GE2025 Kigoma: Serikali kupitia mradi wa SEQUIP yatoa Shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule mpya mbili za sekondari

GE2025 Kigoma: Serikali kupitia mradi wa SEQUIP yatoa Shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule mpya mbili za sekondari

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Serikali Kupitia Mradi wa kuboresha Ubora wa Elimu Sekondari (SEQUIP) imetoa kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya ujenzi wa shule mpya mbili za sekondari zitakazorahisisha upatikanaji wa huduma za elimu mkoani Kigoma.

Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana Kigoma ambayo imejengwa katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma huku ikiwa imeanza kutoa huduma za elimu kwa wanafunzi.

Jumla ya Shilingi Bilioni 4.1 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana Kigoma ikiwemo maabara, vyumba vya madarasa na ofisi, Vyoo vya waliku na wanafunzi, mabweni, nyumba za walimu, Jengo la utawala, Bwalo, Jengo la TEHAMA, na Mashimo ya maji taka.

Pia serikali inaendelea na ujenzi wa shule mpya na ya kisasa ya Amali mkoani Kigoma ikiwa inajengwa katika Wilaya ya Kibondo kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1.6

Ukamilishaji huo wa ujenzi wa Shule mpya ya Amali ambayo inajengwa ni utekelezaji wa sera mpya ya elimu ya mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.
1752652028372.png

1752652041414.png

1752652062637.png

1752652078367.png
 
Back
Top Bottom