Kigwangalla awashushua wanaolilia ajira

kikuna

JF-Expert Member
May 26, 2015
2,573
2,802
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangalla amewakatisha tamaa watu waliokaa na kusubiri ajira za serikali hususani wale wa sekta ya afya kwa kuwaambia watafute kazi za kufanya badala ya kusubiri ajira.

Kigwangalla ametoa neno hilo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo alikuwa akitoa ushauri kwa watanzania hususani vijana kuhusu mambo wanayotakiwa kufanya ili wafanikiwe katika maisha ambapo alisema siri pekee ya mafanikio ni kuwa na mtazamo chanya katika maisha pamoja na kuwa na ndoto na malengo makubwa.

Katika mjadala huo ambao ulikuwa ukichangiwa na watu mbalimbali, mtu mmoja ambaye anajitambulisha kwa jina la Jackline Mwaipopo alimkumbusha Dkt. Kigwangalla kuhusu ajira kwa watu wa sekta ya afya, na kwamba wao kama wataalam wa sekta hiyo hivi sasa wanalazimika kufanya kazi nyingine nje ya sekta hiyo jambo ambalo linaathiri taaluma.

Katika majibu Kigwangalla alionesha kushangazwa na mtu wa aina hiyo, yaani aliyesoma na akapata shahada, halafu anakaa kusubiri ajira za serikali na kuyaita mawazo ya aina hiyo kuwa ni ya kizamani kama inavyoonekana hapa.
Katika mada yake Kigwangalla aliwataka watu wanaotaka mafanikio kuchakarika, kujituma na kuwa na tamaa ya vitu vikubwa huku akitoa kanuni za mafanikio

"Ukitaka kufanikiwa ni lazima ukubali kuamka mapema kama na mara tu alarm yako inavyokutaka. Hii inaimarisha 'willpower' yako! Watu waliofanikiwa huamka mapema halafu Mungu, mazoezi na baadaye chai. Kila kitu kikubwa huanza na ndoto kisha imani juu ya uwezekano wake wa mafanikio halafu mpango wa utekelezaji ambao ni utekelezaji halisi. Hata siku moja usiruhusu nguvu ya woga ikaishinda nguvu ya ndoto na tamaa ya kufanikisha jambo iliyo ndani yako" Alisema Kigwangalla.

Kwa wanaotegemea kusaidiwa, (Kushikwa mkono), Kigwangalla amewaeleza "Utashikwa mkono wakati ukiwa unajaribu kupambana kupanda mlima, siyo wakati unalia lia chumbani kwako!"

Hii ni sehemu ya mjadala kuhusu siri ya mafanikio

Kigwangalla%20twitter%203.JPG


Main sources EATV BLOG
 
Huyu jamaa atolewe kitengo japo kwa miezi 6 tu na apigwe ban kutumia savings zake katika benki anayopokelea mshahara kwa kipindi hicho kifupi tu ili tuone kama kweli ana jeuri ya kuishi katika hizo kauli za kusadikika alizotoa kwa wenzie. Kuongea rahisi sana...

Nadhani atapata maana halisi ya kwanini watu wazima wenye elimu zao wanalilia kuajiriwa!
 
Wanasiasa wanapenda kuharisha sana badala ya kuongea
Hapo anakua mahiri sana kisa anakula bila jasho kumtoka yaani kuongea ongea tu anapata pesa
 
Kama mtu ume plan kufanya biashara au kilimo kwa nn achome muda kusoma u dactar 5yrs then akose ajira akalime vitunguu kwel?bas pesa ya ada kuanzia form 6 hada ngazi ya degree asa ya u dactar angeanzisha msingi angefanya biashara kubwa sana sana....
 
Ni ushauri mzuri sana..
Hauwezi kulialia kuhusu ajira machoni pa wasiojali lolote juu yako!

[HASHTAG]#AmkaUangaze[/HASHTAG]
 
Hivi ukawa unajitahidi kuamka mapema kila siku, unaweza kuteuliwa kuwa waziri?
 
mbona na yeye aendi kulima hivi mtu asomee udaktari miaka 5 harafu umwambie akalime ni upuuzi
 
Huyu kapitiwa na upepo gan juz tuu katoka kujidai fb jinsi jk alipiga simu akaachiwa polisi usku wa manane leo kaja na jingne
[HASHTAG]#Alafu[/HASHTAG] Kujidai wakat una bosi ambaye anytime anakutupa kama tishu iliyotumika ni sawa na kucheka wakunga wakat una ujauzito......yy kama docter heb atwambia aliwah kujiajil vp maana sijawah skia hata kwamba aliwah miliki hata clinic![HASHTAG]#kuna[/HASHTAG] faida ya viongoz vijana na hasara pia zipo,yule mwngne kampa bendera mtoboa pua akakate viuno gabon kamuacha mpiga mbizi aliyeletea taifa heshima#afu anaambiwa ukwel kuwa kumpa bendera mvaa jinsi za kubana ilikuwa makosa yy badala ya kukubali kosa yaishe yy kapanick anatuma vijembe tuu kwa social networks!
 
Vitu kama ivi vinakera, lengo kuu la kusoma ni mtu kuajiriwa, ingelikuwa kujiajiri ningejiajiri tokea nikiwa mdogo.
 
Back
Top Bottom