa-katika-oporesheni-ondoa-ujangili.544391/. Hawa hushirikiana na mtumishi mmoja wa kanisa eneo hilo kwa miaka mingi.Hawa kina "Mkwawa" hujificha nyuma ya nguvu za kisiasa za hawa Wabunge.
Game Frontiers of Tz Ltd,imetajwa sana sana kwa miaka mingi,kada,mfadhili na MNEC wa mkoa wa Kigoma.Kuanzia mapori ya Kipiri,Likuyu,Likawage,Mngeta hadi Tabora hakuna asiyefahamu.Habari zake zilijadiliwa sana hapa Hii ndege(5H-ZAI) ni ya nani na hufanya nini kwenye mbuga ya Selous?
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015,ndege za huyu jamaa zilitumiwa sana na kambi ya Mzee Eddo.Safari za Arusha-Dodoma,au Dodoma-Dsm kampuni ya ndege ya huyu jamaa ijulikanayo kama Zantas Air,ndege zake zilitumika sana.Tulijadili ushirika wa Zantas Air katika kufanikisha kampeni za Mzee wa Monduli kuelekea Ikulu kwenye uzi huu Apson Mwang'onda na Timu yake waelekea Arusha kuratibu Mkutano wa Lowassa
Tunapokuwa tunampongeza Mh.Kigwangala kuanza vita ya "Ujangili",tusiache kumuonya na kumpa tahadhari kuwa vita hivi,visiwe na shinikizo la chuki za kisiasa na uadui wa kiitikadi,bali viwe vita vya kweli vyenye lengo la kuutokomeza mtandao wote wa ujangili.Asiishie kutaja tu nyumba za "Mawaziri Wakuu Wastaafu" zilizojengwa ndani ya kiwanja mali ya Taasisi ya wizara yake,bali atekeleze na ahadi zake za kuiwajibisha kampuni ya OBC ambayo ndani yake tunajua mabosi wake ndani ya chama na serikali wana maslahi nayo.
Si haba,alipoanzia si pabaya,aende mbele zaidi.Kingwangala asiishie kuwataja "majangili" wenye "uhusiano" na maadui wake wa kisiasa na kiitikadi,awataje pia wabunge wa chama chake na viongozi wa chama chake ambao kuna kampuni zinazotuhumiwa kwa ujangili zina mahusiano nao.Akiifikia hatua hii,tutakuwa pamoja naye na kumpa ushirikiano mpaka mwisho wa dahari.