Kigoma: Polisi waua watatu kwa risasi

Kigoma: Polisi waua watatu kwa risasi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,162
Reaction score
64,509
Kigoma. Jeshi la polisi mkoani Kigoma limewaua watu watatu wanaodhaniwa kuwa majambazi huku wanne wakifanikiwa kukimbia.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 12, 2018 kamanda wa polisi mkoani humo, Martin Ottieno amesema tukio hilo limetokea juzi Agosti juzi 10, 2018 saa 5:30 usiku katika kijiji cha Kigina wilayani Kibondo mkoani hapa.

Amesema katika tukio hilo polisi walikamata risasi 69, bunduki aina ya AK 47 yenye usajili wa nchi jirani ya Burundi na magazine tatu.

Amesema watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi walimuua mkazi wa eneo hilo, Lukas Luchapa (38) aliyekuwa akitokea matembezini.

Amesema wakati wakipanga magogo barabarani kuzuia magari, alitokea mtu huyo na walimshambulia kwa risasi.

“Tulipata taarifa hizo na kwa kushirikiana na wananchi tulifuatilia na kubaini walikuwa saba,” amesema Kamanda Ottieno.

Amebainisha kuwa katika msako walioufanya walikutana na watu hao katika msitu uliopo karibu na kijiji hicho na kuanza kupambana nao.

Amesema polisi walifanikiwa kuwaua watatu huku wanne wakitokomea kusikojulikana
“Niwaombe wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi kwa kutoa taarifa watakapomuona mtu mgeni na kumtilia mashaka,” amesema.
 
Pongezi za dhati kwa huyu kamanda ila, angelipatikana mmoja tu aliyejeruhiwa akawataja hao wengine ningempongeza zaidi. Hao waliokimbia ujue ndio jipu baya zaidi kwani sasa wana kisasi na kamanda huyo.
 
Pongezi za dhati kwa huyu kamanda ila, angelipatikana mmoja tu aliyejeruhiwa akawataja hao wengine ningempongeza zaidi. Hao waliokimbia ujue ndio jipu baya zaidi kwani sasa wana kisasi na kamanda huyo.
Hizo ni mbinu tu za Medani Mkuu
 
Hivi polis wajifunza kuua tu. Utasikia " tumewakamata na baada ya kuwahoji wakataka kutupeleka waliko wenzao na njiani wakataka kutoroka chini ya ulinzi tukawapiga risasi na wakapata majeraha, majambazi hao wamefia njiani wakati tunawapeleka hospitalini" huo ndio umekuwa wimbo wa kila siku kwa jeshi letu.
 
b879cde1558737702585f829c3aa9c82.jpeg


POLISI mkoani Kigoma imewaua kwa kuwapiga risasi watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi na kukamatwa bunduki moja na risasi 69.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Kakonko. Alisema majambazi wengine wanne waliokuwa katika tukio hilo, wamekimbia.

Tukio hilo lililotokea juzi kijiji cha Kigina wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma. Kamanda Otieno alisema kuwa awali majambazi hao, walimuua kwa kumpiga risasi kichwani mwananchi mmoja wa kijiji cha Kigina, Lucas Luchapa ambaye walimkuta katika eneo ambalo walikusudia kuweka magogo kufanya utekaji, hivyo mwananchi huyo alihisi kuwa watu hao hawakuwa wema.

Aliongeza kuwa baada ya kuuawa kwa mwananchi huyo, polisi iliendesha msako na kuwazingira majambazi hao katika maeneo ya msitu wa kijiji hicho wakielekea mpakani na Burundi. Ndipo kukawa na kurushiana risasi, zilizosababisha vifo vya majambazi watatu na wengine wanne walikimbia. Kamanda Otieno alisema kuwa baada ya majambazi hao kukimbia, walikamata bunduki moja aina ya AK 47 ikiwa na risasi 60 zilizokuwa kwenye magazini tatu tofauti, huku bunduki hiyo ikiwa na usajili wa nchi ya Burundi.

Katika tukio lingine kamanda huyo wa Polisi alisema watoto wawili wa familia moja wamekufa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kushika moto na kusababisha vifo vyao. Alisema tukio hilo ni la Kijiji cha Kazage kata ya Shunguriba wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wakati watoto hao wakiwa ndani wamelala huku mama yao, Maombi John (25) akiwa amekwenda kisimani kuchota maji.
 
Ukarimu wetu unatutesa sana, hawa watu ni wakorofi mno mno nawaona huku mashambanii kukupiga panga hawaoni ajabu
 
Hizi nguvu wazitumie kupambana na nkurunzinza... Sio na watanzania
 
Makambi ya wakimbizi kigoma yamejaa watu wa namba hiyo...
 
Najarbu Kuwaza hao majambazi wangeingia anga za kamanda mroto. ..
 
Back
Top Bottom