Kigoma sio ndondocha

Inaonesha ni rahisi sana kuwafinyangafinyanga wana kigoma ukiwa umepata elimu kidogo. Yaani wapo km bendera

Haya matusi mnayowatukanaga watu wa Kigoma, Tabora, Lindi, mtwara na Singida mnajua madhara yake?
 
Mleta hoja umefilisika kimawazo tena ni mbumbumbu mkubwa,madhambi ya zitto ni yapi mbona mnaropoka hovyo tu,njoni na data hapa.
 
Hivi ndondocha ni sawasawa na bulicheka au nani ana Afadhali?
 
napata aina fulani ya kapicha hapa || hapa pana suala nature ya mkoa ktk husika na vuguvugu la kimaendeleo hasa ktk kujikomboa kuanzia zama hizo za miaka ya 50 || mwl j k nyerere ni kiongozi gani wa kigoma aliekuwa na mtazamo wa kweli na moyo wa haki na mwl jkn katika kudai UHURU? yaelekea mwl jkn aliwatambua watu hawa mapema infact hawa hawawezi kutofautiana na wakongoman kitabia hasa kutokana ujirani uliopo,hawatofautiani na wanamuziki wa kikongo na hulka yao ya kuhamia BENDI INGINE mara anapoona hali ya kimaslahi haimridhishi || HULKA || AU NATURE YAO TUSIWALAUMU SANA BY NATURE NI MUSICIAN JUST LIKE KONGOMEN
 
Kigoma tulihipokea ACT kwa mikono miwili, maana ndio Chama cha ukombizi dhidi ya wafanyabiashara ( Mbowe... ) malaya ( Slaa ), udini ( Lissu ), ukabila ( Mtei ), ukanda ( Lema ). Hiki ndicho chama chenye demokrasia ya kweli. Zitto ooooooo!!!

Je mnatumia akili zenu?
 

mmh! nina mashaka kama una uelewa na mambo ya siasa. Mbunge mmoja bungeni hawezi kuleta maendeleo jimboni kwake wala kuweza kuzuia agenda inayokwenda kuwaumiza wapiga kura wake, kazi ya mbunge ni kusema tu bungeni kuhusu mahitaji ya kwenye jimbo lake lakini utekelezaji wake utategemea 1. utashi wa serikali iliyoko madarakani, 2. bajeti iliyoko, 3. vipaumbele vya taifa 4. wingi wa wabunge wa kutoka vyama vya siasa. Kwani kama mbunge hoja yake ikipingwa na wabunge wenzake walio wengi atafanya nini peke yake? Kama serikali iliyoko madarakani ikikataa kupeleka miradi ya maendeleo kwenye jimbo fulani huyo mbunge wa jimbo atafanya nini peke yake? Kwasababu mbunge hana hela za kumudu kujenga hata kilometa 1 ya barabara kwa fedha zake. Ndiyo maana kunahitajika vyama vyenye nguvu na wabunge wengi wanaoweza kuisimamia serikali iweze kupeleka miradi ya maendeleo kwenye majimbo yote kulingana na mahitaji ya jimbo. Ndiyo maana UKAWA ipo ili kuhakikisha kuwa wabunge wa CCM (wengi bungeni) hawateki nyara hoja na mipango ya maendeleo ya majimbo ya wapinzani au kupitisha miswada inayokwenda kuwaumiza wananchi. Ndiyo maana hata CCM inasisitiza kwa wanachama wake wachague chama badala ya mtu, maana chama ndicho chenye sera, dira na mipango yote ya uendeshaji na utekelezaji hata kama mtu (mbunge) atafariki au kufukuzwa kwenye chama.
 
Mleta hoja umefilisika kimawazo tena ni mbumbumbu mkubwa,madhambi ya zitto ni yapi mbona mnaropoka hovyo tu,njoni na data hapa.

Data zipo, lakini data ambayo wewe ni rahisi kuielewa na kuikumbuka ni hii hapa: Zitto amedai kuwa chadema hakuna demokrasia ya kweli, inahubiri mambo ambayo itayatekeleza itakapokamata dola ambayo yoyo yenyewe haiyatekelezi ndani ya chama, hivyo chadema itawezaje kuchukua nchi?. Kwani chadema ni nini? chadema ni mkusanyiko wa viongozi, wanachama na wapenzi wake, Zitto alikuwa mwanachama na kiongozi muhimu wa chadema ambaye alipaswa kusikika kwa viongozi, wanachama na wapenzi wote wa chadema akishauri chama kuhusu mambo yasiofaa kwa demokrasia ndani ya chama kwa kutumia vikao halali vya chadema. Badala yake Zitto amesikika pale tu alipokuwa anajiandaa kufanya mapinduzi ya uongozi kwa njia zisizo rasmi. Ndiyo maana tunasema Zitto alikosea kwa makusudi sio kwa bahati mbaya, maana "kunguru hana kibiongo ukiona kibiongo ameinama anaokota kitu na kitu hicho kinaweza kuwa kijiti, kijiwe, nyama yako, nguo yako ya ndani, au kitu kingine cha thamani, hivyo wahi kumkurupusha kabla hajaruka nacho ukapata hasara". Ndiyo maana nawapongeza chadema kumkurupusha kunguru kabla hajasababisha uharibifu mkubwa.
 
Kigoma ni chimbuko la mapinduzi dhidi ya udhalimu ,kamwe si watu wa kupelekeshwa.
 
Ukiwa na uwezo mdogo wa kufikiri, unaweza kusema lolote linalokuja kinywani mwako bila kulitafakari kwanza. Haya tuanzie kwenye familia yenu kuna wasomi wangapi?

Una maana gani? what is the association?
 
Kwa mtu anayejua siasa ilivyo mkoa wa kigoma wala hawezi kuja kuwa mtabiri hapa. Wala hakuna mbunge mwenye uhakika wa kurudi na lolote linaweza kutokea.
 
Sasa hivi ni dhahiri kwamba Zitto ni mkabila na Chama chake kinaendekeza ukanda; kulikoni Leo Zitto Na ACT yake kuwatangazia vita wabunge walioko kigoma Na kwamba ili waendelee kuwa wabunge kigoma lazima wawe ACT!

Kama ACT ni Chama cha kitaifa kwa nini kisitangaze vita majimbo yote Au hata Na mikoa mingine ambayo ACT ina nguvu!

Jihadhalini sana Na Hiki Chama kwani pamoja Na kuwa ni Chama cha kisaliti pia ni Chama cha wana Kigoma!
Hivi ndivyo mwananchi(09.04.2015) inaripoti wakati ikihojiana Na Zitto kuhusiana Na mikakati yake Na Chama chake cha ACT.

Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kimejipanga kuyabeba majimbo yote.

Akizungumza na waandishi wa Mwananchi katika ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Zitto alisema ACT ni chama kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano wake mkuu wa hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na kufanya uzinduzi wa aina yake, huku akisisitiza kuwa chama hicho kinaungwa mkono na watu wengi.

“Tuna wagombea ubunge wengi wakiwamo wabunge wa sasa ambao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba hawatagombea kupitia vyama vyao vya sasa. Wapo ambao hawatakwenda hata katika kura za maoni za vyama vyao na wameshafanya uamuzi,” alisema.

Huku akizungumza kwa kujiamini, Zitto alisema wabunge hao ndiyo sababu ya chama hicho kuwa na uwezo wa kujiendesha na kufafanua kuwa ACT kinawakaribisha wabunge na makada wote kutoka vyama vya Chadema na CCM...


Kuhusu Kigoma

“Nahitaji majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na ACT bila kukosa hata moja na hili hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje ACT,” alisema Zitto ambaye pia alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge katika jimbo jingine lakini siyo Kigoma Kaskazini.

Kauli hiyo ya Zitto inawagusa wabunge wa sasa wa majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali (Muhambwe), Moses Machali (Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) na David Kafulila (Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na Peter Serukamba (Kigoma Mjini, Christopher Chiza (Buyungu) na Albert Obama (Manyovu) wa CCM.
 
Mleta hoja umefilisika kimawazo tena ni mbumbumbu mkubwa,madhambi ya zitto ni yapi mbona mnaropoka hovyo tu,njoni na data hapa.

Mkuu acha jazba, yeye mwenyewe Mkuu Wa Chama chenu kasema. Soma kwanza kabla ya kulipuka
 
Mleta hoja umefilisika kimawazo tena ni mbumbumbu mkubwa,madhambi ya zitto ni yapi mbona mnaropoka hovyo tu,njoni na data hapa.

MwajabuOmary, ina maana wewe huoni ushetani alioufanya?

yaani uko nyakageni halafu unapata kiu ya maji?
 
Last edited by a moderator:
Hope wamekusikia, wamekuelewa... Wanajua kuwa ZZK ni msaliti haaminiki hadi kijijini kwake.... anasingizia kukataa kiinua mgongo wakati wapiga kura wake wamekosa ada za kuwalipia watoto wao shule ... kwanini asiwalipie? nani asiejua kuwa 2010 ZZK alikuwa anampigia JK kampeni? ....

 
... Nani asiejua kuwa 2010 ZZK alikuwa anampigia JK kampeni? ....[/QUOTE]
Umesema kweli mkuu.
 

Naamini akili zako zimeliwa na kaswende ya ubongo nakushauri tafta daktari mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…