Kigwangalla atakuwa waziri mzigo?

Kigwangalla atakuwa waziri mzigo?

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
HKigwangalla ameteuliwa kuwa naibu waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kipinidi cha 2015-2020. Rais JPM ametumia muda mrefu akichakata kile kilichoitwa na wafia chama kuwa ni 'mawaziri bora'. Tayari watanzania wamesahau kauli na majibu aliyotoa Mh. HKigwangalla juu ya wagonjwa kusongamana kwenye hospitali za umma, wakati wa mdahalo juu ya sera za vyama kwenye elimu na afya (MKIKIMKIKI). Alisema hizo ni kauli za kisiasa, na hakuna shida kama hiyo kwenye hospitali. Jibu hili lilikasirisha sana hadhira. Leo ni waziri katika sekta ambayo haamini kama kuna matatizo yanayosemwa na jamii.

Au la, HKigwangalla ukuje hapa na useme majibu yako yalikuwa ya kisiasa kutetea chama chako wakati ule hali ilipokuwa mbaya!

Dk Kigwangala apata wakati mgumu kuitetea CCM - Kitaifa | Mwananchi
 
Last edited by a moderator:
Aangalie sana network ya ukabila inayoanzia hapo alipo mpaka katika hospitali kubwa za umma. la sivyo ataanguka
 
JamiiForums mna maana gani kubadili kichwa cha mada yangu?! niliandika vizuri tu kuwa 'Kigwangalla atakuwa waziri mzigo, au Mungu asaidie' hapo kuna shida gani? wacheni watu wawe free kutoa mawazo, msilete zama za kale hapa! kama hamuwezi kuendesha jukwaa uzeni kwa wengine!
 
Last edited by a moderator:
Tusimhukumu kwa kauli bali matendo. Tuvute subira bado ni mapema.
 
Tusimhukumu kwa kauli bali matendo. Tuvute subira bado ni mapema.

leo ndio unaona haifai kuhukumu kwa kauli bila matendo? au ndio mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu.....??!
 
JamiiForums mna maana gani kubadili kichwa cha mada yangu?! niliandika vizuri tu kuwa 'Kigwangalla atakuwa waziri mzigo, au Mungu asaidie' hapo kuna shida gani? wacheni watu wawe free kutoa mawazo, msilete zama za kale hapa! kama hamuwezi kuendesha jukwaa uzeni kwa wengine!
Huna sababu za msingi kuja na hitimisho kuwa atakuwa waziri mzigo. Ndo kwanza ana siku nne tangu ateuliwe kuwa Waziri.
 
Heading yako yako ndo ilikuwa bomba
 
Huna sababu za msingi kuja na hitimisho kuwa atakuwa waziri mzigo. Ndo kwanza ana siku nne tangu ateuliwe kuwa Waziri.

historia yako inakuhukumu. ndiyo maana nikaandika "au Mungu asaidie"!
 
historia yako inakuhukumu. ndiyo maana nikaandika "au Mungu asaidie"!
Usifanye kumjua Mungu wakati kumbe humjui. Kumbe unajua Mungu ndiyo kila kitu halafu unatanguliza ya kidunia.
 
No reseach , no right to speak.

Heading yake ilimalizia "labda Mungu asaidie" ambacho naona ni kweli, hata Rais wetu, wewe, na wabunge wengine wanapoapishwa wanasema "Ee Mungu nisaidie". Hapo kama Great Thinker umenielewa.
 
Haipendezi, ni upumbavu na ulofa kuandika jambo lisilo na mshiko (ushahidi) hapa jamvini, hasa kumtuhumu binadamu mwenzio kwa mawazo na hisia tu. Kuna sehemu ya udaku upelekwe huko.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Katika mawaziri wapya walioleta minong' ono na waliolalamikiwa sana hapa jiji la Mwanza ni huyu Kigwangala. Kwa jinsi hata mimi ninavyomfahamu hatamfaa Magu lakini kwa vile Tanzania hakuna waziri anayezhindwa kazi, naye ataweza tu. Tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom