Kigwangalla aidharau ofisi ya CAG

NIYOMBARE

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
3,718
4,227
Akijibu swali la nyongeza la mbunge Halima alilouliza kuhusu ripoti ya CAG kueleza kuna mabohari ya dawa hayana viwango, Mh Kigwangalla alianza kwa kusema anakanusha vikali sio kweli kuna mabohari hayana viwango.

Wabunge wakamjibu ripoti ya CAG imesema akijibu kwa jazba kuwa "Hiyo ni ya CAG hapa nazungumza kama serikali". Hali hiyo ilipelekea Tulia kumuagiza akapitie ripoti ya CAG waangalie namna ya kurekebisha kwani wabunge walianza zomea zomea. Waziri wa afya akaahidi kupitia hiyo ripoti na kuleta taarifa bungeni.
 
Serikali yetu haithamini mchango wa CAG na hii imepelekea CAG kupewa pesa ndogo,tutegemee wizi mkubwa utakaofunikwa funikwa.Anyway tusubiri maendeleo baada ya kutumia nguvu kubwa kwa wapinzani.Nategemea waatkumbuka shuka asubuhi.
 
Akijibu swali la nyongeza la mbunge Halima alilouliza kuhusu ripoti ya CAG kueleza kuna mabohari ya dawa hayana viwango, Mh Kigwangalla alianza kwa kusema anakanusha vikali sio kweli kuna mabohari hayana viwango.

Wabunge wakamjibu ripoti ya CAG imesema akijibu kwa jazba kuwa "Hiyo ni ya CAG hapa nazungumza kama serikali". Hali hiyo ilipelekea Tulia kumuagiza akapitie ripoti ya CAG waangalie namna ya kurekebisha kwani wabunge walianza zomea zomea. Waziri wa afya akaahidi kupitia hiyo ripoti na kuleta taarifa bungeni.
Hajui kama realising fund ya donor huwa inarely kwenye hizo report za CAG.

Siajabu amesahau kuwa wizara yake ndio wizara inayotegemea misaada mikubwa ya financial resources kutoka kwa donor eg. Basket fund, Global fund.

Asubiri pia report ya special audt ya mamboya chanjo iliyofanywa Tanzania nzima aone hayo madudu yaliyopo ndani ya wizara yake ndo ajue CAG ni nani na ana mandate zipi!
 
Katika ofisi au taasisi za kiserikali naiamini ofisi ya CAG tu hata pccb sijawahi kuwamini
 
CAG ndio Roho ya nchi ......

Tulivyo na viongozi majizi si ajabu Sasa hivi tungekuwa tupo nyuma sana .......

Richmond....
Iptl.
Ligumi....
Escrow......

Yote ni CAG bila hivyo wangeweza kula hata pesa yetu ya mishahara.......

Waziri asiyemtambua CAG kwanza moja kwa moja kapoteza sifa ya kuwa Waziri.................
 
Huyo jamaa anapenda sifa sana
Kiburi kimemjaa na kujiona yeye ni zaidi ya wengine
Dharau zake zinampunguzia thamani
 
CAG ndio Roho ya nchi ......

Tulivyo na viongozi majizi si ajabu Sasa hivi tungekuwa tupo nyuma sana .......

Richmond....
Iptl.
Ligumi....
Escrow......

Yote ni CAG bila hivyo wangeweza kula hata pesa yetu ya mishahara.......

Waziri asiyemtambua CAG kwanza moja kwa moja kapoteza sifa ya kuwa Waziri.................
Nimeshangaa sana aliposema eti "ya CAG ni ya CAG hapa naongea kama serikali" hadi tulia na waziri kamshangaa ikabidi waweke mambo sawa
 
Back
Top Bottom