Kigwangalla, usiishie kutaja "majangili" wenye uhusiano na "mahasimu wako kisiasa", Taja na wale wa chama chako

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Nimeipokea kwa namna "tofauti" taarifa ya kijana wangu Waziri Kigwangala juu ya kampuni za uwindaji zinazojihusisha na ujangili katika hifadhi na mapori yetu.Taarifa hii ni "nzuri" kwa upande mmoja kwa sababu Mh.Kigwangala amefanyia kazi yale mambo ambayo tuliyaleta hapahapa Jf(mimi barafu nikiwa mmoja wao) kuhusu wahusika wa ujangili na namna wanavyofanya kazi hiyo ya kufisidi wanyama wetu.

Baada ya Kigwangala kuingia katika wizara hiyo,nilimuandika "thread" hapa Jf ili aanze na majangili wa RUAHA NATIONAL PARK.Na hakika,katika watu au kampuni zilizotajwa,kampuni "sugu" ya ujangili katika eneo la Ruaha imetambulika,baada ya Kigwangala kuunda "Task Force" na kwenda kufanya uchunguzi katika vijiji na eneo la watu walio kando ya mbuga ya Ruaha.Uzi huo huko hapa Mh. Kigwangalla, karibu Maliasili na Utalii. Anza na hawa majangili wa Ruaha National Park

Kampuni nyingine iliyotajwa,inayomuhusisha kada na MNEC wa zamani wa CCM mkoa wa Kigoma,ilijadiliwa kwa mapana sana hapa JF,kabla hata Kigwangala hajawa Waziri wa Wizara husika.

Mjadala ule ulijadiliwa kwa kina sana na hakika watu wengi walitoa michango na mawazo yao na kuidokeza serikali mahali pa kuanzia juu ya hizi kampuni za "kihuni" zinazopukutisha mali-asili zetu kwa jina la utalii.Mtajwa na kampuni yake na mienendo yake juu ya shutma za ujangiri,zilijadiliwa kwenye uzi huu Hii ndege(5H-ZAI) ni ya nani na hufanya nini kwenye mbuga ya Selous?

Kampuni ya tatu iliyotajwa na Kigwangala,inamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF),hii ni kampuni ya kimarekani ambayo ina kampuni tanzu za uwindaji za Mwiba Holdings Tz Ltd,Tanzania Game Trackers Safaris Ltd na Wengerl Windrose Safaris Ltd.Kampuni hizi zote tatu zimetajwa na Mh.Kigwangala.Mjadala juu ya hawa FCF na ushiriki wao katika ujangili ulijadiliwa sana hapa JF kupitia uzi huu Nyalandu ahusishwa na Kampuni Inayotuhumiwa Kwa Ujangili

Sina shaka na tuhuma hizi za Mh.Kigwangala,na kila mtu aliye katika sekta ya utalii,anafahamu "tetesi" za ushiriki wa kampuni hizi katika masuala ya ujangili.

Kinachostua wengi,ni kwanini Mh.Kigwangala ameamua kutaja kampuni hizi tu katika tuhuma za ujangili?Je ni kweli hakuna kampuni nyingine "papa" zinazohujumu maliasili zetu huko porini zaidi ya hizi mbili?

Jf ikiwa ni sehemu ya mijadala huru na uchambuzi usio na mawaa,tunaweza kuanza kuangalia dhamira ya Mh.Kigwangala,ni kweli amekazana kabisa kuwamaliza hawa majangili?Maana kwa kinywa chake alituambia kufikia Januari 2018,kampuni ya OBC iwe imefunga virago na kuondoka,lakini mpaka sasa OBC wapo wanakula tu maisha kule Loliondo.Au ama ameanza na majangili tu ambao hawakuwa "upande wetu" wakati tunatafuta nafasi kielekea jumba jeupe?

FCF ambao wanamiliki hizo kampuni za uwindaji za Mwiba Holdings Ltd na nyenzake,ni kampuni ambazo zina "uhusiano" wa moja kwa moja na Lazaro Nyalandu,kampuni hizi zimekuwa kwa kasi wakati Nyalandu akiwa katika hiyo Wizara,chopa yao moja yenye rangi ya kijani ilitumiwa na Nyalandu katika kampeni za kuusaka Urais na baadaye Ubunge mwaka 2015,hawa FCF "walimdhamini" Nyalandu katika sehemu ya kampeni zake.Unapoitaja Mwiba Holdings Ltd na ujangili,unamtaja Nyalandu kwa njia ya nyuma ya pazia.Inawezekana hapa hatafutwi Mwiba Holdings Ltd pekee,hapa anatafutwa na "mwenyeji" wao.Mh.Kigwangala atuambie OBC ya Katibu wake imefikia wapi?

Unapoitaja Mkwawa Hunting Safaris Tz Ltd.Hii Mkwawa inamilikiwa na wale jamaa wenye Mkwawa Drinking Water na Mkwawa Rally Team kule Iringa,Hawa ndio wanamiliki kampuni ya ndege ya "Jambo Aviation",waliamua kujenga kabisa kakiwanja kao ka ndege huko Ruaha Nationala Park eneo la Madogoro ili wasafirishe nyara kwa urahisi.Kampeni za 2015,ndege yao ndogo aina ya C208 usajili wa 5H-AMH ilitumika kumsafirisha huku na kule "jasusi mkubwa" aliyekuwa anaisaka Ikulu ya Magogoni.

Unapoitaja Iringa na Ujangili,huwezi kumaliza orodha bila kutaja Wabunge wawili,mmoja Waziri kwa sasa na mwingine wa Jimbo la Mpakani mwa Iringa na Mbeya aliyejadiliwa hapa Mbunge wa Mbarali atuhumiwa kufukia pembe za ndovu eneo lake la uwekezaji na uzi mwingine huu Mbeya: Mtoto wa Mulla ambaye ni jangili amuua mtu aliyemhisi kumchongea, ajeruhi wengine na mwenzake akajadiliwa hapa https://www.jamiiforums.com/threads/iringa-katibu-wa-mbunge-wa-jimbo-la-isimani-akamatwa-katika-oporesheni-ondoa-ujangili.544391/. Hawa hushirikiana na mtumishi mmoja wa kanisa eneo hilo kwa miaka mingi.Hawa kina "Mkwawa" hujificha nyuma ya nguvu za kisiasa za hawa Wabunge.

Game Frontiers of Tz Ltd,imetajwa sana sana kwa miaka mingi,kada,mfadhili na MNEC wa mkoa wa Kigoma.Kuanzia mapori ya Kipiri,Likuyu,Likawage,Mngeta hadi Tabora hakuna asiyefahamu.Habari zake zilijadiliwa sana hapa Hii ndege(5H-ZAI) ni ya nani na hufanya nini kwenye mbuga ya Selous?

Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015,ndege za huyu jamaa zilitumiwa sana na kambi ya Mzee Eddo.Safari za Arusha-Dodoma,au Dodoma-Dsm kampuni ya ndege ya huyu jamaa ijulikanayo kama Zantas Air,ndege zake zilitumika sana.Tulijadili ushirika wa Zantas Air katika kufanikisha kampeni za Mzee wa Monduli kuelekea Ikulu kwenye uzi huu Apson Mwang'onda na Timu yake waelekea Arusha kuratibu Mkutano wa Lowassa

Tunapokuwa tunampongeza Mh.Kigwangala kuanza vita ya "Ujangili",tusiache kumuonya na kumpa tahadhari kuwa vita hivi,visiwe na shinikizo la chuki za kisiasa na uadui wa kiitikadi,bali viwe vita vya kweli vyenye lengo la kuutokomeza mtandao wote wa ujangili.Asiishie kutaja tu nyumba za "Mawaziri Wakuu Wastaafu" zilizojengwa ndani ya kiwanja mali ya Taasisi ya wizara yake,bali atekeleze na ahadi zake za kuiwajibisha kampuni ya OBC ambayo ndani yake tunajua mabosi wake ndani ya chama na serikali wana maslahi nayo.

Si haba,alipoanzia si pabaya,aende mbele zaidi.Kingwangala asiishie kuwataja "majangili" wenye "uhusiano" na maadui wake wa kisiasa na kiitikadi,awataje pia wabunge wa chama chake na viongozi wa chama chake ambao kuna kampuni zinazotuhumiwa kwa ujangili zina mahusiano nao.Akiifikia hatua hii,tutakuwa pamoja naye na kumpa ushirikiano mpaka mwisho wa dahari.
 
Hii movie naombea tu iwe na nia ya dhati ya kupambana na ujangili kuliko kuwa kiki ya kisiasa.Huwa nashangazwa pia na jeshi la polisi kutokuchukua hatua za kiupelelezi na kupeleka wahalifu wakubwa kama hao mahakamani mpaka wapewe amri na viongozi wa kisiasa!!!!
 
Siwezi kupoteza muda kusikiliza ngonjera za kigwangala..mtu anayeishia kupiga mkwara bila vitendo..anayeishia kutajataja tu majina bila utekelezaji.. hiyo wizara ni ngumu sana..na yeye akitoka hapo basi atakayeingia ujue atamshutumu huyu wa sasa..wanaccm mliopo humu mwambieni Kigangwala kwamba asiiishie kutajataja tu majina bila utekelezaji..maana ccm kwa kusemasema tumeshawazoe
 
Mkuu hii vita sio yakitoto nakumbuka kipindi cha madawa ya kulevye nikiwa dodoma mtaa mmoja hivi nilikuta wakaka wawili wamekaa wanapiga story nami nikija as jiegesha kando yao walicho kijadili nilihisi huenda ni police
walisema file la madawa lipo central na nauye ni miongoni mwa waliopo na ndo maana kavuliwa uongozi na akaja vuliwa uwaziri.
kilichokuwa kibafata ni kuchukuliwa hatua tu
nimelikumbuka leo hili jambo ndo maana nakuambia kuaibishana wao kwa wao ni ngumu
 
barafu hamisi tunamjua sie wanashabihiana na makonda kitabia huanzisha jambo kubwa na mwisho wake haumaliziki ila tunaomba afanikiwe isiwe manza
 
Nimeipokea kwa namna "tofauti" taarifa ya kijana wangu Waziri Kigwangala juu ya kampuni za uwindaji zinazojihusisha na ujangili katika hifadhi na mapori yetu.Taarifa hii ni "nzuri" kwa upande mmoja kwa sababu Mh.Kigwangala amefanyia kazi yale mambo ambayo tuliyaleta hapahapa Jf(mimi barafu nikiwa mmoja wao) kuhusu wahusika wa ujangili na namna wanavyofanya kazi hiyo ya kufisidi wanyama wetu.

Baada ya Kigwangala kuingia katika wizara hiyo,nilimuandika "thread" hapa Jf ili aanze na majangili wa RUAHA NATIONAL PARK.Na hakika,katika watu au kampuni zilizotajwa,kampuni "sugu" ya ujangili katika eneo la Ruaha imetambulika,baada ya Kigwangala kuunda "Task Force" na kwenda kufanya uchunguzi katika vijiji na eneo la watu walio kando ya mbuga ya Ruaha.Uzi huo huko hapa Mh. Kigwangalla, karibu Maliasili na Utalii. Anza na hawa majangili wa Ruaha National Park

Kampuni nyingine iliyotajwa,inayomuhusisha kada na MNEC wa zamani wa CCM mkoa wa Kigoma,ilijadiliwa kwa mapana sana hapa JF,kabla hata Kigwangala hajawa Waziri wa Wizara husika.

Mjadala ule ulijadiliwa kwa kina sana na hakika watu wengi walitoa michango na mawazo yao na kuidokeza serikali mahali pa kuanzia juu ya hizi kampuni za "kihuni" zinazopukutisha mali-asili zetu kwa jina la utalii.Mtajwa na kampuni yake na mienendo yake juu ya shutma za ujangiri,zilijadiliwa kwenye uzi huu Hii ndege(5H-ZAI) ni ya nani na hufanya nini kwenye mbuga ya Selous?

Kampuni ya tatu iliyotajwa na Kigwangala,inamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF),hii ni kampuni ya kimarekani ambayo ina kampuni tanzu za uwindaji za Mwiba Holdings Tz Ltd,Tanzania Game Trackers Safaris Ltd na Wengerl Windrose Safaris Ltd.Kampuni hizi zote tatu zimetajwa na Mh.Kigwangala.Mjadala juu ya hawa FCF na ushiriki wao katika ujangili ulijadiliwa sana hapa JF kupitia uzi huu Nyalandu ahusishwa na Kampuni Inayotuhumiwa Kwa Ujangili

Sina shaka na tuhuma hizi za Mh.Kigwangala,na kila mtu aliye katika sekta ya utalii,anafahamu "tetesi" za ushiriki wa kampuni hizi katika masuala ya ujangili.

Kinachostua wengi,ni kwanini Mh.Kigwangala ameamua kutaja kampuni hizi tu katika tuhuma za ujangili?Je ni kweli hakuna kampuni nyingine "papa" zinazohujumu maliasili zetu huko porini zaidi ya hizi mbili?

Jf ikiwa ni sehemu ya mijadala huru na uchambuzi usio na mawaa,tunaweza kuanza kuangalia dhamira ya Mh.Kigwangala,ni kweli amekazana kabisa kuwamaliza hawa majangili?Maana kwa kinywa chake alituambia kufikia Januari 2018,kampuni ya OBC iwe imefunga virago na kuondoka,lakini mpaka sasa OBC wapo wanakula tu maisha kule Loliondo.Au ama ameanza na majangili tu ambao hawakuwa "upande wetu" wakati tunatafuta nafasi kielekea jumba jeupe?

FCF ambao wanamiliki hizo kampuni za uwindaji za Mwiba Holdings Ltd na nyenzake,ni kampuni ambazo zina "uhusiano" wa moja kwa moja na Lazaro Nyalandu,kampuni hizi zimekuwa kwa kasi wakati Nyalandu akiwa katika hiyo Wizara,chopa yao moja yenye rangi ya kijani ilitumiwa na Nyalandu katika kampeni za kuusaka Urais na baadaye Ubunge mwaka 2015,hawa FCF "walimdhamini" Nyalandu katika sehemu ya kampeni zake.Unapoitaja Mwiba Holdings Ltd na ujangili,unamtaja Nyalandu kwa njia ya nyuma ya pazia.Inawezekana hapa hatafutwi Mwiba Holdings Ltd pekee,hapa anatafutwa na "mwenyeji" wao.Mh.Kigwangala atuambie OBC ya Katibu wake imefikia wapi?

Unapoitaja Mkwawa Hunting Safaris Tz Ltd.Hii Mkwawa inamilikiwa na wale jamaa wenye Mkwawa Drinking Water na Mkwawa Rally Team kule Iringa,Hawa ndio wanamiliki kampuni ya ndege ya "Jambo Aviation",waliamua kujenga kabisa kakiwanja kao ka ndege huko Ruaha Nationala Park eneo la Madogoro ili wasafirishe nyara kwa urahisi.Kampeni za 2015,ndege yao ndogo aina ya C208 usajili wa 5H-AMH ilitumika kumsafirisha huku na kule "jasusi mkubwa" aliyekuwa anaisaka Ikulu ya Magogoni.

Unapoitaja Iringa na Ujangili,huwezi kumaliza orodha bila kutaja Wabunge wawili,mmoja Waziri kwa sasa na mwingine wa Jimbo la Mpakani mwa Iringa na Mbeya aliyejadiliwa hapa Mbunge wa Mbarali atuhumiwa kufukia pembe za ndovu eneo lake la uwekezaji na uzi mwingine huu Mbeya: Mtoto wa Mulla ambaye ni jangili amuua mtu aliyemhisi kumchongea, ajeruhi wengine na mwenzake akajadiliwa hapa https://www.jamiiforums.com/threads/iringa-katibu-wa-mbunge-wa-jimbo-la-isimani-akamatwa-katika-oporesheni-ondoa-ujangili.544391/. Hawa hushirikiana na mtumishi mmoja wa kanisa eneo hilo kwa miaka mingi.Hawa kina "Mkwawa" hujificha nyuma ya nguvu za kisiasa za hawa Wabunge.

Game Frontiers of Tz Ltd,imetajwa sana sana kwa miaka mingi,kada,mfadhili na MNEC wa mkoa wa Kigoma.Kuanzia mapori ya Kipiri,Likuyu,Likawage,Mngeta hadi Tabora hakuna asiyefahamu.Habari zake zilijadiliwa sana hapa Hii ndege(5H-ZAI) ni ya nani na hufanya nini kwenye mbuga ya Selous?

Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015,ndege za huyu jamaa zilitumiwa sana na kambi ya Mzee Eddo.Safari za Arusha-Dodoma,au Dodoma-Dsm kampuni ya ndege ya huyu jamaa ijulikanayo kama Zantas Air,ndege zake zilitumika sana.Tulijadili ushirika wa Zantas Air katika kufanikisha kampeni za Mzee wa Monduli kuelekea Ikulu kwenye uzi huu Apson Mwang'onda na Timu yake waelekea Arusha kuratibu Mkutano wa Lowassa

Tunapokuwa tunampongeza Mh.Kigwangala kuanza vita ya "Ujangili",tusiache kumuonya na kumpa tahadhari kuwa vita hivi,visiwe na shinikizo la chuki za kisiasa na uadui wa kiitikadi,bali viwe vita vya kweli vyenye lengo la kuutokomeza mtandao wote wa ujangili.Asiishie kutaja tu nyumba za "Mawaziri Wakuu Wastaafu" zilizojengwa ndani ya kiwanja mali ya Taasisi ya wizara yake,bali atekeleze na ahadi zake za kuiwajibisha kampuni ya OBC ambayo ndani yake tunajua mabosi wake ndani ya chama na serikali wana maslahi nayo.

Si haba,alipoanzia si pabaya,aende mbele zaidi.Kingwangala asiishie kuwataja "majangili" wenye "uhusiano" na maadui wake wa kisiasa na kiitikadi,awataje pia wabunge wa chama chake na viongozi wa chama chake ambao kuna kampuni zinazotuhumiwa kwa ujangili zina mahusiano nao.Akiifikia hatua hii,tutakuwa pamoja naye na kumpa ushirikiano mpaka mwisho wa dahari.
Ahsante kwa mchango ulioshiba hoja na vielelezo, ingawaje wale wa upande wa pili nawe umewataja kwa mafumbo tu. Kwa mfano " Jasusi mkuu aliyetaka kuingia magogoni 2015"=Benedicto, 'mtoto wa Mulla"=Mulla, "Waziri wa sasa" =Luk...., 'MNEC wa zamani Kigoma"=Sheni. Barafu, tunakuaminia sana kwa hoja zako za haja, usiwe mwoga, mbona jina unalotumia humu ni la bandia? Unaogopa nini sasa na upo upande wa kulinda rasilimali za nchi!!??
 
Ha ha ha ha umenichekesha sana mkuu CHLOVEK
Lakini we si Great Thinker?Si unaona umeelewa kwa urahisi?
 
Kigwangalla wizara imeanza kumshinda...

Alisema mwenyewe kuwa ataweka hadharani majina ya hao wanaotuhumiwa wa ujangili

Screenshot.png

Kilichotokea ameishia tu kuaambia polisi wakamate hao watu, na wasipowakamata ataenda kuwasemea kwa Rais.

Alipoingia kwenye hiyo wizara alikuja na mpango mzuri wakuboresha jinsi vibali vya uwindaji vinavyopatikana, ikiwemo kufanyiwa marekebisho mbalimbali na pia kutolewa kwa njia ya mnada, nakumbuka akaamua kufuta vibali vyote vya uwindaji ili waombaji wavipate kwa njia hiyo mpya. Here is the surprising thing, ikatolewa taarifa kuwa serikali imesitisha zoezi la kugawa vibali vya uwindaji for 2 YEARS, which means wale waliokuwa navyo wataendelea kuwa navyo kwa mfumo ule ule wa zamani. Baada ya hiyo move sijamsikia tena waziri akiongelea swala la vibali.

Hizo ni dalili tosha kuwa wizara imeshaanza kumwelemea na hakuna changes zozote za maana atakazoleta pale. Sasahivi anachofanya ni kudonoadonoa tu pembeni.
 
Mzee barafu kwanza shikomoo, japo sijui umri wako ila kwa hizi hoja zako inadhihirisha wewe ni mtu mzima na mwenye hekima zake!!

Sasa turudi kwenye mada!!!

Je una amini kwamba hii ni vita ya ujangili?

Je unakumbuka lile sakata la madawa? je liliishaje?

Kwangu mimi sioni kama ni vita vya ujangili bali ni vita vya kisiasa!!

Usitarajie atawagusa hao wana ccm wenzake!!

BTW prof wetu mmoja alisema akina Kinana ni majangili wakubwa kabisa....Kama ni kweli unadhan anaweza kumgusa kinana??
 
Kigwa kuna MTU anamtafuta hapo na ni Nyalandu maana ameanzisha vita baridi na jamaa kisa amehama ccm. Barafu Uzi wako ni mzuri sana ila vita hii haiwahuau maccm wenzake imelenga watu fulani fulani
 
Kigwangalla wizara imeanza kumshinda...

Alisema mwenyewe kuwa ataweka hadharani majina ya hao wanaotuhumiwa wa ujangili

View attachment 684788

Kilichotokea ameishia tu kuaambia polisi wakamate hao watu, na wasipowakamata ataenda kuwasemea kwa Rais.

Alipoingia kwenye hiyo wizara alikuja na mpango mzuri wakuboresha jinsi vibali vya uwindaji vinavyopatikana, ikiwemo kufanyiwa marekebisho mbalimbali na pia kutolewa kwa njia ya mnada, nakumbuka akaamua kufuta vibali vyote vya uwindaji ili waombaji wavipate kwa njia hiyo mpya. Here is the surprising thing, ikatolewa taarifa kuwa serikali imesitisha zoezi la kugawa vibali vya uwindaji for 2 YEARS, which means wale waliokuwa navyo wataendelea kuwa navyo kwa mfumo ule ule wa zamani. Baada ya hiyo move sijamsikia tena waziri akiongelea swala la vibali.

Hizo ni dalili tosha kuwa wizara imeshaanza kumwelemea na hakuna changes zozote za maana atakazoleta pale. Sasahivi anachofanya ni kudonoadonoa tu pembeni.
Aliwataja kina Huwel na Shein wa Kigoma na wenzake...Kwenye kutaja,ni kweli kawataja hao wachache,kaacha wabunge na makada wa CCM
 
Back
Top Bottom